Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Educ 331:Mbinu Za Kufunzia Kiswahili Question Paper

Educ 331:Mbinu Za Kufunzia Kiswahili 

Course:Bachelor Of Education

Institution: Kenya Methodist University question papers

Exam Year:2014



CHUO KIKUU CHA KIMETHODISTI, KENYA

MTIHANI WA MWISHO WA TREMESTA YA TATU, 2014

(MASOMO YA LIKIZO)
KITIVO : ELIMU NA SAYANSI YA JAMII
IDARA : ELIMU
KODI : EDUC 331
ANWANI : MBINU ZA KUFUNZIA KISWAHILI
MUDA : SAA MBILI




Maagizo:

Jibu maswali matatu, swali la Kwanza na mengine mawili.

Swali La Kwanza

Bainisha malengo mawili ya kufunza Kiswahili katika shule za upili.

(al. 2)

Eleza sababu tano za mwalimu kuwa na maazimio ya kazi.

(al. 5)

Fafanua njia zozote tatu ambazo unapaswa kutumia kufanikisha lugha ya wanafunzi katika mijadala.

(al. 3)

Dhihirisha mambo sita ya kuimarisha wanafunzi katika stadi ya kusoma.

(al. 6)

Fafanua sifa mbili za shabaha bora ya kufunzia somo la Kiswahili. (al. 4)

Swali La Pili
Tayarisha maazimio ya kazi ya wiki moja kwa kidato cha kwanza. (al. 20)

Swali La Tatu

Fafanua sababu tano za mwalimu wa Kiswahili kujaza na kuhifadhi rekodi endelezi za kazi.

(al. 10)

Eleza njia tano zinazofaa kufundishia funzo la ufahamu.

(al. 10)

Swali La Nne

Mwalimu wa Kiswahili anapaswa kuwa makini katika uteuzi wa nyenzo za kufunzia. Dhihirisha ukweli huu kwa hoja tano.

(al. 10)

Eleza hoja tano kubainisha umuhimu wa kutahini na kutathimini wanafunzi katika somo la Kiswahili.

(al. 10)

Swali La Tano
Hakiki njia ya mijadala kama mbinu ya kufunzia mafunzo ya Kiswahili sekondari. (al. 20)






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers