Kis 212: Ushairi Wa Kabla Ya Karne Ya 20 Question Paper
Kis 212: Ushairi Wa Kabla Ya Karne Ya 20
Course:Bachelor Of Education Arts
Institution: Maasai Mara University question papers
Exam Year:2017
CHUO KIKUU CHA MAASAI MARA
IDARA YA LUGHA,ISIMU NA UTAMADUNI
MTIHANI KWA WANAFUNZI WA MWAKA WA PILI, SHAHADA YA SANAA YA SEMESTA YA KWANZA (2016/2017)
KODI: KIS 212
MADA: USHAIRI WA KABLA YA KARNE YA 20
MAAGIZO
Jibu swali la kwanza na mengine mawili.
SWALI LA KWANZA
a) Huku ukitoa mifano fafanua istilahi zifuatazo(al. 8)
i) fasihi bulibuli
ii) sanaa sifika
iii) sanaa pendwa
iv) fasihi pendwa
b) Jadili sifa nne za maandishi ya kale. (al. 12)
c) Huku ukitoa mifano fafanua fani tano za matumizi ya lugha ambazo zinapatikana katika ushairi(al. 10)
SWALI LA PILI
Utenzi wa sifwa ya nguvumali ni miongoni mwa maandishi ya zamani ambayo yametumia wahusika katika kuendeleza mtiririko wa kisa kinachosimuliwa katika utenzi huu. Huku ukitoa mifano fafanua sifa za wahusika watano wanaopatikana katika utenzi huu. (al. 20)
SWALI LA TATU
Wataalamu wa fasihi wametoa maoni mbalimbali kuhusiana na chanzo cha ushairi wa kiswahili. Huku ukizingatia nadharia zinazofafanua chanzo cha ushairi, zihakiki huku ukibainisha udhaifu na nguvu zake(al. 20)
SWALI LA NNE
a) Tofautisha na kulinganisha mashairi ya kale na yale ya kisasa huku ukitoa mifano mahususi. (al. 16)
b) Kwa maoni yako, ni mashairi gani ambayo ni bora kuliko mengine? (al. 4)
SWALI LA TANO
Ujumbe unaojitokeza katika maandashi ya kale kwa kiwango kikubwa una lengo la kuboresha jamii. Huku ukito mifano kutokana na tenzi za kale ama ushairi wa kale wowote ule, tathmini kauli hii. (al. 20)
More Question Papers
Exams With Marking Schemes