Lswa 105:Historia Ya Kiswahili Question Paper
Lswa 105:Historia Ya Kiswahili
Course:Elimu
Institution: Kenya Methodist University question papers
Exam Year:2012
CHUO KIKUU CHA KIMETHODISTI, KENYA
MTIHANI WA MWISHO WA TREMESTA YA TATU, 2012
(MASOMO YA LIKIZO)
¬
KITIVO : ELIMU NA SAYANSI YA JAMII
IDARA : ELIMU
KODI : LSWA 105
ANWANI : HISTORIA YA KISWAHILI
MUDA : SAA MBILI
Maagizo:
Jibu maswali yoyote matatu
Swali la Kwanza
Kwa kutoa mifano, fafanua vipengele vya kihistoria na kiisimu vinavyothibitisha kwamba Kiswahili ni lugha ya kibantu. (Al. 20)
Swali la Pili
Lugha ya Kiswahili imepata umaarufu katika karne ya ishirini na moja. Jadili
(Al. 10)
Maenezi ya Kiswahili Nchini Kenya na Uganda yalikabiliwa na vikwazo kadhaa wa kadhaa jadili.
(Al. 10)
Swali la Tatu
Jadili matatizo kumi yanayokikumba Kiswahili nchini Kenya na upendekeze hatua zinazoweza kuchukuliwa kusuluhisha matatizo hayo. (Al. 20)
Swali la Nne
Eleza maana ya usanifishaji lugha kisha ufafanue hatua muhimu ambazo hufuatwa wakati lugha inaposanifishwa.
(Al. 6)
Fafanua matatizo mbalimbali yaliyokumba kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki (K.K.A.M) katika kufikia malengo yake ya usanifishaji wa Kiswahili.
(Al. 14)
Swali la Tano
Eleza mchango wa waingereza na wamishenari katika kukuza na kueneza Kiswahili Afrika Mashariki. (Al. 20)
More Question Papers