Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kiswahili Form 1 Question Paper

Kiswahili Form 1 

Course:Secondary Level

Institution: Kcse question papers

Exam Year:2006



KISWAHILI KIDATO CHA KWANZA
MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA

SEHEMU YA KWANZA: UFAHAMU

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.

MAJI
Ni muhimu tutafute njia za kuhifadhi maji ili kila wakati tuwe na akiba yake ya kutumia wakati wa kiangazi. Kuna njia nyingi za kuhifadhi maji. Baadhi ya njia hizo tutaendelea kuzitaja kwa ufupi. Maji hutokana na mvua. Ikiwa basi tutahifadhi akiba ya maji ya kutumia wakati wa kiangazi, ni lazima tuyakusanye wakati wa mvua ya masika. Ni njia gani ambayo tungetumia kuhifadhi maji haya?

Maji yanayokusanywa kutoka kwa mapaa ya nyumba huwekwa kwenye mapipa. Mapipa yaweza kuwa ya mabati ama ya mawe. Kwa kawaida maji haya huwa ya matumizi ya nyumbani tu! Mifugo haitumii maji haya. Hii ni kwa sababu mahitaji ya mifugo ni makubwa kuliko ya wanadamu. Labda uwe na mapipa mengi ndipo uweze kuwapatia mifugo maji hayo.

Katika sehemu zilizo na ukavu wavu hutegemea maji ya visima kutosheleza mahitaji yao. Hata mifugo katika sehemu hizo, hutegemea maji ya visima. Vile vile kunazo sehemu nyingine ambako mipango ya kunyunyizia maji mashambani huendeshwa kwa kutumia maji ya visima. Mipango kama hii haiwezi kuendeshwa kwa njia kubwa.

Ni rahisi kukusanya maji ya mvua na kuyaweka kwa matumizi ya baadaye kwa kujenga mabwawa ya kuzuia maji kwenye mabonde. Mabwawa yenyewe yanaweza kujengwa wakati wa kiangazi. Baadaye wakati mvua itakaponyesha, maji yatajikusanya humo, maji haya yanaweza kutumika wakati wa ukavu.

Katika sehemu ambazo hazipati mvua ya kutosha, mabwawa ya namna hii ni muhimu sana. Maji haya yanaweza kutumiwa na binadamu ikiwa ni lazima ayatumie, itabidi ayachemshe na kuyaweka mahali safi.

MASWALI
1. Eleza njia tatu za kujipatia maji (al 6)

2. Maji huhitajika sana wakati gani wa mwaka (al 2)

3. Kwa nini maji yanafaa kuchemshwa kabla ya binadamu kuyanywa (al 2)

4. Eleza matumizi tofauti tofauti ya maji kama yalivyotokeza katika taarifa (al 6)

5. Ni paa lipi linalofaa zaidi kukusanyia maji? Toa sababu za kuchagua ulilolichagua na silo lingine (al 4)

6. Eleza kwa kifupi maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika taarifa (al 5)
i. Mifugo
ii. Kukusanya
iii. Kiangazi
iv. Masika
v. Kuhifadhi

7. Kamilisha methali zifuatazo zinazohusu maji (al 5)
i. Mkamia maji
ii. Mchimba kisima
iii. Maji yakimwagika
iv. Maji hufuata
v. Atanguliaye kisimani

SEHEMU YA PILI
MATUMIZI YA LUGHA
1. Nini maana ya maneno yafuatayo? (al 10)
a. Jina
b. Kitenzi
c. Kivumishi
d. Kielezi
e. Sentensi

2. Taja aina ya sentensi ujuazo huku ukitoa mfano (al 6)

3. Kwa kutumia viungo muhimu vya maneno, chambua maneno haya.
i. Alienda (al 4)
ii. Wamekichukua (al 5)

4. Andika sentensi zifuatazo kwa wingi (al 5)
i. Popo anaruka akitua mgombani
ii. Mti ule utakatwa
iii. Kisu kile kikali kimemkata
iv. Kikulacho ki nguoni mwako
v. Kunguru mwoga hufukuza mabawa yake.

5. Sentensi zifuatazo zina makosa. Yasahihishe (al 5)
i. Choo yao amechafuka
ii. Chanda mwema huvikwa pete.
iii. Nipeeko huyo chakula.
iv. Meno linalouma atang'olewa.
v. Tulisafiri na ngari.

6. Je, ni nani anayemsalimu mwingine "shikamoo" na atapewa jibu gani? (al 2)

7. Andika neno lingine lenye maana sawa na hilo ulilopewa (al 5)
i. Mwana
ii. Chelewa
iii. Uki
iv. Ishara
v. Hasira

8. Kuna tofauti gani kati ya maneno yafuatayo (al 4)
i. Chini/jini
ii. Pia/bia

9. Andika kinyume cha maneno haya (al 6)
i. Cheka
ii. Kunja
iii. Nadhifu
iv. Ezeka
v. Rafiki
vi. Chini

10. Eleza maana ya semi zifuatazo (al 5)

i. Kata tamaa
ii. Enda sare
iii. Arijojo
iv. Kufa ganzi
v. Mtu wa miraba minne

11. Toa maana mbili ya maneno uliyopewa (al 6)
i. Mbuzi
ii. Oza
iii. Vua

12. Kamilisha tashbihi zifuatazo (al 4)
i. Pendana kama...
ii. Mwepesi kama...
iii. Sauti kama...
iv. Baidika kama...

13. Kanusha sentensi zifuatazo katika wingi (al 4)
i. Mpwa wangu anasomea chuo kikuu
ii. Ukimuona ukimbie
iii. Tausi mzuri ana madaha mengi
iv. Nitakuja kwako.






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers