Kcse 2010 Kiswahili Karatasi Ya 102/3 Question Paper

Kcse 2010 Kiswahili Karatasi Ya 102/3 

Course:Kiswahili

Institution: Kcse question papers

Exam Year:2010



SEHEMU A: USHAIRI (alama 20) 1 (LAZIMA)
Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata.

Dhamiri yangu
Dhamiri imenifunga shingoni.
Nami kama mbuzi nimefungwa
Kwenye mti wa utu. Kamba ni fupi
Na nimekwishachora duara.
Majani niwezayo kufikia yote nimekula.
Ninaona majani mengi mbele yangu
Lakini siwezi kuyafikia: kamba, kamba.
Oh! Nimefungwa kama mbwa.
Nami kwa mbaya bahati, katika
Uhuru kupigania, sahani ya mbingu
Nimeipiga teke na niigusapo kwa mdomo
Mbali zaidi inakwenda na siwezi tena
Kuifikia na hapa nilipofungwa
Nimekwishapachafua na kuhama siwezi.
Kamba isiyoonekana haikatiki.
Nami sasa sitaki ikatike, maana,
Mbuzi wa kamba alipofunguliwa, mashamba
Aliharibu na mbwa aliuma watu.
Ninamshukuru aliyenifunga hapa
****
Lakini lazima nitamke kwa nguvu "Hapa nilipo sina uhuru!"
(E. Kezilahabi)

(a) Taja mambo manne ambayo mshairi analalamikia. (alama 4)
(b) Kwa nini mshairi haoni haja ya yeye kuwa huru? (aiama 2)
(c) Eleza rnaana ya mshororo ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi.
"Kamba isiyoonekana haikatiki." (alama 2)
(d) Taja na utoe mifano ya aina mbili za tamathali zilizotumika katika shairi hili. (alama 4)
(e) Kwa kutoa mifano miwili, eleza jinsi matumizi ya mishata yanavyojitokeza katika shairi hili. (alama 4)

(f) Andika ubeti wa pili kwa lugha nathari. (alama 4)






SEHEMU B: RIWAYA
SA.Mohamed: Utengano
Jibu swali la 2 au la 3

2. "...wewe kwako toka lini mwanamke kuwa mtu? Wangapi umewatenda?"
(a) Eleza muktadhawa dondoo hili. (alama 4)
(b) Kwa kutoa mifano minne mwafaka, dhihirisha ukweli wa dondoo hili. (alama 16)
3. Kwa kurejelea vipengele vifuatavyo vya matumizi ya lugha katika riwaya ya Utengano, onyesha jinsi mwandishi amevitumia kufanikisha maudhui:
i) uzungumzinafsi; (alama 10)
ii) taswira (alama 10)
SEHEMU C: TAMTHILIA
Kithaka Wa Mberia: Kifo Kisimani
Jibu swali la 4 au la 5

4. "Dalili ya mvua ni mawingu."
Kwa kuzingatia utawala wa Mtemi Bokono, thibitisha usemi huu. (alama 20)
5. "Nitoeni! Nitoeni kaburini. Ondoeni udongo. Ondoeni udongo nitoke kaburini."
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Taja na ueleze tamathali za usemi mbili zilizotumiwa katika dondoo hili. (alama 4)
(c) Kwa kurejelea tamthiliya nzima, fafanua hoja sita kuonyesha jinsi dondoo hili linavyoonyesha kinyume cha mambo. (alama 12)

SEHEMU D: HADITHIFUPINA FASIHI SIMULIZI
K. W. Wamitila: Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine
Jibu swali la 6 aula.7
6 "Ana nini mtoto huyu! Ninamtesekea na ufakiri wote huu nilionao..."
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
(b) Eleza tatizo alilokuwa nalo anayerejelewa kisha ufafanue vitendo vinavyodhihirisha kwamba alikuwa na tatizo, (alama 6)
(c) Anayetoa kauli hii alikuwa na msimamo gam kuhusu tatizo la mtoto? (alama 4)
(d) Kwa kutoa mifano mitatu mwafaka, eleza hali zinazoweza kulaumiwa kwa tatizo la anayerejelewa. (alama 6)

FASIHI SIMULIZI
7 Huku ukitoa mifano mwafaka, linganisha na utofautishe kipera cha vitendawili na kile cha methali. (alama 20)








More Question Papers


Exams With Marking Schemes

Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers