Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Kcpe 2008 Kiswahili Question Paper
Kcpe 2008 Kiswahili
Course:Kiswahili
Institution: Kcpe question papers
Exam Year:2008
KCPE 2008
KISWAHILI
SEHEMU YA KWANZA:
LUGHA
Maswali 1 mpaka 15
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo.
Chagua jibu lifaalo Zaidi kati yay ale uliyopewa.
Kwa---1---Kiswahili ni lugha ya Kiafrika ambayo imeenea kote.
Wenyeji asilia—2---wakiongea lugha hii—3—awali ni Waswahili. Waswahili wanapatikana kote katika upwa mzima---4---pwani ya Afrika Mashariki. Kwa muds mrefu Kiswahili ----5---humu nchini lakini mambo yamebadilika.Lugha hii sasa imepewa hadhi---6---nyanja mbalimbali nchini. Lugha hii---7—pakubwa kuwaunganisha wananchi na kudumisha Amani. Wakenya wengi wamejitolea kuikuza lugha hii yao na hawataki tena---8---
1.A. Sababu
B. Hivyo
C. Hakika
D. Vile
2. A. Wamekuwa
B. Waliokuwa
C. Watakaokuwa
D. Wangekuwa
3. A. Tangu
B. Hadi
C. Hata
D. Mpaka
4. A. Wa
B. Kwa
C. Ya
D. Mwa
5. A. Hakikudhaminiwa
B. Haikuthaminiwa
C. Haikudhaminiwa
D. Hakikuthaminiwa
6. A. Katika
B. Kati ya
C. Ndani ya
D. Kuliko
7. A. Imechanga
B. Imechangiwa
C. Imechangia
D. Imechangisha
8.A. Kuizungumza
B. Kuitwaza
C. Kuitumia
D. Kuididimiza
Arusi ya Hadija—9---kijijini mote.
Nyimbo zilisikika kwa siku tatu mfululizo. Vigoli na maghulamu walicheza ngoma bila kusita---10. Ya magari ilionekana—11—kuelekea msikitini kwa sherehe kufunga ndoa. Kijiji chote kilijaa wageni—12---kutayarisha arusi. Nyumba ya bibiarusi ilijaa mapambo tele na kuta—13—kupakwa rangi ya kupendeza.
Arusi ikawa ya kufana mno. Watu—14--. Hata baada ya---15---nilienda nikijisemea kimoyomoyo, “Jambo la heri huenda kwa heri. Mola awajalie mema.”
9. A. Ilitia chumvi
B. Ilitia fora
C. Ilipiga mbiu
D. Ilipiga debe
10. A. Safu
B. Milolongo
C. Msongamano
D. Msitari
11. A. Ikiandamana
B. Ikifuatia
C. Ikifuatwa
D. Ikiandama
12. A. Walivyokuja
B. Walipokuja
C. Waliyokuja
D. Waliokuja
13. A. Yoyote
B. Yote
C. Zote
D. Zozote
14. A. Wameiajabia
B. Wanaiajabia
C. Wakaiajabia
D. Wakiiajabia
15. A. Kutangamana
B. Kujumuika
C. Kufungamana
D. Kufumukana
Kutoka swali la 16 mpaka 30,chagua jibu lililo sahihi.
16. Chagua usemi wa taarifa ulio sahihi wa
“Kilele cha Mlima Kenya kina theluji nyingi.”
A. Fatuma alisema kwamba kilele cha Mlima Kenya kilikuwa na theluji nyingi
B. Fatuma anasema kwamba kilele cha Mlima Kenya huwa na theluji nyingi
C. Fatuma akasema kwamba kilele cha Mlima Kenya kimekuwa na theluji nyingi
D. Fatuma alisema kwamba kilele cha Mlima Kenya kingekuwa na theluji nyingi
17. Ni sentensi ipi inayoonyesha matumizi sahihi la Lau?
A. Lau mwanafunzi anapopita mtihani hutuzwa
B. Lau ungekuja ningekusaidia
C. Nipe lau kitabu kimoja nisome
D. Nitakujuza lau hutaki kujua
18. Chagua jibu linaloonyesha aina za mashairi.
A. Tarbia,Takhmisa
B. Tarbia,Mizani
C. Vina,Takhmisa
D. Takhmisa,Mishororo
19. Chagua kinyume cha sentensi:
Musa alisifiwa kwa utiifu wake.
A. Musa hakusifiwa kwa utiifu wake
B. Musa alikashifiwa kwa utundu wake
C. Musa alikashifiwa kwa ukaidi wake
D. Musa Hakukashifiwa kwa ukaidi wake.
20. Methali yenye maana sawa na “usiache mbachao kwa msala upitao” ni
A. Usione kwenda mbele kurudi nyuma si kazi
B. Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi
C. Usipoziba ufa utajenga ukuta
D. Bora yangu siibadili na rehani
21. Jogoo ni kwa koo,fahali ni kwa
A. Ndama
B. Kipora
C. Tembe
D. Mtamba
22. Chagua aina ya pambo ambalo huvaliwa miguuni.
A. Kipete
B. Kidani
C. Kikuku
D. Kikuba
23. Umoja wa sentensi “Waungwana wowote hawawezi kutufanyia fujo” ni
A. Muungwana yeyote hawezi kutufanyia fujo
B. Muungwana yeyote hawezi kunifanyia fujo
C. Muungwana yoyote hawezi kunifanyia fujo
D. Muungwana yoyote hawezi kutufanyia fujo
24. Chagua sentensi ambayo ni muungano sahihi wa hizi:
Mburukenge aliingia uwanjani.
Mburukenge aliwafadhaisha wanafunzi.
A. Mburukenge aliingia uwanjani na kuwafadhaisha wanafunzi
B. Mburukenge aliingia uwanjani kwa kuwafadhaisha wanafunzi
C. Mburukenge aliingia uwanjani lakini aliwafadhaisha wanafunzi
D. Mburukenge aliingia uwanjani kwani aliwafadhaisha wanafunzi
25. Kumpiga mtu vijembe ni
A. Kumpa sifa asizostahili
B. Kumsema kwa mafumbo
C. Kumchafulia mtu jina
D. Kumfanyia ishara ya dharau
26. Ugonjwa wa ukambi pia huitwa
A. Surua
B. Safura
C. Ndui
D. Tetewanga
27. Sahihisha: Kule mlikolima hamna rutuba.
A. Kule mlipolima hamna rutuba
B. Pale mlipolima hamna rutuba
C. Kule mlikolima hakuna rutuba
28. Chagua nomino kutokana na kitenzi kumbuka:
A. Kumbukika
B. Kumbukwa
C. Kumbusha
D. Kumbusho.
29.Umbu,mkoi,halati,wote ni
A. Jamii
B. Wakwe
C. Jamaa
D. Marafiki
30. Kitendawili “Nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayuko,” jibu lake ni
A. Mwanga
B. Kivuli
C. Mwangwi
D. Upepo
Soma kifungu kifuatacho kasha ujibu maswali 31-40
Uamuzi uliofanywa na serikali wa kuhimiza watoto wote warudi shuleni ni jambo mwafaka.
Watoto walifurika furifuri shuleni ili kusajiliwa. Wale waliokuwa wakirandaranda mitaani walifuatilizwa himahima na kupelekwa shule. Waliokuwa wakubwa ki-umri walipelekwa kwenye shule za ufundi.
Wakatabasamu kwa furaha kama mzazi aliyepata salama.
Kwa miaka mingi, baadhi ya wazazi walikuwa wameshindwa kuwasomesha wana wao. Hii ni kutokana na umaskini uliokithiri mipaka. Hali hiyo ilichangia huzuni kuu miongoni mwa fimilia. Pengo la waliosoma lilizidi kuwa pana kielimu na kiuchumi. Uadui ukaingilia jamii. Ujambazi nao ukazidi.
Sasa watu wote wakipewa haki sawa ya kusoma hata wale watoto wa maskini watamanio masomo watakinaisha kiu yao.
Pia mengi ya matatizo yatapungua. Si kweli kuwa tajiri ni mwerevu kuliko mkata. Kila mwanajamii akipewa nafasi na asome kwa bidii atafua dafu maishani.
Vijana watakaofuzu katika shule za kiufundi wataweza kuajiriwa katika sekta mbalimbali. Mwishowe wakipata mtaji watajiendeleza kwa kuanzisha miradi midogomidogo ya kujitegemea. Hali kama hii ikiena kote nchini viwanda vidogovidogo vitaanzishwa na ajira itapatikana. Hiyo itakuwa njia mojawapo kuu ya kuinua uchumi na kuzalisha nafasi nyingi za kazi
Kitaaluma, hawa vijana wataweza kuwa madaktari, wasanii, walimu….na kazi zingine nyingi. Kisomo ni kitamu. Hakifai kutiliwa nanga.
31. Uamuzi uliofanywa na serikali
A. Ulisababisha kufurika kwa watoto shuleni na kupita mitihani.
B. Ulisababisha kuchipuka kwa vyuo vya ufundi na kuondoa umaskini
C. Ulisababisha kuongezeka kwa watoto shuleni na kupata nafasi ya kujiendeleza
D. Ulisababisha kupungua kwa umaskini na kuwapa watoto nafasi ya kujiendeleza
32. ----baadhi ya wazazi walikuwa wameshindwa kuwasomesha wana wao.
Chagua methali inayoweza kuelezea hali hii
A. Maskini kupata ni mwenye nguvu kupenda
B. Dau la mnyonge haliendi joshi
C. Ng’ombe wa maskini hazai pacha
D. Maskini halali mchana
33. Ukosefu wa walimu unasababisha
A. Umaskini,uadui,huzuni na ujambazi
B. Wivu,ujambazi,kukosa kiu ya kusoma na uadui
C. Utajiri,ukosefu wa kazi, huzuni na ujambazi
D. Ujambazi, wivu, utajiri na kiu ya kusoma
34. Kulingana na kifungu,pengo kubwa la kiuchumi limesababishwa na
A. Watoto kutopata kisomo kwa sababu ya umaskini
B. Uadui na ujambazi uliokumba jamii maskini
C. Watoto kutopelekwa shule za ufundi kwa sababu ya umaskini
D. Wazazi kushindwa kupambana na umaskini
35. Ni kweli kuwa watu wote wakipewa nafasi sawa
A. Watoto wa maskini watakuwa werevu
B. Watoto maskini na tajiri watakuwa sawa
C. Watoto wote wapendao kusoma watakuwa matajiri
D. Watoto wote wapendao kusoma watapata kisomo.
36. Vijana wote wakipata mtaji:
A. Wataanzisha miradi ya kiufundi
B. Wataweza hata kuwa wataalamu
C. Wataanzisha shughuli za kujikimu
D. Watakitilia kisomo chao makini
37. Kisomo hakifai kutiliwa nanga kwa sababu
A. Watu watakuwa wataalamu
B. Kina manufaa mengi
C. Shule zitapanuka
D. Serikali itakigharamia
38. Maana ya kusajiliwa ni:
A. Kurekebishwa
B. Kunufaishwa
C. Kuandikishwa
D. Kufundishwa
39. Watakinaisha kiu yao in maana ya:
A. Watapunguza tamaa yao
B. Wataacha hofu yao
C. Watafurahia hali yao
D. Watatosheleza hamu yao
40. Kichwa kinachofaa Zaidi kwa taarifa hii ni:
A. Ukarimu wa serikali
B. Kupunguza ujinga
C. Masomo ya kiufundi
D. Serikali kupanua masomo
Soma taarifa hii kasha ujibu maswali 41 mpaka 50.
Wanafunzi wa shule ya Mtepetevu walitembelewa na wazazi.
Kabla ya kuruhusiwa kukutana na watoto wao,wazazi waliingia kwenye mkutano.
Takriban kila mzazi alimbebea mwanawe furushi la chakula, licha ya kuwa watoto wao walikuwa wamerudi kutoka nyumbani majuma mawili tu yaliyopita.
Mkutanoni wazazi walizozana kuhusu maakuli shuleni,mavazi na mitindo ya nywele ya watoto hao.
Baadhi walitaka watoto wao wapewe mapochopocho na matunda ghalighali. Wengine wao siku hiyo hawakufikiria sana kuhusu juhudi za watoto masomoni, kinyume na kawaida yao. Hata hivyo,wengi wao waliona mbele,wakapina udekezaji huo.
Mzozo ulipokuwa ukipamba moto,kijana mmoja wa karibu miaka ishirini na minne, aliyekuwa amevalia kilalahoi, akaingia mkutanoni. Baadhi ya wazazi waliomuona walishindwa kwani mkutano ulikuwa wa wazazi. Kijana akaketi na kutega sikio.
Mzazi mmoja alisimama na kusema, “Nimeitazama orodha hii ya vyakula na nimesikitika. Kwa nini hawa watoto hawapewi chapatti kwa kima,pilau na ‘matoke’? Tunalipa! Sasa kwa nini wanakula ugali na ‘githeri”.
Kijana yule alikerekwa,akaunyoosha mkono juu sana na alipoona anapuuzwa,akasimama na kuanza kusema, “Hoja mnazotoa si…..” Baadhi ya wazazi wakamdakia na kusema, “We! Nyamaza. U mtoto! U mkwe wetu…” Kijana akazidi kukakawana na kutaka kupewa nafasi lakini wale waliokuwa karibu naye wakamlazimisha kuketi. Mwenyekiti akasema, “Huu ni mkutano wa wazazi.Jukumu lako kijana ni kunyamaza na kusikiliza kwa makini,kasha uwapelekee wazazi ujumbe.”
Kijana alikazana, “Tafadhali nipeni ruhusa. Kitanda msichokilalia,hamuwajui kunguni wake.” Akaulizwa walikokuwa wazazi wake kwani ndio waliotakiwa mkutanoni. Akajibu, “Bwana Mwenyekiti,sina wazazi! Mimi ni mlezi wa wadogo zangu, nina mdogo wangu hapa. Nimetoka mbali huko kote kuja kuwawakilisha marehemu wazazi wangu. Mimi si mlevi, si mhuni au mkwe wenu. Nina akili razini.
Kuwa kijana si dhambi. Nimemaliza chuo kikuu. Nina kazi lakini mshahara wote unaishia kwenye malezi na sasa mnanikataza kusema lolote. Je, kijana hana haki? Ninajua kuwa maji mengi hayazuiliki lakini tushirikianeni kwani penye wengi hapaharibiki neno”.
Mwenyekiti akampa nafasi ya kujieleza: Kijana akaendelea, “Mimi kijana mlezi, nimewasikiliza kwa makini. Ninapinga hoja ya mavazi ya nyumbani na mapochopocho kama chapatti……Jambo linalofaa ni kuwafunza kutafuta elimu kwa bidii.
Wakihimizwa kuwa na adabu na kuwa na kiu ya masomo,watajikataza wenyewe kufuata tu raha maishani. Kula bila kujua kutafuta kutawatia mashimoni. Mvumilivu hula mbivu.
Kugeuza mandhari ya shule kuwa ni sehemu ya mandarin kutajenga uvivu,wizi, matabaka na wivu shuleni. Wanafunzi watawabeza walimu,badala ya kuwasikiliza. Tuwafunze kujitegemea” Wazazi walimhurumia na kumpigia makofi. Mwenyekiti akamuomba msamaha na kumshukuru kwa niaba ya wazazi.
41. Ni jambo gani linaloonyesha kuwa hawa watoto wanadekezwa?
A. Ingawa walikuwa hawajakaa sana shuleni, wazazi waliwabebea mafurushi ya vyakula.
B. Walikuwa wametoka nyumbani na mafurushi ya vyakula.
C. Wazazi walikuwa wanataka watoto wale mapochopocho,sio tu kuvaa kifahari
D. Wazazi walikuja mpaka shuleni kuwaona watoto hao na vyakula
42. Ukipamba moto maana yake ni:
A. Ukiwa na joto jingi
B. Ukizidi kuendelea
C. Ukiharibika
D. Ukihimizwa
43. Mkutanoni kulikuwa na:
A. Wapinzani,mwenyekiti na kijana
B. Waungaji mkono,kijana na mwenyekiti
C. Wadekezaji,waona mbele na mwenyekiti
44. Kijana alipuuzwa kwa sababu ya
A. Mavazi yake
B. Mazungumzo yake
C. Umri wake
D. Kutaka kuongea
45. Kwa nini kijana alikazana kunyoosha mkono?
A. Alikata kuondoa shaka ya wazazi na kutoa hoja zake
B. Alitaka kusema kuwa yeye ni mlezi si mkwe
C. Alikasirika na kutaka kupingana na wazazi
D. Alikasirika kwa kudharauliwa akataka ajitambulishe
46. Hoja za kijana zilionyesha:
A. Ukaidi wake
B. Ulala hoi wake
C. Ukomavu wake
D. Ujana wake
47. Kulingana na kifungu kitanda msichokilalia hamuwajui kunguni wake ina maana
A. Wazazi hawajua matatizo ya watoto
B. Wazazi hawakujua hali ya kijana
C.Wazazi hawakuamini hoja za kijana
D. Wazazi hawakuamini maoni ya watoto
48. Kulingana na taarifa hii wazazi walipaswa
A. Kujadili jinsi watoto wao walivyokula,walivyovaa na kuwa na mandarin shuleni
B. Kuzungumzia nidhamu na jinsi ya kuwahimiza walimu kuwapa watoto chakula cha kifahari
C. Wakomeshe udekezaji,wahimize nidhamu na kuacha kutaka kugeuaza shule kuwa ni mandarin
D. Kuondoa udekezaji na rah azote zilizokuwapo shuleni kama mavazi ya kifahari na lishe bora
49. Mpangilio bora wa matukio ya siku hiyo huko Mtepetevu ulikuwa
A. Kuwasili, kuingia mkutanoni, kuzozana,kuelewana na kuomba msamaha
B. Kuwasili,kuzozana,kuomba msamaha,kuingia mkutanoni na kuelewana
C. Kuwasili,kuingia mkutanoni,kuelewana,kuzozana na kuomba msamaha
D. Kuwasili,kuzozana, kuingia mkutanoni,kuomba msamaha na kuelewana
50. Kichwa mwafaka kinachofaa kuelezea taarifa hii ni:
A. Dhifa ya wazazi shuleni
B. Ujana shuleni si hoja
C. Mzozo na mapatano shuleni
D. Kudunishwa kwa vijana shuleni
More Question Papers