Form 1 Kiswahili Term 1 2017 Question Paper

Form 1 Kiswahili Term 1 2017 

Course:Kiswahili

Institution: Form 1 question papers

Exam Year:2017



Kanga high SCHOOL
KIDATO CHA KWANZA

JINA…………………………………………….…NAMBARI……..KIDATO……

JIBU MASWALI YOTE:
SWALI LA 1: UFAHAMU: (AL.15)

Asilimia kubwa ya mataifa ya ulimwengu yamefikia ngazi za juu katika maendeleo ya afya ya umma katika miaka thelayhini iliyopita. Kuna sababu nyingi ambazo zimesababisha hali hii. Moja kati ya sababu hizi ni kuwako kwa ufahamu wa kina kuhusiana na magonjwa na vyanzo vyake. Pili, kuwako kwa njia wazi za utambuzi wa makundi yanayoathirika na magonjwa Fulani. Tatu, utekelezaji na usambazaji wa maarifa pamoja na uhamasishaji wa makundi yanayohusika kubadili tabia zao au kuchukua hatua bora za kiafya. Msemo wa kuwa ni heri kuzuia kuliko kutibu umekuwa nguzo kuu ya matendo hayo.

Hata hivyo hali kama hii haionekani kuhusiana na suala la usalama wa umma. Katika miji mingi ulimwenguni, hususan ile mikubwa, viwango vya uhalifu vimepanda. Ghasia zinazohusiana na vijana, ukosefu wa usalama kwa watoto na wanawake, wizi wa magari, uvunjaji wa nyumba, utumiaji wa nguvu, wizi wa mabavu na ukosefu wa usalama kwa jumla, yamekuwa matatizo sugu. Je, ni kwa nini hali ikawa mbaya kiasi hiki ?

Hali hii inatokana na mambo mengi. Mojawapo ni upungufu wa njia asilia za kuukabili uhalifu kama polisi, mahakama na magereza. Pili, ni kutochunguza na kujaribu kusuluhisha matatizo ya kimsingi yanayochangia kuwako kwa uhalifu.

Usalama wa umma ni moja kati ya vigezo vya kimsingi vya maisha bora pamoja na maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Usalama huu unapaswa kuzingatiwa kama msingi muhimu na kila mwanajamii ana jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa umepatikana. Suala la uhalifu sio suala la polisi na mfumo wa utendaji haki tu. Ili kufanikiwa katika uzuiaji wa uhalifu, lazima washika dau wote wahusike katika suala hii. Je, ni mambo gani tunayopaswa kufanya ili tuzuie uhalifu ? Kwanza, pana haja kubwa ya kuchunguza na kuielewa barabara misingi ya uhalifu na ghasia za mijini. Baada ya kuchunguza pana haja ya kuchukua hatua zitakazosaidia kupunguza idadi ya waathiriwa na jamii ya wahalifu mijini. Hatua hizi ni kama kuwako kwa muundo mzuri na salama wa miji, kusaidia watoto na jamaa zisizokuwa na uwezo, kuhimiza uwajibikaji wa jamii, kuzalisha kazi za kuwaajiri vijana, kuhakikisha baadhi ya huduuma kama za polisi na utekelezaji wa haki zimetegemezwa kwenye jamii, kuwawezesha wahalifu kuyarudia maisha ya kawaida na kuwasaidia waathiriwa wa uhalifu.

Pili, njia za kuzuia uhalifu lazima zihusishe sehemu zote za jamii kama polisi, mfumo wa utendaji haki, huduma za kiafya na kijamii, huduma za makazi, sekta ya kibinafsi na mashirika ya umma.


Uzuiaji wa uhalifu unachangia kuleta umoja, ushirika wa raia na utawala ufaao. Unachangia kwa kiasi kikubwa katika ukuzaji na uendelezaji wa taasisi za kidemokrasia, uwajibikaji wa huduma za umma kama polisi na mfumo wa utendaji haki. Kama ilivyo kuhusiana na ugonjwa ni heri kuzuia kuliko kutibu. Vivyo hivyo, uzuiaji wa uhalifu ni bora kuliko kuukabili na kuutibu uhalifu wenyewe.

MASWALI:

(a) Kwa nini maendeleo ya afya yameimarika ? Toa sababu tatu. (al.3)





(b) Kulingana na kifungu hiki, taja uhalifu aina tatu unaothibitisha kwamba hali ya usalama ni mbaya. (al.3)













(c) Jamii inafaa kufanya nini ili kushiriki katika kulinda usalama wao ? (al.3)










(d) Taja faida mbili za uzuiaji wa uhalifu. (al.2)






(e) Onyesha maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika taarifa.)al.4)
(i) Umma …………………………………………………….

(ii) hususan ………………………………………………………

(iii) Matatizo sugu ……………………………………………….

(iv) Uhalifu ………………………………………………………..

SWALI LA 2: MATUMIZI YA LUGHA (AL.35)

A: Eleza maana ya:

Kiimbo –

Shadda –


B: Onyesha shadda katika maneno yafuatayo. (al.1)
maharagwe…………………………………………………………… (al.1/2)

(ii) mama ………………………………………………………………… (al.1/2)

C: Andika konsonanti mbili zinazotamkiwa katika viungo vifuatavyo vya
kutamkia. (al.8)
midomo na meno –

meno

kaakaa gumu –

kaakaa laini –

D: Ni nini tofauti baina ya: (al.4)

¦p¦ na ¦b¦



(ii) ¦dh¦ na ¦th¦

E: Bainisha maneno mbalimbali katika sentensi hizi. (al.3)
Tulifika jana.




Watahiniwa wote walipita mtihani.



F: Kamilisha methali zifuatazo. (al.3)
Mcheza na tope –

Mbio za sakafuni –

Dunia rangi –

G: Taja majukummu manne ya fasihi.






H: Andika maneno mawili yaliyo na silabi za irabu pekee. (al.2)



(I): Tunga sentensi kubainisha maana tofauti ya vitate vifuatavyo. (al.2)

Doa –

Ndoa –

J: Andika maneno mawili yenye silabi mwambatano zifuatazo: (al.6)
Konsonanti, nusu irabu na irabu


Konsonanti, konsonanti na irabu.


Konsonanti na irabu









More Question Papers


Exams With Marking Schemes

Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers