Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Nandi North District - Kiswahili Paper 2 Question Paper

Nandi North District - Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007



Name………………………………………………… Index No. …………………….
School ………………………………………………...
102/2
KISWAHILI
KARATASI LA 2 (LUGHA)
JULAI / AGOSTI. 2007
MUDA: SAA 2 ½
MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA NANDI KASKAZINI -2007
Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya
102/2
KISWAHILI
KARATASI LA 2 (LUGHA)
JULAI / AGOSTI. 2007
MUDA: SAA 2 ½
MAAGIZO KWA MTAHINIWA
• Andika jina lako na namba yako katika nafasi uliyoachiwa hapa juu.
• Jibu maswali yote. Majibu yako yaandikwe katika nafasi zilizoachwa katika kijitabu hiki cha maswali.
ambazo zimerahisesha mawasilano.
2
Karatasi hii ina kurasa 12 zilizopigwa chapa
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo.
SOMA MAKALA KISHA UJIBU MASWALI
Bi mwenyekiti , wataalamu wa lugha, waamuzi na washiriki waliojumuika kwenye mdahalo, mabibi na mabwana. Si vema niwapotezee wakati wenu kutetea mjadala kwa madhumuni ya kuteta tu. Sijaja hapa kupiga makelele mithili ya mbwa mdomo wazi (makofi). Nimefika hapa kuwaandalia hoja madhubuti zitokanazo na kina cha mawazo na maoni murua moyoni mwangu. Mada ya mjadala inasema kuwa Kiswahili inatosheleza matakwa yote kimawasiliano.
Bi mwenyekiti, Swali tunalopaswa kujiulizwa ni, Je, mawasiliano ni nini? Fafanuzi mbalimali
zimetolewa. Aidha wavumbuzi wa kisayansi / kiteknolojia wameasisi mbinu za kisasa zinazorahihisha mawasiliano na kuufanya ulimwengu kuwa kama kijiji. Tukijikita kwenye muktadha wa mjadala huu, twaweza
tukaafiki kwamba mawasiliano ni kupasha ujumbe namna unavyoeleweka na mpokezi. Hivyo ni kusema
kwamba mja aweza akatumia lugha, ishara au alama kumfikishia mwenzake ujumbe uliokusudiwa. Pindi
mpokezi akosapo ufahamu wa jambo linaloangaziwa, basi hapo mawasiliano yatakuwa muhali.
Mawasiliano huwezesha makabila mbalimbali kutangamana huku yakiendeleza biashara. Maazimio na miradi ya taifa yaweza kusambazwa kotekote kwa Kiswahili kupitia radio, magazeti na runinga. Huu ni ukweli
wa wazi usiopingika. Kiswahili bila shaka, chajitosheleza kimawasiliano.
Bi mwenyekiti, niliyoyadokeza yana ithibati. Naomba kutajiwa muktadha wowote, si nyumbani, si ofisini, si kanisani ambamo mawasiliano kwa Kiswahili yangekwama. Duru za kuaminika zashikilia kuwa mtaalamu wa tarakilishi ulimwenguni, Bill Gates, ameunda mitambo itumiayo misamiati na lugha ya Kiswahili. Ajabu!
Bi mwenyekiti, hawa wapinzani wana upungufu mmoja, nao ni yamkini hawajimudu katika lugha ya Kiswahili. Wanatumia upungufu wao huo dhidi ya mjadala unaojitetea wenyewe. Mmoja wa wanenaji amejikanganya na kujipinga kwa kusema, “mwacha mila ni mtumwa.” Kauli hii inazidi kuthibitisha kuwa Kiswahili kina ukwasi wa kutosheleza mawasiliano. Wapinzani wangekuwa weledi wa Kiswahili wangegundua kuwa usemi huu unaafikiana na mjadala (makofi). Ama kwa kweli fumbo mfumbie mjinga, mwerevu
atalifumbua! Aidha uneni usisitizao kuwa “Alalaye usimwamshe, ukimwamsha utalala wewe” unao mashiko.
Bi mwenyekiti, tamati nimefika nikiwasihi wenzangu wasisite kuvuka sakafu ili tuufanikishe mjadala. Asanteni.
a) Upande wa upinzani ulishikilia mada ipi? (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………………
b) Msemaji wa upinzani amejikanganya anapotumia msemo: “Mwacha mila ni mtumwa .” Fafanua.
(alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
c) Mwandishi anasema, “Alalaye usimwamshe ukimwamsha utalala wewe.” Thibitisha ukirejelea
muktadha wa hotuba uliyoisoma. (alama 4)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
d) Kunapatikana shangwe (makofi) zaidi ya mara moja katika taarifa. Eleza chanzo cha shangwe hizo.
(alama 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
e) Mbali na mbinu za mawasiliano zilizozungumziwa katika taarifa, zitaje mbinu nyingine za kisasa
(alama3)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
f) Ukirejelea kifungu, eleza maana ya msamiati huu:
(i) Yamkini----------------------------------------------------------------------------------
(ii) Ithibati-----------------------------------------------------------------------------------
(iii) Muhali-----------------------------------------------------------------------------------
2 UFUPISHO
Soma makala haya kisha ujibu maswali.
Aibu kubwa ya taifa kushindwa kukabiliana na tatizo sugu la ajali za barabarani bado inaendelea kuwafedhehesha wahusika katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano licha ya matumizi ya vidhibiti mwendo na kanda za usalama.
Ajali za baraza barabarani zinaangamiza idadi kubwa ya watu kila mwaka wakiwemo viongozi na
watu mashuhuri.Miongoni mwa sababu ambazo zinaleta maafa barabarani ni pamoja na uendeshaji kasi kupita
inavyotakikana, yaani kukiuka masharti yaliyowekwa na wizara ya uchukuzi na mawasiliano.Madereva wengi hung’oa vidhibiti mwendo vilivyowekwa, hawarekebishi mikanda ya usalama, wala hawayapeleki magari yao kukaguliwa mara kwa mara kama inavyopaswa. Yale yanayopelekwa kwa ukaguzi, mengi hushindwa kutekeleza kanuni zilizowekwa kwa hivyo hutegemea hongo kuwa barabarani.Fauka ya hayo, madereva wa malori na matrela mara nyingi huendesha magari hayo wakiwa walevi. Dawa za kulevya, kama miraa na bangi hutumiwa sana na hawa na matokeo yake huwa ajali mbaya.
Hata hivyo, lawama haiwezi kuelekezewa madereva pekee. Ukiangazia barabara nchini Kenya
utapata kuwa barabara haziko katika hali nzuri. Zile za lami zimekuwa na mashimo
makubwa ambapo mvua ikinyesha hufanya vidibwi mithili ya michimbo ya madini yaliyojaa maji
baada ya kuachwa wazi. Na zile barabara zisizokuwa na lami zimeharibika kiasi kwamba ni vigumu kuzitofautisha na njia za ng’ombe kwenye maeneo kame kinachohitajika kuzirudisha katika kiwango ambacho zitaweza kufaa tena.
Wananchi pia inafaa waelimishwe ili wasikubali kupanda magari ambayo tayari yamejaa. Hili litawasaidia wananchi wenyewe kudumisha usalama wao barabarani. Pia inawafaa watambue ya kwamba wanajukumu la kuwaarifu walinda usalama endapo dereva anaendesha kwa kasi kuliko ile ya kilomita themanini kwa saa iliyokubaliwa.Inafahamika kuwa maafisa wa usalama ndio wafisadi zaidi, hivyo basi huchangia katika kuongeza idadi ya vifo barabarani. Katika vita vya ufisadi na ajali za barabarani ni mwananchi mwenyewe ambaye atawezesha kukomesha hali hii. Kwa mfano, afisa wa usalama akipatikana akichukua hongo, yeye pamoja na yule aliyetoa hongo wakamatwe na kupelekwa kwenye vituo vya kukabiliana na ufisadi na kuchukuliwa hatua kali, matatizo haya yataisha. Lakini kabla kufikia hapo, ni muhimu kumhamasisha mwananchi kuhusu haki zake na namna ya kukabiliana na suala hili la ufisadi. Hali hii inatuonyesha kwamba mipango maalum inapaswa kufanywa na serikali ili kuwaelimisha wananchi kama hatua ya kwanza yakukabiliana na ufisadi hatimaye izilainishe sekta zote wala si ya uchukuzi na mawasiliano pekee.
(a) Eleza mambo yote muhimu anayozungumzia mwandishi katika aya ya pili na tatu.
(maneno kati ya 45-50 Alama 7)
Matayarisho:-
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
Jibu:
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
4
(b) Bila kubadilisha maana iliyokusudia, fupisha aya mbili za mwisho.
Maneno kati ya 35-40 (alama 05)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
Jibu:
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
Utiririko alama 3 (jumla).
3 MATUMIZI YA LUGHA.
a) Onyesha kitenzi kikuu na kisaidizi katika sentensi hii.
Nimewahi kumkumbusha makosa yake. (al 2)
b) Umepewa aina tofauti za nomino. Tunga sentensi idhihirishayo kila aina ya nomino;
(al 3)
i. Nomino ya wingi
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
ii. Nomino ya kitenzi jina
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
iii. Nomino ya kipekee
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
c) Tunga sentensi kutofautisha maneno haya. (al 2)
(i) Dhamini
(ii) Thamini
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
d) Tunga sentensi kuonyesha matumzi ya viakifishi hivi.
(i) Alama hisi (al 1)
……………………………………………………………………………………………………………
(ii) Parandesi (Al 1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(iii) Alama za mtajo / usemi (Al 1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
e) Andika konsonanti mbili zinazotamkiwa kwenye ufizi. (al 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
f) Eleza maana ya msemo huu.
Maisha ya kitwea (al 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
g) Geuza vitenzi vifuatavyo viwe katika kauli ya kutendeana, kisha uvitungie sentensi.
(i) Ja (al 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(ii) Pa. (al 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
h) Eleza maana mbili ya “La” (Al 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(i) Unda vitenzi viwili kutokana na kila moja ya majina
(i) Mtukufu (Al 1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(ii) Mchumba (Al 1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
j) Tumia – ndi- pamoja na viashiria vya ngeli kujaza pengo (Al 2)
(i) Wewe ninayekufuta.
(ii) Nyingi mnaoongoza.
k) Andika kinyume cha;
(i) Tandaza zulia kubwa (Al 1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(ii)Mtweke mchukuzi mzigo huu. (Al 1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
l) Vitaje vipashio vitatu muhimu vya lugha. (Al 3)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
m) Andika kwa msemo wa taarifa (Al 3)
“Lo! Umeweza kuubeba mzigo huu pekeyo?”
Mama alishangaa.
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
n) Tumia “O” rejeshi katika sentensi zifuatazo (al 2)
(i) Mikeka ambayo hufumwa Turkana ni madhubuti.
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(ii) Uchunguzi ambao wangojewa umewadia.
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
o) Eleza matumizi ya “KU” katika sentensi hii.
Kucheza huku hakufai (AL 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
p) Tofautisha nyakati (Al 2)
(i) Akimbia
(ii) Anakimbia
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
q) Onyesha kishazi huru na tegemezi katika sentensi hii (Al 2)
Anamolala mna viroboto wengi.
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
ISIMU JAMII
Wananchi huoyee! Kiti juu!
Leo ni ile siku tuliyoingojea kwa hamu na ghamu. Imefika, haijafika? Naona nyuso zenu zinatangaza
ushindi wa kiti.Naona hamjadanganywa na mpinzani wangu atembeaye na kupaka matope jina langu. Ni nani hajaona maendeleo niliyoleta hapa tangu mnichague nyinyi wenyewe? Kwa hiari yenu mlinichagua niwe mtumishi wenu nami niko chini ya nyayo zenu. Sasa huu ni wakati mwingine naomba, nawasihi,
nawanyenyekea mnikabidhi tena hilo jukumu zito la kuwatumikia.
Mpinzani anawapa pesa kuwahonga, ela nasema kula kwa mpinzani wangu, lakini kura ni kwangu jamani. Kiti juu!
Maswali
A Taja muktadha wa matumizi ya lugha hii (Al 2)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
B Eleza sifa za lugha hii . (Al 4)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
C Jadili mbinu za lugha zilizotumika katika lugha hii . (Al 4)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers