Aks 303: Contemporay Kiswahili Novel And Play Question Paper
Aks 303: Contemporay Kiswahili Novel And Play
Course:Bachelor Of Education Arts
Institution: Kenyatta University question papers
Exam Year:2005
KENYATTA UNIVERSITY
SECOND SEMESTER EXAMINATION FOR THE DEGREE OF BACHELOR OF ARTS
AKS 303: CONTEMPORARY KISWAHILI NOVEL AND PLAY
Jibu swali moja kutoka kila sehemu
SEHEMU YA A
1. "Fasihi ni kioo cha jamii." Jadili kauli hii kwa kurejelea tamthilia moja na riwaya moja.
SEHEMU YA B
2. Jadili kwa tafsili umuhimu wa nchi ya Walenisi katika kuendeleza maudhui ya riwaya ya Walenisi (Katama Mkangi)
3. Huku ukirejelea matukio yoyote manne ya uhalisiajabu, fafanua nafasi ya Babu katika kufanikisha dhamira kuu ya mwandishi katika Babu Alipofufuka (S. A. Mohamed)
4. "Burhani (Mwisho ya Kosa) anaukwepa uhalisi na badala yake anayalazimisha mabadiliko katika wahusika wapotovu ili kukidhi mielekeo ya kidini." Jadili
SEHEMU YA C.
5. Jadili nafasi ya Mwelusi katika kuendeleza maudhui ya ukombozi katika tamthilia ya Kifo Kisimani (Kithaka Mberia).
6. Kwa kuwarejelea wahusika mbalimbali katika tamthilia ya Mama Ee (A. Mwachofi), tathmini maoni kwamba "hii ni dunia ya wanaume, dunia ya mawi".
More Question Papers
Exams With Marking Schemes
Popular Exams
Mid Term Exams
End Term 1 Exams
End Term 3 Exams
Opener Exams
Full Set Exams
Return to Question Papers