Kisw 704: Oral Literature In Kiswahili Question Paper

Kisw 704: Oral Literature In Kiswahili 

Course:Masters Of Arts In Kiswahili

Institution: Chuka University question papers

Exam Year:2013





CHUKA

UNIVERSITY

UNIVERSITY EXAMINATIONS
EMBU CAMPUS
MTIHANI WA MASTER OF ARTS
KISW 704: ORAL LITERATURE IN KISWAHILI
STREAMS: MA (SCHOOL BASED) SAA: 3 HOURS
SIKU/TAREHE: WEDNESDAY 17/4/2013 2.30PM – 1.30 PM
MAAGIZO:

JIBU SWALI LA KWANZA NA MENGINE MAWILI

1. (a) Ukirejelea maoni ya wataalam mbalimbali; fafanua dhana ya fasihi simulizi.
[Alama 20]

(b) Fafanua tanzu kuu nne za fasihi simulizi katika Kiswahili ukionyesha vitanzu vya
kila utanzu. [Alama 10]

2. (a) “Kwa kuwa fasihi simulizi imeanza kuhifadhiwa kimaandishi basi imebadilika na
kuwa fasihi audishi.” Jadili. [Alama 10]

(b) Fafanua tofauti tano kuu kati ya fasihi simulizi na fasihi audishi. [Alama 10]

3. (a) Eleza mchango wa fasihi simulizi katika ukuzaji na maendeleo ya jamii.
[Alama 10]

(b) Tanzu nyingi za fasihi simulizi zinafanana na kuingiliana hivyo basi si rahisi
kuziainisha. Jadili maoni haya kwa kutoa mifano. [Alama 10]

4. (a) Fafanua dhana ya nadharia na nafasi yake katika utafiti wa fasihi simulizi.
[Alama 5]
(b) Eleza nadharia zifuatazo kama zinavyotumika katika utafiti wa fasihi simulizi. [Alama 15]
(i) Umabadiliko
(ii) Uenezaji
(iii) Uamilifu


5. (a) Fafanua chimbuko na maendeleo ya fasihi simulizi katika kama utanzu wa fasihi.
[Alama 10]

(b) Ingawa fasihi simulizi huitwa fasihi kongwe, ni dhairi kuwa sanaa hii inaumbwa
upya kila mara. Dhihirisha kauli hii ukitoa mifano katika tanzu mbalimbali za fasihi simulizi. [Alama 10]

6. Muundo ndio msingi baininishi wa tanzu za fasihi simulizi. Dhibitisha kauli hii kwa kutoa mifano kadha wa kadha. [Alama 20]

---------------------------------------------------------------------------------------------------------------------









More Question Papers


Exams With Marking Schemes

Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers