Educ 331:Mbinu Za Kufundisha Kiswahili Question Paper
Educ 331:Mbinu Za Kufundisha Kiswahili
Course:Elimu
Institution: Kenya Methodist University question papers
Exam Year:2012
CHUO KIKUU CHA KIMETHODISTI, KENYA
MTIHANI WA MWISHO WA TREMESTA YA PILI, 2012
KITIVO : ELIMU NA SAYANSI YA JAMII
IDARA : ELIMU
KODI : EDUC 331
ANWANI : MBINU ZA KUFUNDISHA KISWAHILI
MUDA : SAA MBILI
MAAGIZO:
Swali la Kwanza
Baadhi ya makosa ambayo wanafunzi hufanya katika kuongea na kuandika kwa lugha ya Kiswahili hutokana na maingiliano kati ya Kiswahili na lugha za kwanza. Jadili.
(al. 12)
Eleza stadi nne za kufunzia lugha ya Kiswahili kwa kuzitolea mifano mwafaka.
(al. 8)
Swali la Pili
Eleza shida ambazo huwakumba sana wanafunzi wanaposoma Kiswahili kwa sauti.
(al. 10)
Ni hatua gani anazoweza kuchukua mwalimu kupunguza shida hizo?
(al. 10)
Swali la Tatu
Huku ukitoa mifano mwafaka eleza jinsi teknolojia ya kisasa inavyoweza kutumiwa katika ufunzaji wa lugha ya kiswahili. (al. 20)
Swali la Nne
Taja na ufafanue mambo yoyote matano yanayoweza kutatiza ufahamu sikizi.
(al. 10)
Thibitisha jinsi mafunzo ya sarufi yanavyofaa mwanafunzi.
(al. 10)
Swali la Tano
Mwalimu Rea hatayarishi azimio la kazi; Je katika ufunzaji wake atatatizika vipi?
(al. 10)
Matumizi ya vifaa yana umuhimu gani katika ufunzaji wa somo la lugha ya Kiswahili.
(al. 5)
Kabla mkufunzi kwenda kufunza lugha ya Kiswahili nyanjani katika mazoezi ya kufudisha, anafaa kujiandaa vipi?
(al. 5)
More Question Papers
Exams With Marking Schemes
Popular Exams
Mid Term Exams
End Term 1 Exams
End Term 3 Exams
Opener Exams
Full Set Exams
Return to Question Papers