Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kiswahili Mazoezi Ya Marudio. Question Paper

Kiswahili Mazoezi Ya Marudio. 

Course:Secondary Level

Institution: Kcse question papers

Exam Year:2011



MAZOEZI YA MARUDIO (K.C.S.E)

FASIHI SIMULIZI

1. Fasihi ni nini?
2. Andika tofauti nne kati ya fasihi andishi na fasihi simulizi
3. Fasihi ina majukuu gani katika jamii?
4. Jina la jumla la methali, vitendawili, mafumbo na chemsha bongo ni?
5. Eleza sifa tatu bainifu za:
a. Hurafa
b. Hekaya
6. Je, hitimisho katika hadithi huwa na umuhimu gani?
7. Tegua vitendawili hivi:
a. Chauma bila meno, chaumiza bila silaha.
b. Ungataka kukitafuna huwezi, ki hafifu.
c. Daima twamsikia bali hatumwoni
d. Nyumba yangu dogo lakini wapangaji wengi
e. Nyumbani kuna embe lililoiva lakini siwezi kulila.
f. Nimelala huku nikitazama sinema.
g. Huku fungu, huku fungu, katikati bahari.
h. Ana meno lakini hayaumi.
i. Anapovaa miwani haoni vizuri.

8. Nyimbo zina umuhimu gani katika jamii?

ISIMU JAMII
1. Isimu jamii ni nini?
2. Taja mambo matano ambayo huathiri matumizi ya lugha.
3. Kwa kila sajili, taja istilahi maalum zinahusishwa:
a. Nyumbani
b. Mtaani
c. Shuleni
4. Sokoni na dukani ni mahali pa kufanyia biashara. Taja tofauti zinazojitokeza katika sajili hizi.






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers