Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Laikipia District Mock- Kiswahili Paper 2 Question Paper

Laikipia District Mock- Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007



KARATASI YA V
102/2(Ufahamu, Ufupisho, Matumizi ya lugha na Isimu Jamii)
KISWAHILI
SWALI LA KWANZA –UFAHAMU
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Watu husema mengi kuhusu maisha, Wengine husema mtu anapozaliwa hatima yake huwa imeshaamuliwa na Mwenyezi na hata afanye nini hakuna wa kubadilisha, yaani kama majaaliwa yake ni awe mwizi stadi katika siku zake za halafu, basi atakuwa mwizi stadi bila shaka; kama majaaliwa yake ni awe daktari maarufu, basi atakuwa daktari mashuhuri, na kadhalika, Watu kama hawa wana msimamo sawa na ule wa raia wa Uyunani (Ugiriki) wanaoamini kuwa maisha ya kila binadamu yana sehemu mbili kuu: sehemu mbaya na sehemu nzuri.
Wayunani hawa w'anashikilia kuwa kila mtu lazima azionje sehemu zote mbili katika aushi yake na kwamba haiwezekani kuliepuka jambo hili. Watu hawa pia wanaamini kuwa miungu wao ndio wanaoamua maisha yao yatafuata mkondo gani. Yaani, wana imani kamili kwenye jaala eti kwa vile wino wa Mungu haufutiki.
Kwa bahati mbaya, humu nchini mwetu wapo watu ambao wanashiriki imani hiyo ya majaaliwa. Wao wanaamini kuwa wanapozaliwa, kazi yao kuu ni kuponda raha kwani hatima yao Mungu anaijua na hata wafanye nini hawawezi kuibadilisha. Kwa hivyo kazi yao hapa ni kukaa sambejambe na kuingojea hatima hiyo.
Ukipiga alinacha utagundua kuwa asilimia kubwa ya watu wanaishi katika ufukara mkubwa lakini si kwa sababu hayo ndiyo majaaliwa yao kama wanavyodai, lakini ni kutokana na tabia ya kufanya msirimbo miradi yote iliyo mbele yao.
Maisha si majaaliwa. Hutegemea mipango na juhudi. Mtu asipojibidiisha na kupanga maisha yake vilivyo, basi bila shaka mambo yatamwendea mvange na ataishia kuishi maisha ya ufukara wa sina sinani. Ukitazama binadamu wengi katika nyanja mbalimbali, utaona kuwa hawana utaratibu imara wa kuendesha maisha yao.
Chukua mfano wa vijana.Wao ndio waliokabiliwa vikali na tatizo hili. Wawapo shuleni, wengi wao hawana haja na elimu. Wanaamini kuwa shuleni ni pahali pa kuonjea utamu wa maisha huku wakingoja kubaleghe na kuoa au kuolewa. Wengi hujihusisha na vitendo vya ajabu kama kushiriki katika migomo. Sigara haziwatoki midomoni. Majira ya jioni hawapatikani tena shuleni kwani huwa wametorokea mijini na vitongojini kuponda raha. Dawa za kulevya nazo ndizo hizo. Wengine wanazielewa zote kwa majina hata wameshawahi kuonja kila sampuli ya dawa zenyewe. Si ajabu kuwa tayari baadhi yao ni wagonjwa wa ukosefu wa kinga mwilini. Wapo wale mahiri wa kufanya biashara yenyewe ya kusambaza dawa hizo za kulevya; walanguzi waliokubuhu hasa.
Kuwepo kwao- shuleni hakuhusiani kwa vyovyote na elimu. La hasha. Ni mahali tu kwa kusukumia miradi yao hiyo. Wengine ni majambazi. Wao hushirikiana na wavunja sheria wengine kupora mali ya wenyewe bila ya mtu yeyote kuwashuku. Haya yote huweza kuonekana kama yamepigwa chuku. Lakini ukikumbuka hivi majuzi
kifurushi kilichojaa bunduki kilipatikana chumbani mwa mwanafunzi mmoja chuoni, basi utaanza kuyaamini haya yote.
Wanafunzi wengine huifanya kazi yao kuu kuwa ile ya kuwahangaisha wenzao. Katika baadhi ya shule, wanafunzi hasa wa kidato cha pili hujihusisha na vitendo vya kuwadhulumu wenzao wa kidato cha kwanza.
Wengine wamefika kiwango cha kuwatisha na hata kuwapiga walimu wao. Wawapo huko nyumbani huwa ni balaa tupu, Baadhi yao huvaa mavazi ya ajabu. Kina dada huvaa nguo fupi kiasi kwamba utadhani wako uchi.
Ukiwauliza kisa na maana wanakujibu kuwa eti ndio.mtindo. Wengine huweka herini chungu nzima masikioni mwao na kujipaka rangi za kutisha midomoni. Wengine bila kusita hushirikiana kimwili na wavulana na hata wazee ambao huwafurahisha daima kwa darahima na zawadi kochokocho. Ugonjwa wa 'Ukimwi' si mgeni kwao. Sababu kuu ni kuwa wengine, hasa waliokulia mijini, wana mazoea ya kutembelea vilabu na kushiriki ulevi pamoja na ngono. Si ajabu kwamba baadhi yao wameenda jongomeo na wengine wako safarini kuelekea kuko huko. Wakikutana na kina dada watalii kutoka ng'ambo wanazuzuliwa na hizo ngozi zao nyeupe pepepe na kuapa kuwa nao pia ni lazima watakuwa kama wao. Wanafanya juu chini kutafuta ngwenje ili kujinunulia vipodozi aina aina vya kupaushia ngozi zao. Wasichana wengine hawasomi tena. Wametulia tuli kama maji mitungini humo majumbani wakiwanyonyesha wana wao waliopata kupitia harakati zao hizo.
Wavulana nao hawaachwi nyuma. Neno ‘nidhamu’ ni istilahi mpya kwao. Wao wanaishi leo, kesho itajililia.
Wengine nywele wameziacha kuwa matimtimu utadhani ni wajukuu wa majemedari wa vita vya Mau Mau.
Wamejitoboa mashimo chungu nzima masikioni ili wavae herini mbilimbili au tatutatu kulingana na mtindo uliopo. Wengine hata nywele wameonelea bora kuzisuka ili wafanane sawa bin sawa na akina dada. Na ili wasiachwe nyuma sana na kina dada hao, hawasahau kuvaa mikufu inayong'ara kuliko hiyo ya akina dada.
Nayo mitindo ya nguo huzihangaisha akili zao saa ishirini na nne za kutwa. Macho na masikio yao hukaa
chonjo kila dakika ili wafahamu ni mitindo gani mipya iliyoingia hasa kutoka ng'ambo kunakoishi wazungu wenyewe. Wengine nywele wameziweka 'kalikiti'. Suruali wanavaa zilizoganda mwilini utadhani zimewekwa gundi. Nao wengine wana mikururo ya marafiki wasichana. Ukiwauliza kisa na maana ya kutongoja hadi wakati ufike wanasema ndio mtindo. Ukiwauliza na 'Ukimwi je? Wanakuchezesha kayamba huku wakilumba kuwa Ukimwi ni porojo tupu; eti wamefanya vituko vyao miaka yote hiyo; inakuwaje hawajaenda na ulele ngoma?
Hata hivyo, kwa vile unga wa manga si dawaya chongo, baada ya pata shika zote hizo, kilichokuwa na mwanzo
kinaanza kufikia hatima yake. Ukweli unaanza kuchukua mahali pake. Muda ambao wangetumia kujizatiti kwa
minajili ya siku za baadaye wanashtukia ghafla kuwa tayari umeshawapa kisogo. Majuto na mikasa inawafuata unyo unyo.
Ni muhimu sana vijana kufungua macho yao ili kuona mwanga.Wanafaa kuelewa fika kuwa ujana ni moshi tu.
Dakika hii upo, dakika nyingine ushatoweka. Mungu alipoamua kuwa kila binadamu ni lazima apitie ujanani alikuwa na sababu maalumu. Ujana ni kipindi cha maisha cha kujifunga masombo kwa majukumu ya baadaye.
