Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kis 200: Theory And Analysis Of Kiswahili Literature Question Paper

Kis 200: Theory And Analysis Of Kiswahili Literature 

Course:Bachelor Of Education Arts

Institution: Masinde Muliro University Of Science And Technology question papers

Exam Year:2008



Page 1 of 3

MASINDE MULIRO UNIVERSITY OF SCIENCE AND TECHNOLOGY(MMUST)
UNIVERSITY EXAMINATIONS
2008/2009 ACADEMIC YEAR
SECOND YEAR FIRST SEMESTER EXAMINATIONS
FOR THE DEGREE OF BACHELOR OF EDUCATION (ARTS)
COURSE CODE: KIS 200
COURSE TITLE: THEORY AND ANALYSIS OF KISWAHILI LITERATURE

DATE: 2nd December 2008 TIME: 8.00 a.m. –11.00 a.m.

MAAGIZO
Jibu mswali manne. Maswali mawili kutoka kila sehemu. Kila swali lina alama 17 ½ .

Page 2 of 3

SEHEMU YA ‘A’

1. Kwa kutumia mifano eleza maana ua istilahi zifuatazo katika kazi ya fasihi.
a) Kupiga chuku
b) Uhuishi
c) Ufaraguzi
d) Taharuki

2. Kwa kutolea mifano madhubuti jadili vigezo vyovyote vitano vya kuhakiki kazi
ya fasihi kama anavyopendekeza K. W. Wamitila (2002).

3. Chagua nadharia yoyote moja kati yaa zifuatazo na ueleze jinsi unavyoweza
kuitumia katika kuhakikiwa kazi ya fasihi.
a) Udhanaishi
b) Unisai/umenke

SEHEMU YA ‘B’
4. Jadili maudhui yoyote matano yanayojitokeza katika mojawapo (wa) ya? Vitabu
vifautavyo.
a) Kitumbua kimeingia mchanga
b) Asali chungu
c) Amezidi
d) Vipuli vya figo
e) Ndimi za mauti katika Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine.

5. Kwa kutumia hoja zozote jadili jinsi dhima ya mandhari inavyojitokeza katika
mojawapo wa vitabu vifuatavyo.
a) Utubora Mkulima
b) Kiu
c) Kisima Cha Gining
d) Siku Njema

6. Jadili hulka za wahusika wowote watano (5) katika mojawapo wa vitabu
vifuatavyo.
a) Mke Mwenza
b) Kifo Kisimani
c) “Siku ya Mganga’ katika Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi nyingine.

7. Chambua shairi lifuatalo kwa kuzingatia maudhui na fani kisha uandike ubeti
wa mwisho katika lugha natharia.

Page 3 of 3

1
No inuka inuka hima twaa kalamu
Ya ‘ndika kwa khati njema hino nudhumu
Omeka wenye kusoma waifahamu
Apate yashika na kuyapima yaliyo humu

2
Kuandika anza anza ‘sikawe mkono wangu
Na mimi naanza kisa chenyewe cha mlimwengu
Alivyonifanza nao wajuwe waja wenangu
Wapate jitunza salama wawe hawa ndu zangu

3
Mja sikudhani sikudhainiya ‘tanizunguka
Nikamuamini hafikiriya hatageuka
Kumbe mwafulani hakuzoweya kuaminika
N’shambaini ingawa baya lishanifika

4
Menitenda kisa kisa adhimu mja mcheni
‘Mezinduka sasa n’shafahamu najuwa kwani
Ni yangu makosa najilaumu kumuamini
Sikuwa napasa hata sehemu kumthamini

5
‘Meniuwa mja mja ni nduli tahadharini
Mjaye daraja nda kikatili hana imani
Muonapo mja kaani mbali mujitengeni
Asije akaja (kwani habali) kuhasirini

6
Mja hana haya haya hazimo mwake usoni
Mja ni mbaya hutimba shimo uingiye ndani
Na ukisha ngiya azome zomo furaha gani!
Mmoja kwa miya ndiye hayumo baya kundini






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers