Kiswahili Revision Revisions. Question Paper
Kiswahili Revision Revisions.
Course:Secondary Level
Institution: Kcse question papers
Exam Year:2011
SHINERS GIRLS HIGH SCHOOL
KISWAHILI
1. Andika sentensi zifuatazo upya ukizingatia maagizo yaliyo kwenye mabano.
a. Mazingira yamehifadhiwa. (Hali ya mazoea)
b. Mwalimu anasahihisha kitabu cha mwanafunzi. (Anza kwa: Kitabu)
c. Dhahabu itafuliwa kiwandani. (Wakati uliopita)
2. Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii:
Alimpigia mpira.
3. Tofautisha sentensi hizi kimaana:
Gari liliibwa.
Gari liliibiwa.
4. Kanusha sentensi hizi:
a. Alijitahidi masomoni.
b. Tuliimba tukivuna mahindi.
c. Maharagwe yalivunwa na kutiwa ghalani.
5. Pambanua sentensi hii kwa njia ya mstari.
Nchi iliyo na imani huvutia.
6. Tunga sentensi yenye sehemu hizi:
a. I + N + T + W
b. T + E
7. Andika maneno yenye sauti mwambatano zenye miundo hii:
a. KKI
b. KKKI
c. KKKKI
8. Tunga sentensi zenye miundo hii:
a. KT
b. KN + KT
9. Andika sentensi zifuatazo bila ya kutumia kirejeshi amba-
a. Fulana ambayo imefumwa ni nyekundu.
b. Matendegu ambayo yametengenezwa ni ya kitanda ambacho kilivunjika juzi.
10. Sentensi zinaweza kuwa katika hali tatu: Kwa kila sentensi andika hali zilizokosekana.
a. Goma lililotumiwa katika sherehe zile ni zuri.
b. Mwizi aliyeiba alipatikana amejificha kando ya mto.
11. Panga maneno haya vizuri ili yaunde sentensi sahihi.
a. Hodari yule mwanamuziki nchini amezuru nyingi Africa za.
b. Kompyuta kwa mpya mawasiliano mtandao imerahisisha rununu teknolojia na kupitia wavuti.
12. Tofautisha maneno haya kimaana kwa kuyatungia sentensi:
a. Fasiri, fasili
b. Tunza, tuza.
13. Tunga sentensi mbili kwa kila neno ulilopewa kubainisha maana.
a. Paa
b. Shuka.
More Question Papers
Exams With Marking Schemes
Popular Exams
Mid Term Exams
End Term 1 Exams
End Term 3 Exams
Opener Exams
Full Set Exams
Return to Question Papers