Ni kipindi cha kujitafutia maarifa tunu. Iwapo hali ni kinyume, basi mambo hayana budi kwenda mrama
Maswali
1. Ipe taarifa hii kichwa mwafaka. (alama 1)
2. Eleza msimamo wa watu wengi imani kwenye jaala. (alama 2)
3. Taja vitendo vyovyote vinne vinavyoonyesha upotovu miongoni mwa vijana. (alama 4)
4. Kutokana na taarifa; eleza jinsi vijana wanavyo ambukizwa ugonjwa wa ukimwi (alama 3)
5. Unadhani ni mambo yapi mengine yanachangia tabia potovu kati ya vijana? (alama 2)
6. Toa maana ya: (alama 3)
(a) Kufanya msirimbo
(b) Unga wa manga si dawa ya chongo
(c) Kwenda mrama
MUHTASARI
Soma habari ifuatayo kasha ujibu maswali
Miaka mingi ya kutawaliwa na wakoloni iliwafanya wananchi wengi kupuuza umaarufu na uadilifu wa lugha ya kiswahili kama lugha ya taifa kwa manufaa ya kuarifiana habari mbalimbali kwa ufasaha na kuelewana vema.
Wakoloni pia waliwashawishi wananchi waone kwamba lugha ya Kiswahili ni kwa ajili ya watu wale wasiokuwa na elimu na kwa wale ambao hawajastaarabika. Kwa wale ‘wenye’ elimu na wastaarabu’, wakoloni waliwashawishi kuamini kwamba lugha ya kigeni, yaani kiingereza, ndivyo hasa lugha inayofaa kwa kujieleza na kufahamisana habari.
Kutokana na vikwazo hivi si ajabu kuona hadi hivi sasa, mwananchi halisi akijitwaza kwamba hawezi kujieleza kwa ufasaha au kumpasha mwenzie habari kwa ukamilifu mpaka atumie lugha ya kingereza. Hata katika maofisi mengine ya serikali, hadi hii leo, japo imesha kupitishwa kisheria kwamba Kiswahili ndiyo lugha ya taifa, bado utawaona wanaona wananchi wengine wanapendelea kuzungumza kiingereza wao kwa wao, ili wajulikane kwamba wana kisomo na wamestaarabika.
Vikwazo vya namna hii vimewalemea wananchi vile vile kwa upande wa magazeti. Utaona mwanainchi ambaye anafahamu kiingereza kidogo sana, akijinunulia gazeti kubwa la kingereza na kuanza kuzurura nalo kutwa nzima bila kuambulia mengi ndani yake. Pia utawasikia wananchi wengi wakijidai kwamba hawataki kusoma magazeti ya Kiswahili kwa sababu inakuwa vigumu kwao kuelewa mambo yaliyomo kama vile ambavyo wangelielewa katika gazeti la kiingereza.
Mabeberu wamesha tugundua kwamba tunao upotofu wa aina hiyo, ndipo utaona mara nyingi wanawaletea wananchi magezeti mengi ya kiingereza, mengine yakiwa na nia ya kuwapotosha wakijua kwamba watayasoma tu, mradi yameandikwa kwa lugha la kiingereza.
Mara nyingi taifa fulani la kibeberu likitaka tuchukiane na taifa jingine fulani ambalo ni adui yake kisiasa au kiuchumi, taifa hilo la kibeberu linaandika habari za uchochezi kwenye magazeti yao ya lugha ya kiingereza, mambo kuhusu taifa lile adui yake (ambalo si adui yetu). Magazeti hayo huandikwa kwa lugha nadhifu ya Kiingereza na kuletewa wananchi hapa nchini. Maskini wananchi wengine waliotopea kwa kudhani kiingereza ndicho lugha nzuri ya kigazeti, wanayanunua mara moja na kuanza kuyasoma magazeti hayo, na pia kuwapa watoto wao wasome. Matokeo yake ni kwamba, bila kujitambua, wanajikuta wanafanya yale Mabeberu waliyotarajia wayafanye, yaani wanaanza kuchukiana bure na taifa lile ambalo ni adui wa Mabeberu hao, lakini si adui zetu.
Madhumuni ya kuandika habari kwenye magazeti, ni kutaka kuwafahamisha wasomaji mambo
yaliyotokea au yatakayo tokea siku hata siku,kwa lugha inayofahamika na kueleweka kwa urahisi bila kumtatiza masomaji ikiwa basi ndiyo madhumuni, kuna haja gani kutumia lugha ya kigeni ili kuwaelezea wasomaji wako jambo ambalo wangaliweza kueleza kuelezwa kwa lugha yao wenyewe ambayo wanaielewa vyema. Mtu aelezewapo jambo lenyewe kutoka moyoni na akilini kwa njia adili ambayo anaifahamu vyema
undani wake, huelezea jambo pia wasomaji wake wataielewa kwa ukamilifu. Kwa ujumla jambo ambalo mwandishi huyo ataliandika kwa lugha ambayo ni ya asili yake na ambayo anaielewa vyema, halitamtatiza
msomaji wake ambaye pia anaielewa vyema lugha hiyo.
Maswali
(a) Fupisha aya tatu za mwanzo (maneno 30-40) (alama 6)
Nakala chafu
Nakala safi
. Taja mambo muhimu yaliyoshughulikiwa katika aya ya nne hadi ya sita (Maneno 50-60)
(alama 6)
Nakala chafu
Nakala safi
3.
4. MATUMIZI YA LUGHA
(a) Weka nomino hizi katika ngeli lake. (alama 2)
(i) Mvule
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
Kipofu
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
(b) Tunga sentensi kuonyesha matumizi ya parandesi (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
(c) Andika sauti mbili zinazotamkiwa menoni (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
(d) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutummia jedwali.
Mwanafunzi huyu mwerevu atapita mtihani vyema. (alama 4)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
(e) Andika katika kauli ya kutendesheka. (alama 2)
(a) Iga
…………………………………………………………………………………………………………
(b) Vaa
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………
(f) Onyesha aina ya vitenzi katika sentensi.
Wewe umewahi kufika shule ukiwa umechelewa? (alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
(g) Andika kulingana na maagizo yaliyotolewa. (alama 2)
Jina langu ni maliki lakini huitwa mali kwa kifupi. (Anza kwa: Watu -----------)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
(alama 2)
(h) Kwa kutunga sentensi eleza tofauti kati ya:
Sentensi ambatano na sentensi changamano
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
(i) Onyesha aina za virai katika sentensi (alama 2)
Gari lao lilianguka kando ya jengo.
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………..
(j) Unda vivumishi kutokana na vitenzi : (alama 2)
(i) Samehe
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
(ii) Kakamaa
…………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………
(k) Eleza matumizi ya viambishi vilivyopigiwa kistari. (alama 3)
(i) Kaandika barua
…………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………
(ii) Nikisoma kwa bidii nitapita mtihani
…………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………
(iii) Oliech acheza mpira vizuri
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………
(l) Kanusha.
(i) Wakimenyanamenyana (alama 1)
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
Ningefika mapema ningewahi basi hilo (alama 1)
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………
(m) Onyesha aina za mofimu zilizopigiwa kistari. (alama 2)
Alisita alipofika chumba cha sita
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………
(n) Tunga sentensi kubainisha: (alama 2)
(i) Inchi
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………
(ii) Nchi
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………
(o) Sahihisha sentensi ifuatayo.
Mkutano uliyohairishwa juma lililopita utafanywa leo (alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
(p) Andika katika usemi wa taarifa:
“Nikifaulu nitamshukuru sana Mungu pamoja na wazazi wangu.” Mungai alisema. (alama 3)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
(q) Andika katika wingi:
Kuku wa jirani kijijini mwetu aliangua kifaranga aliyelemaa. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………
Isimu jamii (alama 10)
Taja na ueleze njia tano zinazochongia maenezi ya lugha ya Kiswahili nchini.
(alama 10)






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers