Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kisumu District Mock- Kiswahili Paper 3 Question Paper

Kisumu District Mock- Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007



102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
FASIHI
JULY / AUGUST 2007
MUDA: SAA MBILI NA NUSU
JARIBIO LA TATHMINI YA PAMOJA WILAYA YA
KISUMU 2007
HATI YA KUHITIMU KISOMO CHA SEKONDARI
102/3
KISWAHILI
KARATASI YA TATU
JULY / AUGUST 2007
MAAGIZO
 Jibu maswali manne pekee.
 Swali la kwanza ni la lazima.
 Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani; (Tamthilia,
riwaya, na fasihi simulizi.
 Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
1. HADITHI FUPI: mayai waziri wa maradhi.
(a) Hadithi mayai waziri wa maradhi ni kielezo cha uozo miongoni mwa viongozi. Jadili.
(alama 10)
(b) Jadili maana ya ishara zifuatazo kama zilivyotumika katika hadithi (alama10)
(i) Milio ya bundi
(ii) Mzuka wa ukombozi
(iii) Alama (X)
(iv) Vitabu vingi vizito
(v) Watoto 10 wakondefu
RIWAYA
Z. Burhani: Mwisho wa kosa
Jibu swali la 2 au la 3
2. “Ninaona kama sisi ndio wazee wawili tu kama mahali hapa……
Naam, inaonyesha hivyo. Je, wewe umekuja kwa sababu ya mwanao?”
(a) Eleza muktadha wa dondoo. (alama 4)
(b) Eleza hatima ya mtoto wa mhusika wa pili anayezungumziwa. (alama 16)
3. Jumuiya ya mwisho wa kosa imeonyesha umuhimu wa utangamano. Fafanua kwa mifano
mwafaka kutoka kwa riwaya. (alama 20)
TAMTHILIA
4. Kithaka Wamberia: Kifo kisimani
Jibu swali la 4 au la 5
“Mlilifanya nini jiwe.”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Eleza yaliyolikumba jiwe hilo. (alama 10)
(c) Neno jiwe limetumika kijazanda. Taja na ueleze jazanda zozote zingine tatu zilizotumika
katika tamthilia. (alama 6)
5. Eleza jinsi Bokono alivyoukakamua mkono wake katika tamthilia ya kifo kisimani. (alama 20)
FASIHI SIMULIZI
6. (a) Taja mifano minane ya tanzu fupi katika fasihi simulizi. (alama 4)
(b) Fafanua sifa zozote tatu za mawaidha katika fasihi simulizi. (alama 3)
(c) Eleza umuhimu tatu wa ngomezi. (alama 3)
(d) Eleza istilahi hizi za fasihi simulizi. (alama 3)
(i) Maghani
(ii) Mapisi
(iii) Misimu / simo
(e) Fafanua sifa zozote tatu ambazo mtambaji wa hadithi anastahili kuwa nazo. (alama 3)
(f) Taja methali zozote mbili zilizo na dhana ya tashibiha. (alama 2)
(g) Eleza sifa zozote mbili za nyumba zinazotofautisha nyimbo na ushairi simulizi. (alama 2)
USHAIRI
7. Soma mashairi ya A na B kisha ujibu maswali.
A
Mtu ni afya yake, ndio uzima wa mtu
Mtu ni kuwa na chake, hakuwi ela kwa kitu
Mtu ni bahati yake, kupendekeza kwa watu
Mtu si fakhari kwako, kuitwa nyama ya mwitu
Mtu ni ulimi wake, kunena vyema na watu
Mtu ni kijungu chake, kuweka mawe matatu
Mtu ni mwenda kwa lake., mtoshawa na kula kitu
Mtu si uzuri kwake, kuitwa nyama wa mwitu
Mtu ni mwenye nadhari, apimaye kula kitu
Mtu ni moyo hariri, mwenye imani na watu
Mtu ni alo na ari, shika sana mwana kwetu
Mtu si yake fakhari, kuitwa nyama wa mwitu
Mtu ni mkono wazi, mtasadaku na watu
Mtu ni mwenye maozi, kuoneya kula kitu
Mtu ni alo tulizo, asopenda utukutu
Mtu si jambo pendezi, kuitwa nyama wa mwitu
Mtu ni mwenye ahadi, ndio u’ngwana na utu
Mtu ni alo baridi, mbembeleza wa watu
Mtu ni moyo asadi, asoonewa na mtu
Mtu si yake ifadi, kuitwa nyama wa mwitu
Mtu niliyoyanena, pima sana ewe mtu
Mtu sikuja tukan, kukirihi nyoyo watu
Mtu nakupa maana, wende nyendo za kiutu
Mtu si uzuri sana, kuitwa nyama wa mwitu
Mtu ni mtenda njema, atwiiye Mola wetu
Mtu ni mbele na nyuma, pima sana mwana kwetu
Mtu natiye khatima, fafanua kula kitu
Mtu si yake hisima, kuitwa nyama wa mwitu.
B
MTU HACHAGUI KAZI
Naamba kazi ni kazi, vyovyote vile iwavyo
Madamu si ubazazi, kwa mwanaadamu ndivyo
Kushona na upagazi, pia vile vyenginevyo
Kazi ni kitu azizi, wala vyenginevyo sivyo
Mtu hachagui kazi.
Mtu hadharau kazi, ile ahisiyo duni
Ayuzuie machozi, walilia jambo gani
Ukulima na ukwezi, na uvuvi baharini
Hizi nazo njema kazi, yafaa uzibaini
Mtu hachagui kazi
Si laiki kubughudhi, hakuna iliyo duni
Hayo makubwa maradhi, na tena uhayawani
Kazi zote zina hadhi, hivyo tusibagueni
Inafaa tuziridhi, tuzitende kwa yakini
Mtu hachagui kazi.
Ni wajibu kuipenda, na kuikiri moyoni
Na kwa dhati kuitenda, kwa juhudi na makini
Matatizo huyashinda, na uvivu kuuhuni
Hapo mtu atashinda, na magumu kumhuni
Mtu hachagui kazi
MASWALI
(a) Lipe shairi la A kichwa mwafaka. (alama 1)
(b) Kwa mifano mwafaka fafanua bahari katika shairi la A na B. (alama 4)
(c) Toa sababu za mwandishi kuchagua “Mtu hachagua kazi” kama kichwa cha shairi la B.
(alama 1)
(d) Mtunzi alikuwa na ujumbe gani katika mashairi haya? (alama 4)
(e) Andika ubeti wa pili wa shairi A katika lugha nathari. (alama 4)
(f) Eleza muundo wa shairi la B. (alama 4)
(g) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika mashairi haya. (alama 2)
(i) Nadhari
(ii) Ubazazi






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers