Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Kiswahili Darasa La Sita Question Paper
Kiswahili Darasa La Sita
Course:Primary Level
Institution: Kcpe question papers
Exam Year:2005
DARASA LA SITA MUHULA WA III - 2005
KISWAHILI
Jaza nafasi zilizoachwa wazi.
Endapo ni ukweli kwamba binadamu ya 1. ______ aliishi Afrika basi 2. ______ kudai kuwa 3. ______ ya mwanzo aliianza 4. ______ humu. Binadamu 5. ______ alihitaji kuwinda na 6. ______ chakula chake na kwa hivyo, 7. ______ avumbue vyombo 8. ______ kufanya hivyo. Bara la Afrika lilikuwa 9. ______ hatua kimaendeleo 10. ______ usuli wa Wazungu.
1.
A. Hawali
B. Wali
C. Awali
D. Mbeleni
2.
A. Tunaeza
B. Tunaweza
C. Tunawaza
D. Tunaaweza
3.
A. Teknologia
B. Technologia
C. Teknolojia
D. Tekmolojia
4.
A. Barabarani
B. Baharini
C. Baharani
D. Barani
5.
A. Huyo
B. Huyu
C. Huo
D. Hao
6.
A. Kukula
B. Kupiga
C. Kupika
D. Kupikia
7.
A. Ilimbidi
B. Ilibidi
C. Alibidi
D. Ilimbidi
8.
A. Vitavyomsaidia
B. Vinayomsaidia
C. Vitakavyomsaidia
D. Visaidia
9.
A. Likipiga
B. Vinapiga
C. Inapiga
D. Linapiga
10.
A. Kabla
B. Kabla ya
C. Baada
D. Baada ya
Jaza nafasi iliyoachwa wazi ukitumia jibu sahihi lililopo kwenye mabano.
11. Vitu vimekuwa ______ sokoni.
(kali, ghali, gali)
12. Wageni kwa hivi sasa wame ______
(asili, wasiri, wasili)
13. Watu huoga kisha ______
(hukula, hukulanga, hula)
14. Sijamtembelea kaka kwa siku ______
(mingi, nyingi)
Kamilisha methali zifuatazo
15. Mtegemea nundu haachi
A. Kunona
B. Kuona
C. Kula
D. Kufa
16. Nyani haoni
A. Mkiawe
B. Kundule
C. Domole
D. Dondale
17. Baniani mbaya kiatu chake
A. Kizuri
B. Kibaya
C. Dawa
D. Sumu
Matumizi ya -ingine
18. Gari ______ jeupe limewasili leo
A. Lingine
B. Zingine
C. Mwingine
D. Jingine
19. Nguo ______ zote ni chafu isipokuwa hii.
A. Zingine
B. Nyingine
C. Zote
D. Lingine
20. Chakula ______ kinapikwa na nyoko
A. Kingine
B. Chengine
C. Lingine
D. Pengine
Kinyume: chagua jibu lifaalo zaidi
21. Fumba ______
(Vumbua, fumbua)
22. Anika ______
(Anikisha, anua)
Chora maumbo yafuatayo
23. Duara
24. Pia
Tegua vitendawili vifuatavyo
25. Hiwali amekonda lakini hana mganga
(mikia ya panya, mijusi, sindano)
26. Hata zangu ameshindwa
(njaa, mauti, nyuki)
27. Funga mizigo twende Zaire
(mtama, merikebu, mkia ya mbwa)
Andika tarakimu zifuatazo kwa nambari.
28. Milioni moja
29. Milioni nne, mia nane elfu
30. Milioni sita, elfu sita tisini na tisa, mia tisa na tisa
Andika majina ya wadudu katika sentensi zifuatazo
31. Mimi nina miguu mingi, nina sumu. Mimi ni
(nyoka, viroboto, tandu)
32. Ninapenda sana kuishi kwenye vichunguu walivyovijenga wao ni
(kunguni, viroboto, mchwa)
33. Mimi ni ndege ninapenda giza na ninapopumzika kichwa changu huangalia chini. Mimi ni
(kinyonga, popo, bundi)
Chagua mojawapo ya maneno haya kukamilisha sentensi.
Mtoro, mdadisi, mkalimani.
34. Mtu anayetafsiri lugha kwa ya pili ______
35. Mtu anayeondoka mahali bila ruhusa ______
36. Mtu mwenye hamu ya kujua ______
Tumia neno linalofaa kukamilisha sentensi hizi.
37. Ukisafiri ______ ndege utafika salama
(pamoja, kwa, na)
38. Tulilala ______ yeye
(kwa, na, katika)
39. Tuliandamana ______ hadi nyumbani
(naye, wao, wote)
40. Katika karamu niliyoandaliwa tulikula chakula chote ______ kijiko
(na, mwiko, kwa)
Soma ufahamu huu kisha ujibu maswali.
Kobe alitamani kubadili maskani yake. Basi akamwomba tai amchukue mpaka kwenye mastakimu yake mpaya. Akaahidi kumpa ujira wake. Tai akakubali. Akamkamata Kobe gamba lake akapaa naye juu sana. Njiani wakakutana na Kunguru, akamwambia Tai, "Bwana wee huna habari, huyo Kobe anafaa sana kwa chakula, dhihaka mbali."
Tai akamjibu akamwambia, "Ndiyo bwana, lakini gamba lake ni gumu mno."
Kunguru akamwambia "Ah! Hilo si neno. Mwamba waweza kulipasua mara moja wala siyo kazi kubwa."
Basi akakata shauri la Kunguru akamwaga Kobe kwenye mwamba mkali. Ndipo wale ndege wawili wakafaidi chakula chao, yaani Kobe.
Maswali
41. Kobe alitamani
A. Kuhamia maskani mapya
B. Kuhama maskani mapya
C. Kuchukuliwa na tai
D. Kubadili mastakini mapya
42. Tai angelipwa ujira wake
A. Kabla hajamchukua kobe
B. Baada ya kumfikisha kobe katika maskani yake
C. Punde tu angekubali kumbeba kobe
D. Angemfikisha kobe salama katika makao mapya
43. Tai alikubali kuchukua kobe kwa sababu
A. Alitaka kumla
B. Aliahidiwa malipo
C. Akijua ni chakula kinachofaa
D. Alitaka kumbwaga penye mwamba
44. Kunguru na Tai
A. Wote ni ndege
B. Wanaishi pamoja
C. Ni ndege walao mizoga
D. Ni ndege wanaozaa watoto
45. Neno lenye maana sawa na maskani ni?
A. Kiota
B. Chengo
C. Pango
D. Msalani
46. Dhihaka ni sawa na?
A. Mzaha
B. Haraka
C. Wahaka
D. Uongo
47. Gamba kwa kobe ni sawa na ______ kwa mti
A. Ganda
B. Gome
C. Ngozi
D. Utando
48. "Ah!" ni tamko la kishangao kinachotumiwa
A. Kuonyesha furaha
B. Kushangilia
C. Kuonyesha tukio la kukera
D. Kuitikia jambo
49. Kunguru alimaanisha nini aliposema "Hilo si neno"
A. Kobe hana la kufanya
B. Kobe hana taabu
C. Gamba la kobe si gumu
D. Ugumu wa gamba la kobe hauwezi kuzuia kumla
50. Habari hii inatufunza kwamba
A. Kobe ni mnyama mjinga
B. Tai ni ndege mwenye nguvu
C. Kunguru ana akili kuliko tai
D. Usimwamini adui wa jadi hata kama ana dhiki.
More Question Papers