Lswa 105:Historia Ya Kiswahili Question Paper
Lswa 105:Historia Ya Kiswahili
Course:Elimu
Institution: Kenya Methodist University question papers
Exam Year:2012
CHUO KIKUU CHA KIMETHODISTI, KENYA
MTIHANI WA MWISHO WA TREMESTA YA TATU, (MCHANA) 2012
KITIVO : ELIMU NA SAYANSI YA JAMII
IDARA : ELIMU
KODI : LSWA 105
ANWANI : HISTORIA YA KISWAHILI
MUDA : SAA MBILI
Maagizo:
Jibu maswali matatu
Swali la kwanza
Fafanua nadharia tatu zinazoelezea chimbuko la Kiswahili.
(alama 15)
Eleza upungufu wa nadharia inayodai kwamba Kiswahili ni lugha ya mseto.
(alama 5)
Swali la Pili
Wafanya biashara waarabu walifanikiwa kueneza Kiswahili nchini Tanganyika kuliko nchini Kenya. Thibitisha madai haya kwa kutoa mifano mwafaka. (alama 20)
Swali la tatu
Elaza maana ya usanifishaji kisha ufafanue hatua muhimu ambazo hufuatwa wakati lugha inaposanifishwa. (alama 20)
Swali la Nne
Tathmini malengo ya kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki. (alama 10)
"Kiswahili kinahitaji kusanifishwa upya" Jadili kauli hii.
(alama 10)
Swali la Tano
Elaza jinsi sera ya lugha nchini Tanzania ilivyosaidia lugha ya Kiswahili kuenea. (alama 20)
More Question Papers