Edk 201: Kiswahili Poetry  Question Paper

Edk 201: Kiswahili Poetry  

Course:Bachelor Of Education (Arts)

Institution: Rongo University question papers

Exam Year:2017



Jibu swali la kwanza na mengine mawili

1.a.Fasili dhana ya ushairi huku ukirejelea wanampokeo na wanamapinduzi wowote wawili(6mks)

b.Fafanua mchango wa wakoloni waingereza katika ushairi wa kiswahili (12mks)

c.Huku ukitolea mifano ,eleza sifa zozote NNE za ushairi wa kiswahili (8mks)

d.Eleza changamoto zozote NNE zinaweza kumkumba mchanganuzi wa tenzi za kiswahili (4mks)

2.a.Riwaya na tamthlia ya kiswahili zimenufaika sana na taaluma ya ushairi.Jadili hoja hii kwa kutolea mifano ya kiswahili (8mks)

b.Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali

Siwati
Siwati nshishiyelo,siwati;kwani niwate?
Siwati ni lilo hill,'talishika kwa vyovyote
Siwati ni mimi nalo,hapano au popote
Hadi kaburini,mimi nalo tufukiwe


Siwati ngaadhibiwa,adhabu kila mifano
Siwati ningaambiwa,'tapewa kila kimono
Siwati lililo sawa ,silibanduliwa mkono
Hata nangaumwa na meno,mkono siubanduwi


Siwati si ushindani,mukasema nashindana
Siwati ifahamu,sibabuye waungwana
Siwati ndangu imani,niithaminiyo sana
Na kuwaita naona,itakuwa ni muhali


Siwati nimeradhiwa,kufikwa na kila mawi
Siwati ningaambiwa,niaminiyo na hayawi
Siwati kisha nikawa ,kama nzi ;hivyo siwi
Thamma nakiri siwi,na Mn'gu nisaidiya
(Abdalla Abdilatif ,sauti ya dhiki,1973)


Changanua matumizi ya lugha katika shairi hili(8mks)
Eleza Uhuru aliotumia mshairi katka shairi hili(4mks)

3.Onyesha tofauti na mfanano uliopo kati ya utenzi wa Liyongo na Takhmisa ya Liyongo(20mks)


4.Kwa kutolea mifano mwafaka,onyesha namna ambavyo ushairi wa kiswahili umekuwa ukibadilika kiumbo tangu jadi hadi leo(20mks)


5.a.Huku ukitolea mifano mwafaka,jadili maudhui yoyote matatu ya mashairi katika diwani ya Bara Jingine ya Kithaka wa Mberia(10mks)

b.Fafanua aina zozote tano za bahari ya kimapokeo(10mks)






More Question Papers


Exams With Marking Schemes

Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers