Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Teso District Mock - Kiswahili Paper 2 Question Paper

Teso District Mock - Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2007



Jina………………………………………………… Nambari. …………………….
Shule ………………………………………………...
102/2
KISWAHILI
KARATASI 2
(LUGHA)
JULAI/AGOSTI 2007
SAA: 2 ½
WILAYA YA TESO BARAZA LA MITIHANI - 2007
Hati ya kuhitimu kisomo cha sekondari (K.C.S.E)
102/2
KISWAHILI
KARATASI 2
(LUGHA)
JULAI/AGOSTI 2007
SAA: 2 ½
• Jibu maswali yote
• Majibu yako yaandikwe katika nafasi zilizoachwa katika kijitabu hiki.
Ni vigumu kusema bayana ni mfumo upi ambao ni aali kuliko mwingine. Mfumo wa ubepari na ule
wa soko huria unampa mtu mwenye juhudi nafasi ya kujiendeleza kabisa bila ya kuwepo kwa vizuizi.
Lakini kujiendeleza huku huenda pia kukahusisha hadaa na ghilba katika biashara anayoifanya.
Ukomunisti kwa upande wake unaudhibiti uhuru wa kibinafsi wa mtu sana. Kila binadamu huhitaji uhuru ili aweze kujiendeleza. Miaka iliyotangulia kusambaratika kwa mfano wa ukomunisti ilitawaliwa na tuhuma na vita vya baridi baina ya Marekani (iliyowasilisha upande mmoja) na
Urusi[upande wa pili]. Labda hali hii imebadilika. Lakini kukua mno kwa ubepari na mfumo wa soko
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo.
Swali la kwanza
UFAHAMU
Soma taarifa hii kisha ujibu maswali
Siasa ya ulimwengu ilibadilika pakubwa katika miaka ya mwanzoni mwa 1990. Mfumo wa
ukomunisti ulioshamiri katika mataifa ya Ulaya Mashariki ulisambaratika. Huu ni mfumo ambao
ulikuwako kwa miaka mingi. Mfumo huu ulijengwa kwenye imani ya kuwa, mataifa yana jukumu
kubwa la kuhakikisha kuwa pana usawa katika ugavi wa rasilmali za taifa linalohusika. Huduma nyingi za kijamii zilifuata mkondo wa maamuzi ya viongozi wa nchi na chama ambacho kilikuwa na satua kubwa juu ya raia.
Mataifa mengi yaliyofuata mkondo huu wa siasa yaliamini kuwa yalitilia maanani utu na raia wake.
Siasa ya ukomunisti iliamini kuwa siasa iliyoshika mizizi katika nchi za Ulaya ya Magharibi na Marekani, ya ubepari, ilikuwa mbaya. Waliamini kuwa ubepari unawavua watu utu wao ama kuwafanya watende matendo ambayo hayana chembe ya ubinadamu. Walishikilia kuwa ubepari ni mfumo uliotovukwa na utu. Si ajabu kuwa mtu mmoja anaweza kuwa tajiri kupindukia katika mazingira ya kuzungukwa na mamilioni ya mafukara. Ukomunistgi uliamini kuwa ubepari ni mfumo hasi ambao hatimaye unaweza kuiangamiza nchi. Nchi zilizofuata siasa ya ubepari na mfumo wa soko huria, zilikuwa na sababu zao.
Wao waliamini kuwa ukomunisti ulikuwa mfumo unaowatia raia kwenye kongwa kama watumwa.
Walishikilia kuwa ukomunisti ulikuwa na imani potovu kuhusu umuhimu wa dini katika maisha ya binadamu. Kila binadamu anahitaji uhuru wa kuamua ataufuata mkondo upi wa mawazo na ataifuata dini ipi. Uhuru wa aina hii haupatikani katika nchi zilizoufuata ukomunisti. Aidha walishikilia kuwa dola haipaswi kufanya maamuzi yote kuyahusu maisha ya raia zake. Kila kiumbe ana uhuru wa kuamua mambo yake ya kibinafsi. Kwa kiasi fulani, waliopendelea siasa ya ubepari na soko huria waliakisi maneno yaliyotamkwa na mtaalamu mmoja zamani kuwa, ‘binadamu huzaliwa huru lakini kila mahali anaishi katika minyororo’.
huria kuna hatari pia za kuyaangamiza mataifa yasiyokuwa na uwezo wa kushindana na hayo yenye uwezo mkubwa.
MASWALI
a) Taja sifa mbili hasi za mfumo wa ubepari na soko huria. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
b) Eleza msingi mkuu wa siasa ya ukomunisti. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
c) Bainisha hatari zinazoweza kuibuka kwa mataifa machanga iwapo yatafuata mfumo wa
ubepari na soko huria. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
d) Fafanua kifungu hiki, “binadamu huzaliwa huru lakini kila mahali anaishi katika minyororo”
(alama1)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
e) Wakereketwa wa ubepari walikuwa na maoni yapi kuhusu ukomunisti? (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
f) Kwa kuzingatia muktadha huu, ni mfumo upi ungefaa kwa jamii yako? Toa sababu. (alama 1)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
g) Eleza mbinu za uandishi zilizotumika katika makala hii. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
h) Fafanua msamiati huu kama ulivyotumika katika kifungu. (alama 3)
i) ulioshamiri
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) aali
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
iii) tuhuma
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
Swali la pili
UFUPISHO
Soma taarifa hii kisha ujibu maswali
Katiba hutumiwa kuelezea mfumo mzima wa serikali ya nchi na hasa kanuni ambazo huunda na
kudhibiti utendakazi wa serikali hiyo. Kwa msingi huu basi, katiba inakuwa kama roho ya nchi hiyo; ikiwa itakuwa mbaya basi nao utendakazi wenyewe utakuwa mbaya. Kanuni huweza kuwa za sheria ambazo hutambuliwa na mahakama ambazo zina jukumu la kuhakikisha kuwa zimetekelezwa na kufuatwa bila ya ubaguzi wala mapendeleo. Zipo kanuni nyingine ambazo hutokana na maelewano, desturi, itikadi na kaida ambazo hudhibiti jamii inayohusika na huwa sehemu ya haki za jamii yenyewe.
Nchi ambayo inatawaliwa kwa msingi wa katiba hujulikana kama serikali ya kikatiba. Serikali
ambayo inatawaliwa kwa kutegemea katiba huheshimu sheria na kanuni zilizopo. Serikali hiyo
hutumia katiba iliyopo kama msingi wa utendakazi wake na huhakikisha kuwa raia wa nchi hiyo
anaitii na kuiheshimu katiba iliyopo. Kinyume cha serikali ya kikatiba ni serikali ya ki-imla. Serikali ya aina hii haiongozwi na sheria zozote bali huongozwa na matakwa na hawaa ya nafsi ya kiongozi mmoja au kigaro kidogo cha watu wanaomzunguka kiongozi wa aina hiyo. Katika nchi ya aina hiyo sheria zilizopo hutumiwa kama nyenzo ya kuhalalisha udhalimu na kulilinda tabaka la viongozi na vibaraka wao.
Matendo ya serikali ya kikatiba kwa upande mwingine huongozwa na kudhibitiwa na vizuizi fulani.
Vizuizi hivi hutokana na kuwako kwa sheria zinazolinda haki ya kila mmoja. Haki hizo hulinda raia wa nchi bila ya kujali rangi, jinsia, maumbile, dini, vionjo wala makazi yake. Jamii ya aina hiyo haiongozwi tena na msemo wa ‘mwenye nguvu mpishe’ au ‘mnyonge kupata ni mwenye nguvu kupenda’. Badala yake huongozwa na msemo wa ‘sheria ni msumeno hukata mbele na nyuma’.
Ikiwa mwenye madaraka atakiuka sheria zilizopo, ataadhibiwa bila ya mapendeleo. Mnyonge naye akikiuka sheria, ataadhibiwa vivyo hivyo.
Hapo kabla tulinganisha katiba ya nchi na roho ya nchi hiyo. Nchi ambayo haina roho ni nchi
iliyokufa na isiyotegemewa kuwa na uhai wowote. Hii ina maana kuwa ili kuwa na katiba nzuri na ya kutegemewa kuna mambo kadha ya kuzingatia. Msingi wa katiba nzuri ni ufahamu wa raia wa nchi kuwa nchi yao ina hadhi kubwa kuliko wao wenyewe. Katiba nzuri ni ile ambayo itakuwa na uwezo kuilinda jamii hiyo kwa kipindi kirefu. Haihalisi kuwa na katiba ambayo itatumiwa kwa miaka michache kisha baadaye isiweze kufaa tena. Vivyo hivyo, ni haramu mutlaki kwa katiba kuwepo kwa muda ili kuyakidhi mahitaji ya kundi fulani la watu ambalo litakuwepo kwa muda tu. Ni misingi ipi basi muhimu katika kuunda katiba ya aushi?
Msingi wa kwanza na wa lazima ni uzalendo. Uzalendo unakuwa nguzo kuu kwa kuwa
tunapozungumzia katiba ya nchi fulani humaanisha inahusu jamii fulani inayojitambua kama ya taifa fulani. Uzalendo ni hisia ya kuipenda nchi yako kwa dhati na kuwa tayari hata kuifia. Ikiwa hisia za uzalendo ni za dhati, basi itakuwa rahisi kwa jamii inayohusika kuiwazia katiba ambayo itaendelea kuwako kwa miaka mingi ijayo. Jamii inayoongozwa na hisia za uzalendo na utaifa haitakubali kupofushwa na tama za muda mfupi tu. Msingi mwingine muhimu ni utambuzi wa kuwa jamii inajumlisha watu wa kila aina na wenye tofauti anuwai. Tofauti hizi zinaweza kuwa za kirangi,kilugha, kiitikadi, kielimu, kijinsia, kimaumbile n.k. Katiba nzuri lazima itilie maanani uhalisi huo na iuakisi.
Katiba haina budi kutambua kuwa kila jamii ina historia yake na hasa utamaduni na upekee wake.
Kuna baadhi ya matendo ambayo ingawa yamezoeleka kwingine ni mageni na yanatisha katika
utamaduni mwingine kwa mfano uhusiano wa kimapenzi kati ya mwanaume na mwanamume (yaani
ubasha) mwenzake na kati ya mwanamke na mwanamke mwenzake (usagaji). Hamna nchi ambayo
inashabihiana na nyingine katika ngazi zote. Uhalisi huu lazima uwepo katika katiba ya nchi
inayohusika. Haimkiniki kufuasa sheria na kanuni za nchi ajinabi au mataifa mengine kwa kuwa yameendelea tu. Hii haina maana kuwa jamii haiwezi kukopa mambo fulani yanayoweza kuifaidi. La hasha, inaweza. Lakini kukopa nako kunahitaji kuchuja; yapi yanafaa na yapi yanaihasiri jamii. Ni muhimu kujua kuwa kiini cha katiba yoyote ile ni uwezo wa jamii wa kujiamulia mambo yao na kuyaendesha ipasavyo. La sivyo tutawapa wengine nafasi ya kutumia vitiba vyao kututimba sisi.
MASWALI
a) Zungumzia mambo yanayojitokeza katika aya nne za kwanza katika kifungu hiki. (tumika
maneno 70 – 80) (alama 9)
Nakala chafu
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
Nakala safi
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
b) Fupisha aya mbili za mwisho. (Tumia maneno 45 – 54) (alama 6)
Nakala chafu
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
Nakala safi
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)
3. a) Akifisha;
Una kiberiti yule mtu aliniuliza na nilipotoa kiberiti na kuwasha yule mtu alinizaba kofi Maria
alieleza (alama 4)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
b) Sahihisha sentensi hii (alama 1)
Mahali hapa mna kuvutia.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
c) Andika ukubwa wa (alama 2)
i) Mwizi alifuata njia hii.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) Ngoma ilipatikana karibu na shoka
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
d) Andika sentensi hii kulingana na maagizo
Mwanafunzi mmoja tu ndiye aliyefuzu katika mtihani huo.
(Tumia : hakuna / ila) (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
e) Yakinisha (alama 2)
i) Msipokuja leo asubuhi, yule msichana hatawaandalia vyakula vya kila aina.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) Hakula mkate wala nyama
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
f) Geuza kwa umoja; (alama 2)
i) Pulikeni wanetu, msicheze na dunia. Mnasikia?
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) Yesu aliwatuma mitume wakahubiri.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
g) Taja aina mbili kuu za sauti za Kiswahili. (alama 2)
i)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
h) Andika upya sentensi zifuatazo katika kauli ulizopewa katika mabano. (alama 2)
i) Omela alimlisha mtoto wangu nami nikamlisha wake. (kauli ya kutendesheana)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) Mtoto alikunywa maziwa (kauli ya kutendesheka)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
i) Andika sentensi zifuatazo bila kutumia amba. (alama 2)
i) Kimbunga ambacho kilitokea kilisababisha hasara kubwa.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) Chui ambaye alisakwa na msasi ameuawa.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
j) Eleza matumizi ya –ki- huku ukitoa mifano mitatu tofauti. (alama 6)
i)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
iii)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
10
k) Fafanua maana mbili za sentensi hii. (alama 2)
Oshale alitimua mbio kuona ndovu.
i)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
l) Changanua kwa matawi; (alama 4)
Mwanafunzi aliyefanya vizuri amejiunga na chuo kikuu.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
m) Onyesha kundi nomino na kundi tenzi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
Kitoto hicho chake cheusi kilipotea jana asubuhi.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
n) Tumia tanakali ya sauti mwisho wa sentensi. (alama 1)
i) Mama alisaga ngano ikawa unga.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
o) Andika kisawe cha; (alama 1)
i) Istiwai
……………………………………………………………………………………………………
ii) Hau
……………………………………………………………………………………………………
p) Eleza maana ya methali ifuatayo. (alama 2)
Usimlaumu dobi, kaniki ndiyo rangi yake.
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
q) Eleza maana ya: (alama 1)
Jifanya mawele
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
r) Bainisha maneno haya (alama 2)
Kito
Kitu
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ISIMU JAMII (alama 10)
4. a) Eleza maana ya Isimu Jamii. (alama 2)
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
b) Fafanua sifa mbili za kila mojawapo ya sajili zifuatazo (alama 8)
i) Sajili ya mapenzi
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
ii) Sajili ya majambazi
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
iii) Sajili ya wazee
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………
iv) Sajili ya hospitali
……………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………………






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers