Lswa 105:Historia Ya Kiswahili Question Paper
Lswa 105:Historia Ya Kiswahili
Course:Elimu
Institution: Kenya Methodist University question papers
Exam Year:2013
CHUO KIKUU CHA KIMETHODISTI, KENYA
MTIHANI WA MWISHO WA TREMESTA YA KWANZA, 2013
(MASOMO YA LIKIZO)
KITIVO : ELIMU NA SAYANSI YA JAMII
IDARA : ELIMU
KODI : LSWA 105
ANWANI : HISTORIA YA KISWAHILI
MUDA : SAA MBILI
MAAGIZO:
Jibu maswali yoyote matatu
Swali la Kwanza
Eleza asili ya neno Kiswahili.
(alama 5)
Watafiti wa Kiswahili, kama vile Mbaabu (1985:1) wanasema kuwa kuna Waswahili wa aina tatu. Fafanua kauli hii.
(alama 15)
Swali la Pili
Toa ushahidi wa kihistoria unaothibitisha kuwa Kiswahili ni lugha asili ya Kibantu. (alama 20)
Swali la Tatu
Eleza mambo yaliyochangia hali bora ya Kiswahili nchini Tanganyika ikilinganishwa na Kenya na Uganda (alama 20)
Swali la Nne
Taja na ueleze sababu zinazosababisha Kiswahili kuwa na nafasi finyu nchini Uganda kuliko ilivyo katika nchi ya Kenya na Tanzania. (alama 20)
Swali la Tano
Eleza maana ya ’usanifishaji.’
(alama 4)
Taja na ueleze sababu nne za usanifishaji wa Kiswahili.
(alama 16)
More Question Papers