Lswa 105:Historia Ya Kiswahili Question Paper
Lswa 105:Historia Ya Kiswahili
Course:Elimu
Institution: Kenya Methodist University question papers
Exam Year:2013
CHUO KIKUU CHA KIMETHODISTI, KENYA
MTIHANI WA MWISHO WA TREMESTA YA PILI, 2013
(Mchana)
KITIVO : ELIMU NA SAYANSI YA JAMII
IDARA : ELIMU
KODI : KISW 105/LSWA 105
ANWANI : HISTORIA YA KISWAHILI
MUDA : SAA MBILI
Maagizo:
Jibu maswali matatu
Swali la Kwanza.
Lahaja ni nini?
(al. 2)
Lahaja huzuka vipi?
(al. 5)
Taja lahaja kumi za Kiswahili na kule zinakozungumzwa.
(al. 5)
Eleza sababu za kukisanifisha Kiswahili.
(al. 8)
Swali la Pili
Eleza mchango wa waarabu na waingereza katika kukieneza Kiswahili.
(al. 10)
Waarabu waliacha athari gani katika lugha ya Kiswahili?
(al. 10)
Swali la Tatu
Eleza harakati zinazofanywa na wataalamu wa lugha ya Kiswahili kukikuza Kiswahili ili kitosheleze mahitaji ya mawasiliano katika ulimwengu wa sasa. (al. 20)
Swali la Nne
Sera ya lugha ni nini?
(al. 2)
Linganisha sera za lugha za Kenya, Tanzania na Uganda.
(al. 18)
Swali la Tano
Huku ukitoa mifano eleza maana ya:
(al. 6)
Lingua franka
Lugha rasmi
Lugha ya taifa
Kiswahili ni lugha ya kimataifa. Jadili kauli hii ukirejelea mifano mahsusi.
(al. 14)
More Question Papers