Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kiswahili Form 1 Question Paper

Kiswahili Form 1 

Course:Secondary Level

Institution: Kcse question papers

Exam Year:2006



SHULE YA UPILI YA WASICHANA - IGUNGA

MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA WA PILI

KISWAHILI KIDATO CHA KWANZA

UFAHAMU
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali

Kwa muda mrefu tulikuwa tukivutana, si kwa sababu ya kutoheshimiana au kuchukiana bali kwa sababu ya mapokeo tofauti na kushindwa kukabiliana na maisha - pambano lote lililomea juu ya mti uitwao ''kazi'' katika mapokeo yangu juu ya mti huo, nilichukua matawi mawili mawili makubwa. Sikuelewa wema sababu iliyomfanya mama aingilie kati na kuniachisha raha za michezo ili niende kutekeleza kazi fulani hapo nyumbani. Aling''ang''ania kunituma kazi ambazo nilionyesha dalili dhahiri za kuzichukia. Mambo haya yamenikera kwa muda mrefu kwani mimi kama vijana wengine nilitamani kukaa raha mustarehe. Nilichelewa kugundua kuwa mtu mkunguni huhepa kazi zile za sulubu akijidai kuwa anaona raha. Raha hii hutafutwa sana hata kama itawakefyakefya wengine. Nilikosa kujua kuwahudumia wazazi kulinitayarisha kuwa mtu bora, mwenye kukubalika katika taifa, kuwa kielelezo kwa wengine, na kuwa mzazi na kiongozi bora wa kesho. Sikufahamu katika ubongo wangu wa kitoto kuwa nchi hustawishwa na kazi na bidii ya wazalendo wake. Kwa hivyo pambano letu liliendelea isipite siku bila manung''uniko. Katika juhudi ya kuepuka kazi ya kuteka maji nilijitahidi kupasua kila kibuyu nilichokabidhiwa lakini hazina ya zao hili ilinishangaza.

Nilipokuwa madikia kuwa barubaru tosha, malalamiko yangu yakiendelea kutafsiriwa na vitendo, mama alinikalisha kitako na kunieleza kuwa, ikiwa nitakuwa kijana na kujitegemea na kutegemewa basi itabidi nifuate waadhi wake.
''Ili usije tekwa na ushababi na kuwa habithi, nakusihi uwe na mawazo sahihi kuhusu kazi.'' Mama alisema. Aliendelea kunieleza kuwa kazi ni maisha, bila kazi hakuna maisha. Mtu huambiwa amekufa ikiwa viungo vyake havifanyi kazi. Kukataa kazi ni kujitakia kifo. Vijana wengi kwa kupotoka kwao hususia kazi na kujitosa katika anasa ambapo wao hukwama katika sharabu kali za aina nyingi. Hujikuta wametumbukia majanga makubwa wakiwa katika hekaheka za kutafaraji. Hali nzuri ya roho hustareheka haizuki kwa mtu, lazima kuwa na maandalio kabla ya mtu kupata raha. Na hata baada ya kuipata, jukumu liko bado kuliendeleza. Bila jitihada ya kuendeleza jukumu hili mtu huishia kuwa ovyo.

Uchunguzi uliofanywa ulionyesha kuwa watoto wasiofunzwa kufanya kazi kidogo kidogo katika kukua kwao, ndio hukabiliwa na matatizo ya kuwa watu wasio na nidhamu katika taifa. Wengi wao huwa wahuni na wavunjaji wa sheria, na baadaye huwa wazazi wasioweza kutoa mafunzo bora kwa watoto wao wenyewe.

MASWALI
a. "Hazina ya mama...ilinishangaza"
Fafanua usemi huu (al. 3)

b. Eleza manufaa manne yanayotokana na kuwatumikia wazazi (al. 4)

c. Fafanua hatari zinazotokana na kufanya kazi mtu akiwa mtoto (al. 3)

d. Mwandishi alikuwa na manung''uniko gani katika kukua kwake (al. 3)

e. "Mtu mkunguni" ni mtu wa aina gani (al. 3)

f. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika taarifa (al. 5)

i. Harakati
ii. Yanikera
iii. Sulubu
iv. Barubaru
v. Hususia

g. Andika kichwa cha taarifa hiyo (al. 2)

MATUMIZI YA LUGHA
1. Tambua na kubainisha vivumishi vilivyo katika sentensi zifuatazo (al. 10)

i. Viatu vyeusi viliwapendeza wasichana.

ii. Mahali humu mnaingia wezi.

iii. Maji yalipatikana pahali pachache sana.

iv. Kuimba kwenu kunasisimua.

v. Ni nyavu zipi zilizotumika kuvulia samaki?

2. Kamilisha sentensi zifuatazo kwa kuunga viambishi vifaavyo (al 10)

i. Kitabu __le __refu __na mambo mengi.

ii. Jina __lilotangazwa redioni __ refu.

iii. Mahali ha__ ndi__ ali__patikana.

iv. Chuo __kuu __a walimu __tajengwa

v. Milango yote __livunjika __lipokuwa __safirishwa.

3. Eleza maana ya misemo ifuatayo (al.6)

a. Mtu wa miraba minne

b. Lala kifudifudi

c. Tia fora

4. Toa maana mbili za maneno yafuatayo (al. 4)

i. Mbuzi

ii. Kaa

5. Kamilisha tashbihi zifuatazo (al. 5)

a. Yule mvulana ni nyeusi kama ______

b. Mtoto yule ni mkaidi kama ______

c. Siti aliimba usiku na mchana kama ______

d. Huyu mwanaume ni mjanja kama ______

e. Yule mbilikimo ni mfupi kama ______

6. Kamilisha methali zifuatazo (al. 5)

a. Achanikaye kwenye mpini ______

b. Kila chombo ______

c. ______ wakunga na uzazi ungalipo

d. ______ tembo hulitia maji

e. ______ jembe si mkulima

7. Chagua neno lifaalo kutoka kwenye mabano kukamilisha sentensi zifuatazo (al. 5)

a. Aliji ______ hadhi yake alipoanza kutukana watu waliohudhuria (shusha, shuka)

b. Tajiri yule ana ______ vijakazi wake kazi kama punda (fanyiza, fanyika)

c. Mtu yule ana sura mbaya yenye ku ______ (ogopana, ogofya)

d. Hajani ______ bado kuhusu jambo hili (juvya, julika)

e. Mkuu wa kijiji aliwa ______ vijana dhidi ya kutembea usiku (kanya, kana)

Sentensi zifuatazo zina makosa. Zisahihishe (al. 5)

a. Kule ndimo alikoingia.

b. Humo chumbani ndiko mlimorembeshwa.

c. Mle ndimo alipofungiwa.

d. Maji yapo mtungini.

e. Mahali huku ni mzuri.






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers