Kcse 2011 102/2 Kiswahili Karatasi Ya 2 Lugha  Question Paper

Kcse 2011 102/2 Kiswahili Karatasi Ya 2 Lugha  

Course:Kiswahili

Institution: Kcse question papers

Exam Year:2011




UFAHAMU (Alama15)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.
Changamoto kubwa inayowakabili watu wengi katika mataifa yanayoendelea ni suala la chakula. Suala hili linaweza kuangaliwa katika sawia mbili tofauti. Kuna tatizo linalofungamana na uhaba wa chakula chenyewe, Uhaba huu unaweza kutokana na utegemezi mkubwa kwa zaraa kama nyenzo kuu ya uzalishaji wa chakula.
Zaraa katika mataifa mengi hususan yanayoendelea, hutegemea mvua. Kupatikana kwa mvua huathiriwa na mabadiliko ya tabianchi ulimwenguni. Matendo na amali za watu kama ukataji wa miti na uchafuzi wa mazingira huwa na athari hasi kwenye tabianchi hiyo. Mabadiliko ya tabianchi huweza kuvyaza ukame kutokana na ngambi ya mvua.
Kibinimethali hutokea wakati mafuriko yanapotokea na labda kuyasomba mazao mashambani na kusababisha baa la njaa. Hali hizi mbili husababisha matatizo makubwa ya chakula na kuathiri pakubwa suala zima la usalama wa chakula. Hi kuzuia uwezekano wa kuwepo kwa shida hii, pana haja ya kuwepo kwa mikakati na sera za kuhakikisha kuna usalama wa chakula. Kwa mfano, pana haja ya kukuza kilimo cha umwagiliaji ili kuepuka adha inayosababishwa na ukosefu wa mvua. Kwa upande mwingine, sharti zichukuliwe hatua mufidi za kuzuia na kupambana na athari za gharika.
Changamoto nyingine inahusiana na usalama wa chakula chenyewe. Chakula kilichosibikwa na vijasumu au kwa njia nyingine ile huweza kumdhuru anayehusika. Msibiko wa chakula unatokana na vyanzo tofauti. Mathalan, uandalizi wa chakula kilichochafuliwa na choo, kutozingatia mbeko za usafi, uandaaji wa chakula na kukiweka katika hali ya uvuguvugu kabla ya kukipakua - hali inayochochea ukuaji wa viini na ulaji wa chakula kisichoandaliwa vyema.
Ili kuepuka uwezekano wa kuadhirika, pana haja ya kuzingatia usafi wa chakula na uandalizi unaofaa. Fauka ya hayo, vyombo vya uandalizi viwe safi, kanuni za usafi zifuatwe, upikaji na uandaaji uwe kamilifu. Hali hii isipozingatiwa, siha za raia wenyewezitaathirika pakubwa.
Maswali
(a) Taja aina mbili za kuangalia suala la chakula katika mataifa yanayoendelea.
(alama 2)
(b) Taja hatua mbili zmazoweza kuchukuliwa kupambana na tatizo la chakula.
(alama 2)
c) Eleza jinsi nne tofauti namna chakula kinavyoweza kuwa si salama? (alama 4)

(d) Kwa nini inahalisi kukipakua chakula baada ya kukiandaa tu? (alama 1)

(e) Ni mapendekezo gani anayoyatoa mwandishi kuhakikisha kuwa chakula kinafaa?
(alama 4)
(f) Eleza maana ya maneno haya jinsi yalivyotumiwa: (alama 2)

(i) Ngambi yamvua ....................................................................................................
(ii) Adha......................................................................................................................

MUHTASARI
Uwazaji tunduizi ni tendo ambalo huhusisha matumizi ya akili. Uwazaji huu umekitwa kwenye matumizi ya michakato kama makini, upangiliaji, uteuzi na tathmini. Hata hivyo, uwazaji huu si mchakato mwepesi bali ni mchakato changamano.
Mchakato wa uwazaji tunduizi unahusisha stadi na mikabala tofauti. Mathalan, kuweza kutambua na kubainisha misimamo ya watu wengine, hoja wanazozua na uamuzi waliofikia, kutathmini au kupima ushahidi uliopo ili kubainisha mitazamo tofauti. Vilevile. uwazaji tunduizi hushirikisha kupima hoja za upinzani na ushahidi uliopo kwa njia ya haki pamoja na kutambua yaliyofichwa au ukweli uliofunikwa na taswira ya juu juu. Hali kadhalika, uwazaji tunduizi hujumuisha kutambua mbinu zinazotumiwa kufikia misimamo fulani kwa mvuto zaidi na kwa matumizi ya mbinu za kishawishi. Aidha, uwazaji huu huhitaji kutathmini masuala kwa mtindo ulio wazi, kufikia uamuzi kama hoja zinazotumiwa zina mashiko au zinakubalika kuwa nzuri. Zaidi ya hayo, uwazaji tunduizi unahusisha kuwasilisha mtazarao kwa njia yenye uwazaji mzuri na inayoshawishi.
Uwazaji tunduizi una manufaa anuwai. Mosi, unasaidia kujenga makini ya utendaji. Pili, hupevusha uwezo wa usomaji kwa kuufanya usomaji huo uwe na malengo wazi. Fauka ya hayo, unamsaidia mtumiaji kutambua hoja kuu katika matini au ujumbe fulani bila ya kuzongwazongwa na hoja duni za pembeni. Uwazaji huu unasaidia kuuchonga uwezo wa kuikabili au kuiitikia hali fulani na kukuza stadi za uchanganuzi. Mwanadamu huwa mtu tofauti na bora anapoujenga na kuuimarisha uwazaji tunduizi wake.
Maswali
(a) Bila kubadilisha maana aliyokusudia mwandishi, fupisha ay a mbili za mwanzo.
(Maneno 70 - 80) (alama 10; alama 2 za utiririko)



















(b) Andika kwa muhtasari mambo muhimu katika aya ya tatu.
(Maneno 35 - 40) (alama 5; alama I ya utiririko)












3 MATUMIZI YA LUGHA.
(a) Tumiamzizi '-enye'katika sentensi kama:
(i) Kivumishi........................................
(ii) Kiwakilishi ......................................
(alama 2)
(b) Andika sentensi ifuatayo katika ukubwa:-
Paka mweupe araenaswa mguuni .(alama 2)
(c) Taja mfano mmoja mmoja wa sauti zifuatazo:-
(i) Kiyeyusho ..............................................................................................................
(ii) Kimadende..............................................................................................................
(alama 1)

(d) Onyesha shamirisho kitondo, kipozi na ala katika sentensi ifuatayo:-
Kipkemboi alimbebea mwalimu mzigo kwa gari. (alama 3)



(e) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia jedwali.
Maria alipika taratibu huku mama akimwelekeza vizuri. (alama 4)
(f) Nomino 'furaha' iko katika ngeli gani?
......................................................................................................................... (alama 1)
(g) Andika kinyume cha sentensi:
Watoto wameombwa waanike nguo. (alama 2)
(h) Andika sentensi ifuatayo upya kwa kufuata maagizo uliyopewa. Mama alishangilia arusi ya mwana. Anza: Mwana .................................................................................................. (alama 2)

(i) Tumia kirejeshi 'O' katika sentensi ifuatayo:-
Mtu ambaye hutupa tope hujichafua mwenyewe. (alama 2)
(j) Kanusha sentensi ifuatayo:
Mgonjwa huyo alipona na kurejea nyurabani. (alama 2)
(k) Ainisha vihusishi katika sentensi:
Ame aliwasili mapema kuliko wengine halafu akaondoka. (alama 2)
(1) Tunga sentensi mbili kuonyesha maana tofauti za neno "chuma". (alama 4)
(i) .................................
(ii) .................................
(m) Unda noniino kutokana na kitenzi 'tafakari' ................................................. (alama 1)
(n) Eleza maana mbili za sentensi:
Tuliitwa na Juma ........................................................................................... (alama 2)
(o) Ainisha viambishi katika kitenzi:-
Tutaonana................................................................................................ (alama 2)


(p) Tunga sentensi moja ukitumia kiunganishi cha kinyume. (alama 2)
(q) Huku ukitoa mifano eleza miundo miwili ya silabi za Kiswahili. (alama 2)
(r) Akifisha kifungu kifuatacho:
Mzee alimwambia mwanawe njoo nikupeleke kwa babu yako angalau umjue
mtoto aliuliza nani babu? (alama 4)
ISIMUJAMII
(a) Bainisha changamoto tano zinazoikabili lugha ya Kiswahili kama somo katika
shule za upili nchini Kenya. (alama 5)

(b) Eleza namna tano za kukabiliana na changamoto ulizobainisha hapo juu.
(alama 5)










More Question Papers


Exams With Marking Schemes

Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers