Lswa 105:Historia Ya Kiswahili Question Paper
Lswa 105:Historia Ya Kiswahili
Course:Elimu
Institution: Kenya Methodist University question papers
Exam Year:2011
FACULTY : EDUCATION & SOCIAL SCIENCES
DEPARTMENT : EDUCATION AND PRE-UNIVERSITY
TIME : 2 HOURS
MAAGIZO Jibu Swali la KWANZA kutoka Sehemu A na mengine MAWILI kutoka Sehemu B
Sehemu A
Swali 1
a) Jadili huku ukitoa mifano mwafaka nadharia tatu ambazo zinaeleza chimbuko la Kiswahili. (alama9)
b) Eleza dhana zifuatazo
i) pijini
ii) krioli
iii) lugha ya taifa
iv) lugha rasmi (alama8)
c) Fafanua fasiri tatu kuhusu dhana ya mswahili ni nani kama inavyoelezwa na wataalamu wa historia ya lugha. (alama3)
Sehemu B
Swali 2
a) Lugha ya Kiswahili haikuenea kwa mapana nchini Uganda kama nchini Tanzania na Kenya. Fafanua dai hili. (alama15)
b) Eleza sababu TANO zilizokwaza kuenea kwa Kiswahili nchini Kenya kabla ya uhuru.(alama5)
Swali 3
a) Eleza majukumu sita ya kamati ya usanifishaji wa lugha ya Kiswahili. (alama12)
b) Fafanua sababu zilizopelekea Kiunguja kuchaguliwa kama lahaja ya usanifishaji. (alama8)
Swali 4
Teknolojia ya kisasa ya mawasiliano inatumia Kiswahili. Thibitisha dai hili kwa kutoa mifano toshelevu. (alama20)
Swali 5
Jadili hali iliyopelekea Kiswahili kuenea zaidi nchini Tanzania kuliko nchi nyingine za Afrika mashariki. (alama20)
More Question Papers