Kiswahili Poetry Question Paper
Kiswahili Poetry
Course:Bachelor Of Education
Institution: Jaramogi Oginga Odinga University Of Science And Technology question papers
Exam Year:2013
CHUO KIKUU CHA JARAMOGI OGINGA ODINGA - BONDO
IDARA YA KISWAHILI NA LUGHA NYINGINE ZA KIAFRIKA
MWAKA WA PILI SEMISTA YA PILI
AGOSTI–DESEMBA 2013
(MAIN–SCHOOL BASED)
COURSE CODE: AKI 204
COURSE TITLE: KISWAHILI POETRY
DATE: 30/8/2013 TIME: 9.00-11.00 AM
DURATION: 2 HOURS
MAAGIZO:
Jibu maswali matatu, swali la kwanza ni la lazima.
OASIS OF KNOWLEDGE
1(a) Huku ukizingatia vipengele maalumu, fafanua dhana ya "ushairi wa Kiswahili."(Alama 10)
(b) Bainisha sifa kuu zinazotofautisha ushairi wa kimapokeo na ushairi huru. (Alama 10)
(c) Fafanua kwa kina nadharia mbili zinazotumiwa na wataalamu kuelezea chanzo cha
ushairi wa Kiswahili. (Alama 10)
2 Talii mabadiliko ya kimaumbo katika ushairi wa Kiswahili kufikia sasa. (Alama 20)
3 Huku ukirejelea mifano mwafaka, eleza mashairi yafuatayo:
(a) Tenzi (Alama 5)
(b) Wimbo (Alama 5)
(c) Ukawafi (Alama 5)
(d) Shairi huru (Alama 5)
4 "Utenzi wa Mwanakupona unamdhalilisha mwanamke." Jadili ukweli wa kauli hii. (Alama 20)
5 Jadili dhana ya "kichomi" katika diwani ya Kichomi (E. Kezilahabi, 1974).(Alama 20)
More Question Papers