Kisw 221:Mofolojia Ya Kiswahili Question Paper

Kisw 221:Mofolojia Ya Kiswahili 

Course:Elimu

Institution: Kenya Methodist University question papers

Exam Year:2013



CHUO KIKUU CHA KIMETHODISTI, KENYA

MTIHANI WA MWISHO WA TREMESTA YA PILI, 2013

(MASOMO YA LIKIZO)
KITIVO : ELIMU NA SAYANSI YA JAMII
IDARA : ELIMU
KODI : KISW 221
ANWANI : MOFOLOJIA YA KISWAHILI
MUDA : SAA MBILI




Maagizo:

Jibu maswali matatu.

Swali la Kwanza
Huku ukitoa mifano mwafaka, fafanua dhana zifuatazo za kimofolojia. (al. 20)

Mofimu

(Al. 4)

Alomofu

(Al.4)

Mofu

(al. 4)

Mzizi wa neno

(al. 4)

Kiambishi

(al. 4)

Swali la Pili

Fafanua kwa tafsili sifa bainifu za mofu.

(al. 8)

Kwa kuzingatia kigezo cha maana na kile cha mofolojia ya mofu, eleza aina mbalimbali za mofu za Kiswahili.

(al. 12)

Swali la Tatu

Fafanua kwa kina namna ngeli za Kiswahili zinavyoainishwa kimofolojia.

(al. 12)

Jadili matatizo yaliyopo katika uainishaji wa ngeli za Kiswahili kimofolojia.

(al. 8)

Swali la Nne
Kwa kutoa mifano mwafaka bainisha namna ambavyo mofu zifuatazo zinavyodhihirika katika vitenzi vya Kiswahili. (al. 20)

Mofu za ukanushi

(al. 2)

Mofu za njeo

(al. 2)

Mofu za vipatanishi

(al. 2)

Mofu rejeshi

(al. 2)

Mofu za masharti

(al. 2)

Mofu za kauli

(al. 2)

Mofu za yambwa

(al. 2)

Mofu {ji} ya kujitendea

(al. 2)

Mofu za hali

(al. 2)

Mofu {ka} ya mfululizo.

(al. 2)

Swali la Tano
Jadili kwa kina dhana ya viwakilishi ukirejelea mifano. (al. 20)






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers