Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Chavakali Pre-Registration Examination. Question Paper

Chavakali Pre-Registration Examination. 

Course:Secondary Level

Institution: Kcse question papers

Exam Year:2008



Kiswahili Karatasi ya 102/1.

Maagizo:

Andika Insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima. Kisha chagua Insha moja kutoka hizo nne zilizobakia. Kila insha ina alama 20. Insha zako zisipungue maneno 400.


1. Wewe ni katibu katika mkutano uliofanyika wa Shirika la Maendeleo ya Wanawake. Ajenda za mkutano huu ni kama ifuatavyo:

i. Kufunguliwa kwa mkutano

ii. Kusoma na kudhibitisha kumbukumbu za mkutano uliotangulia

iii. Yatokanayo na kumbukumbu hizo

iv. Kujadili maendeleo ya miradi katika mwaka

v. Mikakai(mbinu) ya kutafuta fedha za kuendeshea shughuli za Shirika

vi. Njia za kuimarisha elimu ya mpango wa uzazi na malezi ya watoto

vii. Mengineyo

viii. Kufunga mkutano.

Andika kumbukumbu za mkutano huo.

2. Andika Insha itakayodhibitisha ukweli wa methali "Jitihada haiondoi kudura"

3. Vyombo vya habari vimekuwa kizuizi kikubwa kwa ujenzi wa jamii mpya baada ya ghasia za baada ya uchaguzi mkuu. Jadili

4. Wewe ni mwanachama wa kundi la Tafrija na Kwaya shuleni mwenu. Halmashauri ya shule imeandaa dhifa ya kuwazawadia wanakwaya hao. Umeulizwa na Mwalimu Mfadhili wa kundi hili kuandaa ratiba ya matukio yote ya siku hiyo.

Iandike ratiba hiyo.

5. Andika Insha itakayomalizika kwa...

ama kwa hakika yote niliyoshuhudia yalikuwa kama ndoto ambayo ningemlipa yeyote yule ili kuifanikisha. Hela hizo zote ningezitoa wapi mimi katika hiyo hali yangu?






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers