Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kis 218: Kiswahili Kwa Wanahabari Question Paper

Kis 218: Kiswahili Kwa Wanahabari 

Course:Bachelor Of Science In Communication And Journalism

Institution: Moi University question papers

Exam Year:2013



1. a. Eleza kwa kina matatizo yaliyomo katika kila moja ya anwani hizo
i. Polisi walimhoji mshukiwa katika wizi jana
ii. Wazee wa kaya waandamana na kutaka haki kuhusu suala la ardhi (Katika Taifa Leo, Oktoba, 3, 2012)
b. Ziboreshe anwani hizo kwa kuziandika kwa muundo na mtindo ufaao.
c. Bainisha tofauti za maana zilizomo katika anwani zifuatazo
i. Mombasa Academy nambari moja nchini katika rekodi za upigaji mbizi (Taifa Leo, Julai, 2, 2012)
ii. Upigaji mbizi; Mombasa Academy nambari moja
d. Eleza kwa kifupi athari ya miundo hii kwa uendelezaji wa ujumbe

2. Pambanua namna vyombo vya habari vinaweza kuchangia kukua kwa Kiswahili kama kitambulisho cha taifa

3.Ukitumia mifano mwafaka eleza kwa kina sababu zozote nne zinazoathiri matumizi ya Kiswahili sanifu katika uwanja wa uwana habari

4. Ukitumia mifano faafu, fafanua hoja ya kwamba, "uteuzi wa maneno huathiri kiwango cha mawasiliano"

5. a. Fafanua maana ya dhana ya vitenzi na ueleze sura zake mbalimbali
b. Eleza namna vitenzi hutumika na kubainika katika, anwani za magazeti na vile vile katika, ripoti za michezo. Toa mifano mitatu kwa kila moja ya sehemu hizo

6. Ukitumia mifano mwafaka changanua umuhimu wa kipengele cha mshikamano katika uandishi wa habari. Toa hoja nne.






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers