Midview High Schools Kiswahili Form 1 Term Iii 2017 Question Paper

Midview High Schools Kiswahili Form 1 Term Iii 2017 

Course:Kiswahili

Institution: Form 1 question papers

Exam Year:2017



Shule ya Upili ya Midview
Mtihani Wa mwanzo Wa muhula Wa tatu mwaka 2017.
Kiswahili
Kidato cha Kwanza.

1)Nyambua maneno haya
Kitenzi. Tendeana. Tendesha
Jenga
Fungua
Piga
Lima. (ala 4)
2)Tunga sentensi kuonyesha tofauti za maana za jozi zifuatazo za maneno;
a)Fua,via
b)Choka,shoka. (ala 2)
3)Andika maneno mawili yenye maana sawa na;
a)Rafiki
b)Shamba. (Ala 4)
4)Onyesha kielezi katika sentensi hizi;
a)Wanafunzi wote wako darasani.
b)Mchezaji Yule ameanguka kichalichali.
c)Mgeni huyo ana tambia mbaya sana.(ala 3)
5)Andika maana mbili za sentensi hii.
Waite wale. (ala 2)
6)Changanua mzizi,viambishi awali na tamati katika
a)Aliyeogeshwa
b)Ninapokea. (ala 3)

SEHEMU B.
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali.
Sheila:Niaje Saimo?Uko wapi?
Saimo:Tao.Subiri nine.I can see you.
Sheila:You are joking. Niko salon somewhere hidden.Saimo hunioni.Wewe ni liar.
Saimo:(Akicheka)Sawa switi.Ni salon gani basi?
Sheila:Tausi.Utanibaia nini?

Maswali.
1)Hii ni sajili gani? (ala 2)
2)Eleza sifa za sajili hii. (ala 4)
3)Andika kifungu hiki kwa lugha sanifu.(ala 4)

SEHEMU D.
FASIHI SIMULIZI
1)Methali ni nini? (ala 2)
2)Eleza umuhimu Wa methali katika jamii. (ala 10)
3)Taja methali zenye maana sawa na;
a)Samaki mkuje angali mbichi.
b)Cha kuvunda hakina ubani.
c)Polepole ndio mwendo. (ala 3)

SEHEMU D.
USHAIRI
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

Nina hiari kwa ari,kukariri,vizuri hiki shairi,
Niwatambue siri,nibashiri,haya dhahiri shahiri,
Subira yavuta hero,msubiri,niambe kwa umahiri,
Shairi la mashauri,nakariri,busara ni utajiri.

Tenda wema kwa hiari,na kwa ari,yote yatakuwa shwari,
Utakuwa mashuhuri,na hodari,tabasamu 'tashmiri',
Yalotendwa kwa hiari,hunawiri,had I mwisho wa dahari,
Shairi la mashauri,nakariri,busara ni utajiri.

Imani na desturi,ni hiari,iwapo 'tazihitari',
Iwe kutoa mahari,kutahiri,lakini ujihadhari,
Usiteme ya sukari,na mazuri,urambe yalo shubiri,
Shairi la mashauri,nakariri,busara ni utajiri.

Ninakupa mashauri,sighairi,siwe mwenye taksiri,
Matajiri mashuhuri,askari,na hata madaktari,
Majivuno huaziri,tahayuri,ndo malipo ya kiburi,
Shairi LA mashuhuri,nakariri, busara ni utajiri.

Kutoka alfajiri,adhuhuri,alasiri na nadhari,
Japo taweka nadhiri,tafakari,tafadhali tahhadhari,
Lazima uwe tayari,na ni heri,utimize kwa hiari,
Shairi la mashuhuri, nakariri, busara ni utajiri .

Maisha kama bahari,ni hatari,yabidi uwe jasiri,
Katu hakuna ya heri,yaso shari,kwa yote uwe tayari,
Hadhari yasikwadhiri,tahadhari,kabla ya athari,
Shairi la mashuhuri, nakariri, busara ni utajiri.

Nyenyekea kwa jabari,sighairi,hekima 'furike furi',
Siwe kama msafiri,ni kafiri,msimamo hadhihiri,
Leo hebu stakiri,tabasuri,sidharau mashauri,
Shairi la mashauri, nakariri, busara ni utajiri.

Maswali.
1)Lipe shairi hili anwani mwafaka.
(ala 1)
2)Hili shairi ni la aina gani?(ala 2)
3)Ni nini dhamira ya shairi?(ala 2)
4)Taja mashauri manne ambayo mshairi amedokeza katika shairi lake.(ala 4)
5)Kwa kutoa mifano taja mbinu mbili za lugha zinazojitokeza katika shairi hili.(ala 4)
6)Nakili mwandamizi Wa mleo katika ubeti Wa tank.(ala 1)
7)Thibitisha kwamba hili shairi ni la arudhi.(ala 4)






More Question Papers


Exams With Marking Schemes

Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers