Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Nyamira District Mock - Kiswahili Paper 3 Question Paper
Nyamira District Mock - Kiswahili Paper 3
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2007
102 / 3
KISWAHILI
KARATASI 3
(FASIHI)
JULAI-AGOSTI 2007.
MUDA: SAA 2 ½
MTIHANI WA MWIGO-WILAYA YA NYAMIRA - 2007
Hati ya kuhitimu elimu ya sekondari.
102 / 3
KISWAHILI
KARATASI 3
(FASIHI)
JULAI-AGOSTI 2007.
MUDA: SAA 2 ½
MAAGIZO KWA MTAHINIWA.
• Jibu maswali manne.
• Swali la kwanza ni lazima.
• Maswali mengine matatu yachaguliwe kutaka
• Sehemu nne zilizobaki: tamthilia, Riwaya,. Hadithi fupi na ushairi. Usijibu maswali mawili kutoka kitabu kimoja.
Karatasi hii ina kurasa 8 zilizopigwa chapa
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo.
FASIHI SIMULIZI.
1. Soma wimbo ufuatao kasha ujibu maswali.
Lala mlezi wa mwana x2
Mama yako huyoo
Amekwenda mtoni.
Lala, lala, mlezi wa mwana x2
Akipata nyama mama we!
“mlezi una uhuru kwenda nyumbani”
Siku ya mboga shangazi
“mlezi njoo tule”
Kiazi cha mtoto, kiazi
Kimekwisha kabisa.
Uji wa mtoto, uji
Umekwisha kabisa.
Umekisha kabisa.
Umekisha kabisa.
(a) Hii ni aina gani ya wimbo? Eleza. (alama1)
(b) Unafikiri ni matukio gain yaliyopelekea msanii kuutunga wimbo
huu? (alama 3)
(c) Fafanua sifa anazopaswa kuwa nazo mtambaji bora wa fasihi
simulizi. (alama 4)
(d) Dokeza mbinu moja ya kifasihi inayotokea wimboni ukitoa sababu
ya matumizi yake. (alama 2)
(e) Eleza kwa kifupi nafasi ya nyimbo katika jamii ya kisasa (alama 6)
(f) Taja matatizo yanayoweza kumkumba mtafiti wa kazi ya fasihi simulizi kama hii.
(alama 4)
TAMTHILIA
Kifo kisimani.
2. Huku ukitolea mifano maradhawa, jadili dhana kuwa tamthilia ‘kifo kisimani’
inamulika na kupiga vita utawala dhalimu katika mataifa ya kiafrika.
(alama 20)
RIWAYA
Z. Burhani: Mwisho wa kosa
3. “…. Juu ya masomo yako na makaratasi yako na kizungu chako, wewe ndiye
mjinga mbele ya watu wote………..”
(a) Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
(b) Dhana ya elimu na usomi imechorwa riwayani kama kitovu cha uovu
katika jamii. Thibitisha kauli hii huku ukiwarejelea wahusika wowote watano.
(alama 10)
(c) Ustaarabu na maendeleo ni pande mbili za sarafu moja. Fafanua
kulingana na riwaya ‘mwisho wa kosa’ (alama 6)
HADITHI FUPI
K.W Wamitila: Mayai Waziri wa Maradhi
Jibu swali la 4 au la 5
Uteuzi wa Moyoni
4 Mwandishi wa ‘uteuzi wa Moyoni’ amewasawiri wahusika wa kike kama ambao
hawajazinduka kijamii, kisiasa na kielimu. Jadili. (alama 20)
5 “Ah…..Na hata tabia na mienedo yenyewe nitaionea wapi na lini mwalimu? Si
ninyi ndinyi mnaoshinda naye shuleni?”
(a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake. (alama 2)
(b) Taja sifa nne za mhusika Makulu katika hadithi. (alama 4)
(c) Fafanua matumizi ya mbinu methali katika hadithi hii. (alama 4)
(d) Eleza athari za madawa ya kulevya, katika jamii kwa mujibu wa ‘Fumbo
la Mwana.’ (alama 10)
6 FASIHI-USHAIRI
Soma shairi hili kasha ujibu maswali.
1. Pasi kuhofu lawama, imenibidi kunena,
Nina mengi ya kusema, ambayo ni ya maana
Kwetu sote ni lazima, viumbe kuambizana,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema.
2. Sahau I akilini, yataka kukumbushana,
Madamu tu duniani, la kosa huelezana,
Ili tuwe hadharini, tujilinde na fitina,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema
3. Uchochezi ukitiwa, uwongo unapofana,
Lolote laweza kuwa, hata watu kupigana,
Fitina yaweza ua, binadamu wengi sana,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema.
4. Fatani anapojua, jamii yasikizana,
Aweza leta adawa, ya fitina kugombana,
Hata akawa baguwa, ndugu wakafarikana,
Yashinda kifo fitina, fatani si ntu mwema.
5. Nahakikisha wenzangu, fitina ina laana,
Fitina kwa Bwana Mungu, katu hataki iona,
Yasaliti walimwengu, mume mke kuachana,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema.
6. Fitina si kitu safi, nazidi toa bayana,
Fitina ina makofi, muda ukijulikana,
Fitina ni ukorofi, mfano wake hapana,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema.
7. Fitina yashinda tusi, uovu wa kutukana,
Fitina ina maasi, madhambi ya kujazana,
Fitina ina utesi, tena usowezekana,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema
8. Fitina si masihara, yashinda hata khiana,
Fitina ina madhara, nchi zaweza gongana,
Fitina aina izara, na aibu nyingi sana,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema.
9. Fitina haina shaka, ni mbovu nasema tena,
Fitina mali hakika, ya ghibu nawe waona,
Fitina ina mashaka, na dhiki kila namna,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu mwema.
10. fitina kitu haramu, tamati zaidi sina,
Fitina na binadamu, wawe wakichukiana,
Fitina ni mbaya sumu, ya au sifa na jina,
Yashinda kifo fitina, fatani si mtu, mwema.
Maswali:
(a) Bainisha athari tano za fitina kulingana na mshairi (alama 5)
(b) Ubeti wa sita umechukua mikondo na bahari tofauti tofauti. Zitaje na utoe mifano
(alama 4)
(c) Andika ubeti wa nne kwa lugha ya nathari (kawaida) (alama 3)
(d) Mshairi ametumia mbinu zipi kufanya jumbe zake zieleweke kwa bayana zaidi.
(alama 4)
(e) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi.
(i) Adawa
(ii) Fatana
(iii) Wakafarikana
(iv) Tusi (alama 4)
7. Soma shairi hili kisha ujibi maswali yanayofuata.
1. Tusitake kusimama, bila kwanza kusimama,
Au dede kuwa hima, kabla hatujakaa,
Tutakapo kuchutama, kuinama inafaa,
Tujihimu kujinyima, makubwa kutoyavaa.
2. Tusitake kuenenda, guu lisipokomaa,
Tujizonge na mikanda, inapochagiza njaa,
Na mazuri tukipenda, ni lazima kuyandaa,
Tujiase kujipinda, kujepusha na balaa.
3. Tusitake uvulana, au sifa kuzagaa,
Tushikaye nyonga sana, tunuiyapo kupaa,
Kama uweza hapana, tutoelee dagaa,
Tujiase hicho kina, maji yajapokujaa.
4. Tusitake vya wenzetu, walochuma kwa hadaa,
Wanaofyatua vitu, na kasha vikasambaa,
Uwezo hatuna katu, umaskini fazaa,
Tujihimu kula vyetu, siendekeze tamaa.
5. Mtaka kuiga watu, kufata kubwa rubaa,
Vyao vijaile kwetu, vifaa vingi vifaa,
Tunamezwa na machatu, tusibakishwe dhiraa,
Tujihimu kilo chetu, hata kama twapagaa.
(a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (alama 1)
(b) Eleza madhumuni ya shairi hili (alama 2)
(c) shairi hili ni bahari gani? Toa sababu. (alama 4)
(d) Bainisha umbo katika ubeti wa kwanza na wa mwisho ukizingatia vina na mizani.
(alama 4)
(e) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha nathari. (alama 4)
(f) Taja mbinu moja ya kisanii inayoibuka katika ubeti wa nne. Kwa nini
imetumiwa? (alama 2)
(g) Eleza msamiati ufuatao kama unavyotokea katika shairi. (alama 3)
(i) Kuiga
(ii) Dede
(iii) Tujizonge.
More Question Papers