Shule Ya Upili Ya Wasichana Elerai (Mck) Mtihani Wa Mwisho Wa Muhula Kiswahili Kidato I Mwaka 2012 Muhula I Question Paper
Shule Ya Upili Ya Wasichana Elerai (Mck) Mtihani Wa Mwisho Wa Muhula Kiswahili Kidato I Mwaka 2012 Muhula I
Course:Kiswahili
Institution: Form 1 question papers
Exam Year:2012
SHULE YA UPILI YA WASICHANA ELERAI (MCK)
MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA
KISWAHILI KIDATO I
MWAKA 2012 MUHULA I
SAA 1 ½
JINA …………………………………………………………………NAMBARI…………………….TAREHE………………..
Jibu maswali yote katika karatasi hii.
A.UFAHAMU
KITUO CHA UPIMAJI NA NASAHA (VCT)
Yapata mita mia mbili upande wa kushoto wa barabara inayotoka mjini Kibewte pana jengo kubwa la rangi ya hudhurungi , paa la vigae na madirisha makubewa ya vioo yenye mapazia ya nili yaliyorembwa maua mazuri. Jengo hili limepakana na kituo cha mafuta cha BP kwa upande wa kulia. Mkabala wa jengo lenyewe pana ujia mwembamba unaotumiwa na watembeaji wanaomiminika kama chungu kila uchao kuelekea mjini . Kwenye jengo hilo zuri na linalovutia macho ndipo kilipo kituo cha upimaji na Nasaha cha mji wa Kibwete.
Kwenye jengo lenyewe linavutia kwa rangi na sura yake pamoja na mandhari ya pale nje. Pana kitalu kizuri kilichopandwa maua ya kila aina kama asumini. Kitalu hicho kimezugushiwa uzio ili kuyakinga maua hayo mazuri. Ujia mdogo unaotoka barabarani kuelekea kituoni umesakifiwa vyema ; hauna vumbi na daima huwa safi. Jengo lenyewe lina bango kubwa lenye maandishi JISHINDE USHINDE VCT.
Kituo hicho kimegawika katika sehemu nne kuu. Kuna sehemu ya mapokezi ambayo ina makochi mazuri yaliyopangwa kwa nidhamu. Katikati ya makochi hayo yaliyofunikwa kwa bahameli ya buluu, pana kimeza kidogo cha duara. Juu ya kimeza hicho pana majarida na vijitabu vya kila aina vinavyohusu afya magonjwa na hata burudani. Sehemu ya pili inahusiana na Nasaha au ushauri.Hapa ndipo wanaposhauriwa na kupewa nasaha waliofika hapa kabla ya kupimwa kama wana virusi vya Ukimwi au la . Wahudumu waliopo hapa ni wapole na wana vipaji vya kuogea vizuri na watu wanaofika hapo.
Sehemu ya tatu ni chumba cha upimaji damu ambako ndiko shughuli ya kuchukua damu na kuipima inapotokea . Hapa pia hufanyiwa ushauri kwa kiasi Fulani . lengo kuu ni kuhakikisha kuwa anayetaka damu yake ipimwe amekata kauli kabisa . Sehemu ya mwisho ya kituo chenyewe ni mahali pa kuhifadhia vifaa mbalimbali vinavyotumiwa katika kituo kizima.
Wahudumu wa kituo hiki ni wapole na wana welewa mkubwa wa kazi yao. Wana uwezo mkubwa wa kufahamisha na kuwaelekeza watu wote wanaofika pale. Kwa kweli uzuri wa kituo hiki hauishii kwenye sura ya nje tu bali unaonekana pale ndani . Kituo hiki kinaonyesha uzuri wa ndani na nje sio ule wa mkakasi ndani kuwa kipande cha mti.
Maswali
a) Eleza sifa za jengo la mji wa kibwete la upimaji na nasaha .(al 4)
b).Fafanua sifa nne za mazingira yanayozunguka jengo la upimaji na Nasaha la mji wa
Kibwete(ala 4)
c) Jengo hili la mji wa Kibwete liligawika katika sehemu nne zitaje(al2)
d)Wana sifa gani wahudumu wa kituo hiki ?(al3)
e) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika habari uliyoisoma (al2)
i. Chungu
ii. Mandhri
iii. Welewa
iv. Kitalu
MATUMIZI YA LUGHA
1.Fupisha sentensi zifuatazo iwezekanavyo.
a) Baba yake mama alikutana na msichana mweupe pe!pe! pe! (ala 2)
b) Viti meza , kabati na dawati vyote vya thamani kubwa vilitapakaa uwanjani(al2)
c) Baba na mama yake mariamu wamewasili(2mks)
2. Onyesha shadda katika maneno haya (ala5)
a) Kibao
b) Kosa
c) Limau
d) Teta
e) Bikira
3 a) Orodhesha irabu zote za Kiswahili (ala5)
b) Orodhesha konsonanti zozote tano za Kiswahili (ala5)
4. Sauti zifuata hutamkiwa wapi ?
K ,
ng’
5. Taja irabu ya kati na mbele (ala1)
6.Taja sauti ziitwazo viyeyushho (ala2)
7 Tumia vitate vifuatavyo kuunda sentensi moja moja sahihi (ala 4)
i. Paa
ii. Baa
iii. Dada
iv. Tata
8 Unda sentensi moja moja ya neno moja kutoa dhana zifuatazo ?ala3)
i. Amri
ii. Kauli / taarifa
iii. Swali
9. Tumia kiunganishi mwafaka kuunganisha sentensi fupi fupi zifuatazo
Juma anavua sare yake.
Hamisi ataifua sare ya Juma .
Mama anapika chakula kitamu
Mtoto anamsumbua mama kwa kilio kisichokoma.
10. Fafnua maana ya misemo ifuatayo (ala5)
i. Chanda na pete
ii. Chana mbuga
iii. Mgomo baridi
iv. Weka uporo
v. Kazi ya kijungu jiko.
11 Andika wingi wa sentensi zifuatazo (ala10)
i. Jimbi limewika usiku kucha
ii. Mwanafunzi amesoma kwa bidii
iii. Kiwavi ameharibu mmmea kabisa
iv. Chura huimba wakati wa mvua
v. Kiokote huyu atasomeshwa na msamaria mwema.
12. Akifisha Sentensi zifuatazo ipasavyo:
i. juma atanunua vitu vifuatavyo mkate viazi mboga na majani chai (ala3)
ii. Kazi iliyo ngumu ni ni kufunza maths katika shule za upili(ala1)
iii. ngombe wote wanangangania nyasi kidogo kibandani (ala2)
FASIHI
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu masweali .
PENYE NIA PANA NJIA
1 kama uko safarini,chomboni umeingia,
bahari kuu kinani, mawimbi yakachachia,
Usikate tumaini, hapo ndipo penye ndia.
Penye nia ipo njia , usikate tumaini
2. Hapo hapo mawimbini, wewe hapo pigania,
Hapo ndipo milangoni, mawimbi yakuzuia
Mtima utie kani, bandarini utaingia
Penye nia ipo njia , usikate tumaini
Maswali
i. Mwandishi ametumia uhuru wa kishairi katika ubeti wa kwanza. Tambua uhuru
huo(al 1)
ii. Eleza umbo la shairi hili (ala5)
14 Tofautisha sifa za fasihi simulizi na zile za fasihi andishi (ala 10)
15.Ainisha aina za maneno katika sentensim zifuatazo
i. Mwambari na Juma watawasili kesho jioni(ala2)
ii. Pakia matomoko yote
16 Kanusha sentensi hizi (ala5)
a. Malimau yote yameiva
b. Joka lililouliwa liliwatisha wapiti njia
c. Tutaenda pamoja kuhudhuria mkutano
d. Mwanafunzi mtiifu husoma kila wakati
e. Mama amepika chakula kitamu
17 Andika sentensi hizi kwa umoja. (al6)
a) Vikombe vyenye nyufa vitatupya na wageni.
b) Vitumbua vyao vyote vimetiwa mchangani
c) Vilemba hivyo vimepeperushwa na upepo
18 Kamilisha methali ifuatayo
Sikio la kufa ….(ala 1)
MWISHO
More Question Papers
Exams With Marking Schemes