Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Narok District Mock- Kiswahili Paper 2 Question Paper

Narok District Mock- Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007



Jina………………………………………………… Namba yako …………………….
Shule………………………………………………...
102 / 2
KISWAHILI
(Ufahamu , Ufupisho, Matumizi ya lugha na IsimuJamii.)
LUGHA
KARATASI 2
JULAI / AGOSTI 2007
SAA 2 ½
MTIHANI WA MWIGO WILAYA YA NAROK-2007
Cheti cha Elimu ya Sekondari Kenya.
102 / 2
KISWAHILI
(Ufahamu , Ufupisho, Matumizi ya lugha na IsimuJamii.)
LUGHA
KARATASI 2
JULAI / AGOSTI 2007
SAA 2 ½
MAAGIZO:
• Andika jina lako na namba katika nafasi zilizoachwa hapo juu.
• Jibu maswali yote.
• Majibu yako yaandikwe katika, nafasi zilizoachwa katika kitabu hiki cha maswali.
Karatasi hii ina kurasa2 zilizopigwa chapa
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo
1. UFAHAMU
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali:
Baada ya kutambiwa hadithi na nyanyake, kombe alikwenda shingo upande na kujisukumia kitandani.
Huku akili ikimzunguka na moyo wake ukimpapa kwa nguvu kifuani kama kwamba ukitaka
kutorokea mbali, kombe alijaribu kufunga macho. Alijaribu kujisahaulisha aliyokuwa ameyasikia kutoka kwa nyanyake. Lakini wapi! Kila alipozidi kufanya hivyo ndivyo hali hiyo nayo alivyoihisi kumvamia zaidi akamlaani kimoyomoyo nyanyake ambaye bila shaka wakati huu alikuwa katika usingizi wa pono. Ilikuwa baada ya muda ambapo kwa namna ambavyo hakuifahamu, macho yake yalilegea na kumwia mazito katika hali hii aliona dude; jinyama si jinyama jitu si jitu halikuwa na kichwa wala miguu na lilikuwa likimjia. Jitihada zake za kuliepuka hazikuonekana kufua dafu;akatamani ardhi ipasuke angalau immeze!
Mungu husaidia wale wanaojaribu kujisaidia, kwa hivyo hakukata tamaa. Kufumba na kufumbua
miguu yake ilipata nguvu na kuimarika chini yake kwa hivyo bila ajizi huyoo akapasua mbuga
tambarare. Alienda shoti kiasi cha kuweza kuvunja rekodi mashindanoni lakini ah! Nini tena? Kumbe zilikuwa za sakafuni tu.
Mbuga zilifinyika na kupisha hali tofauti kabisa mbele yake. Huku ng’o huku ng’o wala atokako hakuridhiki. Isitoshe kutazama nyuma akaona dude hilo si mbali sana liko naye tu, likiviringia kama gurudumu mtelemkoni. “ uchokozi gani huu sasa?” Akajiuliza kimoyomoyo. “ je nilithibitishie kuwa mimi si mwoga? Lakini roho haikumjasirisha kufanya hivyo. Hangeweza kulikadiria uwezo wala nguvu zake.
Hakukuwa na wakati wa kukaribisha mawazo zaidi. Akasikia sauti ndani kwa ndani ikimhimiza,
“Endelea, kimbia. U mweza wa kuogelea” Na hapo, huyoo akajichoma majini na kuanza kuyachapa
kwa moyo wa ushindani.
Katika kuogelea, mara kifudifudi mara kingalingali, aliweza kuona kitu kama jipira likielea likimjia tu,“ Haidhuru,” akajiambia liko mbali.” Huku akijitahidi kuongeza umbali kati yake na dubwani hilo,alisikia kitu kama sauti kali ikimsumbwi lililomfanya asahau kabisa nadharia yake ya kukata shauri upesi upesi. Kabla hajaimarika alipigwa mwereka na kuviringishwa kama pia. Akashikwa na kisuunzi,dunia nzima ikayumbayumba na kuzunguka kama tiara.
Mara alipigwa na mkondo kasi wa maji akapelekwa vuu na kugongwa kwa nguvu maweni ambapo
alivunjwavunjwa na kuchubuliwa ngozi. Akachomwa na maumivu makali yalimfanya apige ukelele
uliopasua mbingu. Alichuruzika majimaji yenye mwonjo wa chumvi ulimini. Majimaji haya
yalimtapakaa mwili mzima, Ahaa matokeo ya majeraha mabaya sana! Hapo pole pole alianza
kurudiwa na fahamu zake. Kuzinduka akajikuta mafinyoni mwa kitanda chake cha mwakisu, jasho
jembamba likimtoka mwili mzima. Akajinasua mafinyoni akajikagua, akasonya na kuketi. Kila kitu kilikuwa kimya isipokuwa mikoromo ya ndugu zake wakiokuwa wakifurahia usingizi bila shaka.
Akavuta shuka yake iliyokuwa imesegeka upande, akjifunika barabara, ili kufurahia usingizi wa wakati uliokuwa umesalia.
MASWALI.
1. a) Ipe kichwa mwafaka habari hii. (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
b) Kulingana na habari hii unafikiri kombe alitambiwa hadithi ya aina gani na nyanyake.
(Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
c) Kwa nini kombe alimlaani nyanyake kimoyomoyo? (Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
d) Kwa nini kombe aliwaza kuwa “Mungu huwasaidia wale wanaojaribu kujisaidia?
(Alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
e) Eleza maana ya maneno yalioandikwa kwa herufi za mlazo kama yalivyotumiwa katika
taarifa hii.
(i) Kutambiwa
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(ii) Ajizi
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(iii) Kingalingali
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(iv) Kisuunzi
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(v) Kitanda chake cha mwakisu.
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(alama 5)
f) Eleza maana ya semi zifuatazo kama zilivyotumiwa (Alama2)
(i) Usingizi wa pono
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
(ii) Alienda shoti
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
2. MUHTASARI
Kwa jumla, ujanja tofauti tofauti ulizua wachuna wa koo, mbari na wa milango tofauti. Kulizuka wale waliotegemea siri ya kugeuza mchanga na ukawa chuma, yaani wafua vyuma. Wacheza ramli pia walizua wachuna. Masonara pia na watu wengine wengi, walitumia tambo za kila aina.
Akiendelea kuandika, Dzombo akasema: upekuzi umenielimisha kwamba, baada ya kuchipuka kwa
koo za kichuna, kitu muhimu cha kwanza walichokisisitiza ili waweze kudumisha uchuna wao,
kilikuwa ni kutumia ule ulaghai uliosema kuwa ati hawakuwa watu kawaida. Wengi walisema asili zao si za kibinadamu. Wengine wakajitia kusema ati hata damu zao hazikuwa nyekundu bali buluu!
Waliapa kuwa kuzaliwa kwao hakukuwa kwa kawaida, kwa hivyo, hawakuwa na mama wala baba
sembuse babu na nyanya?
Walijitia umashuhuri kwa kusema hakujulikani walikotokezea, ingawaje hawakuwa na budi ila kuwata wale waja wao. Waliotawaliwa wakatazamiwa washukuru sana bahati yao njema! Walijipa sifa za kimiungu na kuanzisha tafrija, nderemo, tamaduni, mila na desturi zilizokuwa na lengo moja tu.
Kuwatenganisha na binadamu wengine kwa makusudi ya kudumisha janja hizo zao. Walijitia kutawa na ngozi zao zikachujuka sana. Lakini sio ngozi tu ndiyo iliyobadilika pekee, pia nywele na kucha.
Haya yalikua na yakawa marefu. Hivi basi ndivyo walivyokoma kuwa binadamu na kuwa mazimwi.
Hofu na woga uliwashika wenzao kila walipojidhihirisha. Nao kwa kutumia woga na hofu hii,
wakaweza kuzika makucha yao zaidi kwa wenzao ili kuzidisha urundikaji wa ziada.
Wengine wao kama wale wafua vyuma, waliwatingisha waja wao kwa kuwalaghai ati chuma
hakingeweza kupatikana kisipofuliwa kwa mafuta ya binadamu. Ubaradhuli huu ukazua tabia ya kutoa kafara ya machipukizi wawili bikira – mvulana na msichana, kila mwaka kwa Mungu wa chuma. Na kwa kuwatia fedheha za namna hii wenzao, koo za wachuma zikaweza kuwatatanisha na kwa hivyo,kuwatawala, navyo jinsi idadi yao ilivyoongezeka, ndivyo walivyozidi kukama ziada kutoka kwa waja wao. Ili kujikinga na uporaji huu wa kichuna, hawa waja sasa nao wakaanza kuficha mazao yao.
Lakini sasa wachuna nao wakawa wameota meno. Kujenga magereza kukawa itikadi ya ustaarabu
wao!
Fedheha zao ambazo sasa zilijulikana kama sheria au dini, wakaziambatanisha na fedheha za
kimabavu. Lakini desturi ikawa mabavu kwanza kisha dini. Kwani wachuna, kwa kutumia hiyo
miundo ya ziada, waliweza na kuwafunga mabarubaru ambao hawakuwa na kazi nyingine isipokuwa
ile iliyohakikisha kuwa amri na sheria za wachuna zinaogopwa na kufuatwa. Kwa kuwashibisha
wachache wachuna wakawa wameshagundua vipi njaa na shibe ni fimbo na silaha kwao.
Miaka nenda miaka rudi, koo za wachuna zikawa zimejipanua vilivyo. Jamii bila wachuna ilionekana kama haiko kamilifu kwa hivyo, walizidi kujitenga kimaisha, kwao maskani waliokokuwa wakiishi,kukaitwa, “ mijini”na kwa wale wengine “ mashambani” jamii ikawa sasa imejigawa vipande viwili mji na shamba. Tabaka mbili: Mla na mliwa. Daraja mbili: akili na tani.
MASWALI.
a) Andika kwa ufupi yanayozungumziwa na mwandishi katika aya ya pili na ya tatu (Maneno kati ya
ya 50-60) (Alama6)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
b) Bila kubadilisha maana iliyokusudiwa na mwandishi, fupisha aya ya mbili za mwisho
(Maneno kati ya 60-70) (Alama7)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
MATUMIZI YA LUGHA:
a) Andika anavyoitwa (aitwaye) mtendaji wa vitendo hivi; (Alama3)
(i) Cheka
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(ii) Gomba
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(iii) Kaa
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
b) Andika tofauti za kimaana zinazojitokeza katika sentensi zifuatazo: (Alama2)
(i) Waliowasili ni wana wake tu.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
(ii) Waliowasili ni wanawake tu.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
c) Taja matumizi mawili mawili kwa kila mojawapo ya alama zifuatazo za uakifishaji . (Alama4)
i) Koloni (nukta mbili)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) Mstari wa mshazari
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
d) Jaza mapengo katika jedwali lifuatalo kama ulivyoelekezwa (Alama4)
KITENZI MZIZI WA 1 KAULI YA KAULI YA KAULI YA
( T) ( T ) KUTENDEA KUTENDEWA KUTENDANA
PIKA PIK PIKIA PIKIWA PIKIANA
Amekuwa
Niliteuliwa
e) Kanusha sentensi ifuatayo (Alama2)
Nikimshika mwizi nitampeleka kituo cha polisi
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
f) Geuza sentensi hizi ziwe katika usemi halisi. (Alama4)
i) Mwenye hoteli alitaka kujua jumla ya vikombe vya chai tulivyohitaji
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) Mama alipoingia alituambia tuache kupiga kelele mara moja
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
g) Pigia mstari shamirisho zilizo kwenye sentensi zifuatazo na useme ni za aina gani (Alama4)
i) Jirani atamchinjia mama kuku
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) Asha anawafumia mikeka wazee
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
h) Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi tofauti ya neno ila (Alama2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
i) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia njia ya jedwali (Alama4)
I. Mwaridi umechipua mapema sana
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
j) Tenganisha mofimu katika maneno yafuatayo (Alama2)
(i) Mgeni
(ii) Uchumi
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
k) Vitenzi vilivyopigiwa mistari ni vya aina gani? (Alama2)
i) Wanafunzi walikuwa hawajawahi kukariri mashairi.
ii) Wanasiasa ni watu wa kustaajabisha
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
L) Eleza maana ya semi zifuatazo (Alama2)
a) Kumbatia chui
b) Kunjua jamvi
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
m) Andika sentensi ifuatayo kwa ukubwa (Alama2)
Mbuzi alipigwa kwa kijiti akafa
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
n) Eleza maana NNE za kitawe kifuatacho: (Alama2)
Kaa
(i)…………………………………………………………………………………………………
(ii)……………………………………………………………………………………..…………
10
(iii)………………………………………………………………………………………….……
(iv) ………………………………………………………………………………………….……
o) Eleza maana ya methali (Alama1)
Kupanda mchongoma kushuka ndio ngoma
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
4. ISIMU JAMII
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata
Muuzaji: Kila sketi ni shilingi mia nunua
Mnunuzi: (Akipekuapekua) Aah hii ni juu sana, nikatie.
Muuzaji: Auntie, ni bei ya jioni, bei imeteremka sana.
Mnunuzi: Niuzie semanini
Muuzaji: Hiyo ndiyo bei niliyonunua, ongeza kumi. Aah hutaki kunikuta hapa kesho?
Mnunuzi: Sina zingine
Muuzaji: Ongeza tano. Haya ng’ara.
MASWALI:
a) Tambua sajili iliyotumika hapa. (Alama1)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
b) Endeleza neno ‘semanini’ kwa njia sahihi (Alama1)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
c) Taja sifa zozote saba za sajili /rejista iliyo hapo juu. (Alama7)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………
d) Rejista ni nini? (Alama1)
……………………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………………






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers