Lswa 400:Nadharia Ya Uhakiki Wa Fasihi Na Sanaa Za Maonyesho Question Paper
Lswa 400:Nadharia Ya Uhakiki Wa Fasihi Na Sanaa Za Maonyesho
Course:Elimu
Institution: Kenya Methodist University question papers
Exam Year:2013
CHUO KIKUU CHA KIMETHODISTI, KENYA
MTIHANI WA MWISHO WA TREMESTA YA KWANZA, 2013
KITIVO : ELIMU NA SAYANSI YA JAMII
IDARA : ELIMU
KODI : LSWA 400
ANWANI : NADHARIA ZA UHAKIKI WA FASIHI
MUDA : SAA MBILI
Maagizo: Jibu Maswali Matatu
Swali la Kwanza
Eleza maana ya nadharia kisha ufafa111aaanue umuhimu na nadharia katika kuhakiki kazi za fasihi.
(Alama 6)
Mchango wa Aristotle na Plato kuhusiana na sheria za utunzi wa kazi za fasihi umechangia pakubwa katika uundaji wa sheria mwafaka. Jadili mawazo yao kuhusiana na swala hili.
(Alama 4)
Swali la Pili
Nadharia nzuri huwa na sifa kadha. Fafanua sifa hizo.
(Alama 10)
Uchambuzi wa kazi za fasihi hujikita katika vipengele mbalimbali. Fafanua vipengele ambavyo uhakiki wake unaweza kuzingatia nadharia mbalimbali.
(Alama 10)
Swali la Tatu
Nadharia ya umaksi ni ya kimapinduzi. Jadili kauli hii ukirejelea milimili yake muhimu na mifano katika fasihi ya Kiswahili. (Alama 20)
Swali la Nne
Onyesha jinsi ushairi wa Kiswahili unaweza kuhakikiwa kwa mjibu wa matapo yafuatayo:
Urasmi
(Alama 10)
Ulimbwende
(Alama 10)
Swali la Tano
Tapo la uhalisia limetawala pakubwa uandishi na uhakiki wa kazi za fasihi. Jadili kauli hii ukirejelea mifano ya kazi za kihalisia katika fasihi ya Kiswahili.
(Alama 20)
More Question Papers
Exams With Marking Schemes
Popular Exams
Mid Term Exams
End Term 1 Exams
End Term 3 Exams
Opener Exams
Full Set Exams
Return to Question Papers