Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

National Mock / Post Mock Kiswahili Fasihi Question Paper

National Mock / Post Mock Kiswahili Fasihi 

Course:Secondary Level

Institution: Kcse question papers

Exam Year:2010



SEHEMU YA A: – TAMTHILIA
AMEZIDI: Said Ahmed Mohamed
1. “Wewe kula tu na kulala Ah! Hata Mungu alifanya kazi siku saba na akapumzika…”
a) Nani alitamka maneno hayo? (alama 1)
b) Kwa nini ikambidi kusema hayo? (alama 3)
c) Kwa kutumia mifano yoyote miwili, onyesha vile swala la majaliwa linavyojitokeza katika tamthilia hii.
(alama 4)
d) Taja na ufafanue shida zozote nne zinazokabili bara la Afrika kama inavyosawiriwa na mwandishi wa Amezidi.
(alama 12)
2. a) Kwa kuzingatia mazingara ya darasa kama inavyomulikwa na mwandishi, dondoa na ufafanue dosari zozote nne ambazo zinachangia elimu duni barani. (alama 12)
b) Ulaghai kwa umma na ukosefu wa uwajibikaji umechangia kwa kiwango kikubwa uzoroteshaji wa chumi za nchi mbali mbali barani. Kwa kurejelea wahusika wowote wanne, tetea ukweli wa kauli hii. (alama 8)

K. Ongeti : VISIKI
3. a) Uhusiano wa Matanga na Huzuni si wa dhati . Ni nini hasa kinachosababisha hali hii? (alama 6)
b) Unafikiri Mwalimu ana dhima gani katika tamthilia hii? (alama 4)
c) Mwandishi wa tamthilia hii amejitokezaje katika utumiaji wa lugha ili kudhihirisha ukomavu wake katika utanzu huu? (alama 10)
4. Wanapohitaji kura, wao hutuahidi mashamba makubwa. Lakini wapi? Wapi? Nani akupe shamba?
a) Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
b) Mgogoro juu ya mashamba ni kati ya nani kulingana na dondoo hili? Mgogoro wenyewe ni juu ya nini hasa?
(alama 7)
c) Anwani VISIKI inaweza kufasiriwa kwa njia nyingi kutegemea muktadha na mhusika. Pambanua maana zozote tatu zinazoweza kupatikana kutoka kitabuni. (alama 6)
d) Askari wanaendelezaje ukatili katika tamthilia hii? (alama 3)



5. SEHEMU C USHAIRI
1. Siku moja itafika, nijifungie safari;
Safari ndefu hakika, isiyotaka magari;
Magari hayatafika, wala meli za fahari;
Siku yangu!
2. Siyo nadhiri naweka, katu siyo ubashiri;
Ni mwendo uliopangika, ni muhali kughairi;
Kwenda nawajibika, kubeta sina hiari;
Siku yangu!
3. Roho inanitutika, kila nikitafakari;
Ziara is’o shirika, hata akhi hujibari;
Wanabaki kuteseka, na kunipami kwaheri;
Siku yangu!
4. Siku itakapofika, zamani za kuabiri;
Kutazuka hekaheka, kibuhuti cha Suduri;
Na mwingi mno wahaka, kwa wendani na wambari;
Siku yangu!
5. Ziara itafanyika, na mola ndiye Sayari;
Ngia itanimulika, nifike pasi usiri;
Niwache mkitamka, mabayangu na mazuri;
Siku yangu!
6. Binadamu hutoweka, siku yake ikijiri;
Ugeni una mipaka, nami leo nahajiri;
Mipaka yangu yafika, mungu amenihitaji;
Siku yangu!
7. Sina budi kuitika, wito huu wa kahari;
Ziara kukamilika, moyoni sifanyi ari;
Nenda zangu haraka, moyoni sifanyi ari;
Siku yangu!
8. Haki sasa naondoka, ni mja sina hiari;
Huko nitasetirika, dahari hata dahari;
Buriani wahibaki, na maswahaba kwaheri;
Siku yangu!
Maswali:
a) Mtunzi wa shairi alikuwa na dhamira gani katika kutunga shairi hili? (alama 3)
b) Idhini ya ushairi/ mtunzi inajitokezaje katika shairi hili? (alama 4)
c) Kwa kutumia ithibati kemkem (kutoka katika shairi hili), eleza kwa undani muundo wa shairi hili. (alama 4)
d) Eleza ujumbe unaotolewa na mwandishi katika ubeti wa saba na nane. (alama 4)
e) Mafungu yafuatayo yametumiwa kumaanisha nini?
i) ni muhali kughairi. (alama 1)
ii) ziara is’o shirika. (alama 1)
f) Toa mifano miwili ya jazanda katika utunzi huu. (alama 3)

6. Mtu na awe na macho, kamili yote mawili,
Na kila kitu ambacho, alikiumba Jalali,
Kama hana kichwa kwacho, si mtu bali tumbili,
Kichwa ni yeye wakili, wa kila kitu mwilini.
Wa kila kitu mwilini, ni yeye huwa wakili,
Na yeye ndiye mashini, ya kuendesha kauli’
Kito cha matumaini, usukani wa akili,
Kichwa ni yeye wakili, wa kila kitu mwilini.
Wakili wa kila kitu, viungo vyote vya mwili,
Kichwa kinaleta utu, kwa sifa ya taamuli,
Ama ufanywe utu, kwa sifa ya taamuli,
Kichwa ni yeye wakili, wa kila kitu mwilini.
Mtu huwa ni sanamu, hajaumbika kamili,
Kama hanayo fahamu, fahamu yake thakili,
Si kichwa cha binadamu, binadamu wa asili,
Kichwa ni yeye wakili, wa kila kitu mwilini.
Tazama mwendawazimu, kichwa kilotanakali,
Huingiwa na zahamu, kukiuka ya awali,
Mfano wa marehemu, kila kiungo hajali,
Kichwa ni yeye wakili, wa kila kitu mwilini.
Kichwa chenyewe si hoja, hoja ubongo mkali,
Kiwe kijua vioja, kwa kamili atikali,
Si kichwa chenye kuvuja, si kichwa chenye manzili,
Kichwa ni yeye wakali, wa kila kitu mwilini.
Kichwa kiwe peke, juu ya kiwiliwili,
Shingoni ukitungike, na nywele kama ulimi,
Moyo visiunganike, kichwa hakitahimili,
Kichwa ni yeye wakili, wa kila kitu mwilini.

Maswali:
a) Fafanua ujumbe unaobebwa na kiitikio cha utungo huu. (alama 3)
b) Andika ubeti wa sita katika lugha nathari. (alama 4)
c) Mja asiye na ‘kichwa’ amefananishwa na nini? Toa mifano miwili. (alama 2)
d) Ingawa kichwa ni muhimu, ni sharti kishirikishwe na viungo vipi ili kipate ukamilifu wake? (alama 3)
e) Shairi hili ni la bahari gani? Toa sababu. (alama 2)
f) Eleza mpangilio wa vina katika ubeti wa pili. (alama 2)
g) Taja na ueleze maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi.
i) Neno la mwisho katika utao wa mleo ubeti wa kwanza. (alama 2)
ii) Neno la mwisho katika ukwapi wa mwanzo ubeti wa tano. (alama 2)






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers