Lswa 105:Historia Ya Kiswahili Question Paper
Lswa 105:Historia Ya Kiswahili
Course:Education
Institution: Kenya Methodist University question papers
Exam Year:2013
CHUO KIKUU CHA KIMETHODISTI, KENYA
MTIHANI WA MWISHO WA TREMESTA YA KWANZA, 2013
KITIVO : ELIMU NA SAYANSI YA JAMII
IDARA : ELIMU
KODI : LSWA 105
ANWANI : HISTORIA YA KISWAHILI
MUDA : SAA MBILI
Maagizo:
Swali la Kwanza
’Kiswahili ni lugha ya kiarabu’. Jadili nadharia tete hii huku ukionyesha mihimili na udhaifu wake. (Alama 20)
Swali la Pili
Kwa kujikita katika misingi ya kiisimu thibitisha kwamba Kiswahili ni lugha ya kibantu. (Alama 20)
Swali la Tatu
Fafanua mambo yoyote manne yaliyochangia maenezi ya lugha ya Kiswahili katika Afrika Mashariki. (Alama 20)
Swali la Tatu
Eleza maana ya usanifishaji wa lugha.
(2 Marks)
Yadokeze majukumu manne yaliyopendezekezwa kushughulikiwa na Baraza la lugha la Afrika Mashariki (ITLC) mwaka wa 1930.
(Alama 4)
Fafanua hali iliyopelekea Kiswahili kuyumba nchini Uganda wakati wa Ukoloni.
(Alama 12)
Swali la Tano
Ukirejelea lahaja tatu Kinzani, eleza mvutano uliokumba uteuzi wa lahaja ya usanifishaji.
(Alama 15)
Eleza maana ya sera ya lugha na udhihirishe hatua nne zilizodokezwa na Hugen (1966) za upangaji lugha.
(alama 5)
More Question Papers