Lswa 105:Historia Ya Kiswahili Question Paper
Lswa 105:Historia Ya Kiswahili
Course:Elimu
Institution: Kenya Methodist University question papers
Exam Year:2011
FACULTY : EDUCATION & SOCIAL SCIENCES
DEPARTMENT : EDUCATION AND PRE-UNIVERSITY
TIME : 2 HOURS
MAAGIZO Jibu Swali la Kwanza na mengine yoyote mawili kutoka yale yaliyosalia
Swali 1
a) Nini maana ya lahaja (alama2)
b) Taja lahaja zozote mbili za bara (alama2)
c) Toa tofauti zozote nne za kimatamshi kati ya Kiswahili sanifu na kimvita. (alama4)
d) Fafanua mchango wa tume ya Mackay katika kuendeleza Kiswahili nchini Kenya. (alama5) e) Kwa nini mapendekezo ya tume ya Koech hayajatekelezwa mpaka sasa. (alama2)
f) Toa mbinu zozote tano za uundaji wa istilahi. (alama5)
Swali 2
Kiswahili ni lugha ya kibantu. Jadili. (alama20)
Swali 3
Nchini Tanganyika wamishonari walikuwa na mchango mkubwa katika maenezi ya Kiswahili. Kuzingatia mifano mbalimbali fafanua kauli hii. (alama20)
Swali 4
a) Ni nini maana ya usanifishaji. (alama2)
b) Fafanua sababu za usanifishaji. (alama8)
c) Tathmini mafanikio na matatizo ya kamati ya usanifishaji ya Kiswahili (ILC) (alama10)
Swali 5
Elezea jinsi Kiswahili kinavyoweza kuimarisha umoja katika Afrika mashariki na kati. (alama20)
More Question Papers