Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kisw 211: Fonetiki Na Fonolojia Question Paper

Kisw 211: Fonetiki Na Fonolojia 

Course:Fonetiki Na Fonolojia

Institution: Egerton University question papers

Exam Year:2014



JIBU SWALI LA KWANZA NA MENGINE MAWILI

SWALI LA KWANZA

(a) Fonimu ni nini? (Alama 2)
(b) Fafanua kwa kifupi dhana ya fonimu kama tukio la: (Alama 12)
(i) kifonolojia
(ii) kisaikolojia
(iii) kifonetiki
(c) Pambanua nafasi ya virindima vifuatavyo katika kubadili mikondo-hewa kuwa nguvu
sikizi (Alama 16)
(i) nyuzi za sauti
(ii) kilimi
(iii) ulimi
(iv) midomo

SWALI LA PILI

(a) Tofautisha baina ya fonolojia arudhi na fonolojia vipande-sauti (Alama 4)
(b) Kwa kutoa mifano mwafaka, fafanua mifanyiko ifuatayo ya kifonolojia; (Alama 16)

SWALI LA TATU

(a) Jadili dhana ya irabu-msingi kwa kerejelea jedwali la IPA. (Alama 8)
(b) Eleza jinsi sauti za irabu hutamkwa kwa kuzingatia sifa bainifu zifuatazo (Alama 12)
(i) mwinuko wa ulimi
(ii) mkao wa midomo

SWALI LA NNE

(a) Fafanua matamshi ya sauti zifuatazo kwa kuzingatia sifa ya mahali na hali ya
mkondohewa; (Alama 20)
(i) vizuiwa
(ii) vikwamizo
(iii) ving'ong'o
(iv) likwidi
(v) viyeyusho

SWALI LA TANO

(a) Fafanua dhana ya alofoni kwa kuitolea mifano (Alama 4)
(b) Eleza jinsi mbinu hizi zinavyoweza kutumiwa kutambulisha fonimu za lugha ya
Kiswahili (Alama 16)
(i) mfanano wa kifonetiki
(ii) jozi ya mlinganyuo-finyu
(iii) mgawanyo wa kamilishani






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers