Lswa 105:Historia Ya Kiswahili Question Paper
Lswa 105:Historia Ya Kiswahili
Course:Elimu
Institution: Kenya Methodist University question papers
Exam Year:2012
CHUO KIKUU CHA KIMETHODISTI, KENYA
MTIHANI WA MWISHO WA TREMESTA YA PILI,(MASOMO YA LIKIZO) 2012
KITIVO : ELIMU NA SAYANSI YA JAMII
IDARA : ELIMU
KODI : LSWA 105
ANWANI : HISTORIA YA KISWAHILI
MUDA : MASAA MAWILI
Maagizo:
Jibu maswali matatu.
Swali la Kwanza
Jadili kwa kina huku ukitoa mifano mwafaka nadharia tatu ambazo zinaeleza chimbuko la Kiswahili.
(alama 15)
Eleza upungufu wa nadharia inayodai kwamba Kiswahili ni lugha ya kiarabu.
(alama 5)
Swali la Pili
Fafanua sababu sita zilizosaidia kuenea kwa Kiswahili nchini Tanganyika kabla ya uhuru.
(alama 12)
Eleza kwa kutoa mifano sababu zilizochangia msafara michache ya biashara nchini Kenya ikilinganishwa na nchini Tanganyika.
(alama 8)
Swali la Tatu
Bainisha sababu zilizoifanya lugha ya Kiswahili kusanifishwa.
(alama 4)
Eleza ni kwa nini lahaja ya kiunguja ilichaguliwa kuwa msingi wa kusanifisha lugha ya Kiswahili.
(alama 10)
Je, Pana haja ya kukisanifisha Kiswahili upya? Fafanua kwa kutoa idhibati kamili.
(alama 6)
Swali la Nne
Kiswahili kinatumika katika teknolojia ya sasa ya mawasiliano. Thibitisha dai hili kwa kutoa mifano. (alama 20)
Swali la Tano
Kwa kuzingatia nchi zifuatazo za Afrika ya kati na ulimwenguni kwa jumla, onyesha hali ya sasa ya Kiswahili.
Burundi
(alama 5)
Zaire.
(alama 5)
Sudan.
(alama 5)
Marekani na Dubai.
(alama 5)
More Question Papers