Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Nandi North District - Kiswahili Paper 3 Question Paper
Nandi North District - Kiswahili Paper 3
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2007
Name………………………………………………… Index No. …………………….
School ………………………………………………...
102/3
KISWAHILI
FASIHI
KARATASI LA 3
JULAI / AGOSTI. 2007
MUDA: SAA 2 ½
MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA NANDI KASKAZINI -2007
Hati ya kuhitimu Elimu ya Sekondari Kenya
102/3
KISWAHILI
FASIHI
KARATASI LA 3
JULAI / AGOSTI. 2007
MUDA: SAA 2 ½
MAAGIZO
• Jibu maswali manne.
• Swali la kwanza ni la lazima.
• Usijibu maswali mawili kutoka katika kitabu kimoja.
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo.
SEHEMU YA A
SWALI LA LAZIMA
Lisome shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
1. Naruka mithili ndama, nikiwajuza ujumbe
Mnisikie waimama, vichwa msije kavimbe
Shikeni haya daima, yawape tiba ya tembe.
2. Mbona wengi twalalama, kuhusu mola
muumbe?
Yakini hatuna wema, dini twaiweka ombe
Tushike kweli hekima, Mungu mmoja
tuombe.
3. Dini yangu waisema, kwa kuipiga vijembe
Wewe wajiona kama, ulo wahedi kiumbe
Na’budu Mungu wa mema, haujui hivyo
kiumbe.
4. Kanisani tuna ngoma, kucheza sisite
chembe
Kumpe Yesu heshima, divai twanywa
kombe
Mbona kashifa e mama, Zikatazo kama
wembe
5. Nakwambia sasa koma, ama tukuite
ng’ombe
Vijijini wanisema, “Yeye mumini
mzembe”
Hivyo hakina ungama, hayo mabaya
siambe?
6. Mbona wafanya unyama, wataka vipi
niombe?
Naomba nikisimama, siketi ili niimbe
We kusini watazama, ili mola ukaomba.
7. Ninafungeni nudhuma. Metamatika ujumbe
Tuacheni uhasama, nawaombeni viumbe
Mola awape neema, kiumini sijitambe.
Maswali
a) Shairi hili ni la bahari gani? (alama 2)
b) Ni ujumbe upi muhimu unaopatikana katika shairi? (alama 2)
c) Uandike ubeti wa tatu katika lugha ya nathari. (alama 4)
d) Zieleze arudhi zilizozingatiwa katika kulitunga shairi hili. (alama 5)
e) Ni onyo gani mzungumziwa anapewa na mshairi? (alama 2)
f) Kwa nini mshairi ametumia maneno “Muumbe” na “Na’budu”? (alama 2)
g) Vifafanue vifungu hivi kama vilivyotumiwa katika shairi: (alama 3)
(i) Kiumini sijitambe
(ii) Kwa kuipiga vijembe
(iii) Zikatazo kwa wembe
SEHEMU B: RIWAYA ( MWISHO WA KOSA)
2. “Alikwenda moja kwa moja kwake, akajitupa juu ya sofa na kuachia machozi yamtirike kama
yalivyotaka. Kwa mara ya kwanza alifurahi …..”
a) Ueleze muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Kieleze kisa cha mhusika katika dondoo hili tangu mwanzo hadi mwisho. (alama 12)
c) Kwa kutumia mifano katika sura hii, jadili swala la ufisadi kama linavyoshughulikiwa.
(alama 4)
AU
3. ‘Udungu ni kufaana, sio kufanana’. Jadili ukweli wa kauli hii kwa mujibu wa riwaya ya Mwisho wa
Kosa. (alama 20)
SEHEMU YA C: TAMTHILIA ( Kifo Kisimani)
4. Inaonekana kuwa makofi hayajakutosha, hata mengine nitakufanyia kama nyongeza…. Hii itakuwa
siku muhimu kwako. Itakuwa siku ya furaha isiyosahaulika.”
a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Eleza tabia za msemaji. (alama 6)
c) Dhihirisha umuhimu wa msemaji katika kukuza dhamira ya mwandishi. (alama 5)
AU
5. Jadili Maudhui yafuatayo
i) Ujasiri (alama 8)
ii) Usongombwiko / unafiki ( alama 8)
iii) Uasi (alama 4)
SEHEMU YA D: HADITHI FUPI
(Mayai waziri wa maradhi)
6. a) Alipokuwa nyumbani pekee, Mayai waziri wa maradhi alizitazama picha zilizomwonyesha maisha yake katika hatua mbali mbali. Taja na ueleze zozote tano. (alama 10)
b) Kwa kurejelea kitabu Kizima cha Mkusanyiko wa hadithi, Mayai waziri wa maradhi na hadithi zingine, Jadili maswala yoyote matano ibuka. (alama 10)
SEHEMU YA E – FASIHI SIMULIZI
7. Huku ukitoa mifano, linganisha na kutofautisha vipera vifuatavyo vya fasihi simulizi.
(alama 20)
i) Hekaya na hurafa
ii) Ngano za usuli na visasili
iii) Ngano za mtanziko na ngano za mazimwi
iv) Miiko na itikadi
v) Misimu na mighani
Mwisho
More Question Papers