Form 4 Kiswahili: Kis 102/3 Question Paper
Form 4 Kiswahili: Kis 102/3
Course:Kiswahili
Institution: Form 4 question papers
Exam Year:2021
SEHEMU YA A:TAMTHLIA
P.Kea:Kigogo
1.LAZIMA
"Unalidharau gogo lililokuvusha moto,Soo?"
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (al.4)
b) (i) Bainisha tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili. (al.2)
(ii)kwa kurejelea tamthilia nzima,toa mifano mingine saba ya matumizi ya tamathali ya usemi iliyotajwa hapo juu.
c) Eleza umuhimu wa msemaji maneno haya katika kuijenga tamthilia ya kigogo (al.7)
SEHEMU YA B: HADITHI FUPI
A.CHOKOCHO NA D.KAYANDA :Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
Jibu swali la 2 au la 3
2. Alifa Chokocho: Masharti ya kisasa
"Ila tu ,zaidi ya hayo, nataka ujue ya kwamba mimi ni mwanamke wa kisasa..."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
b) kwa kutoa hoja nane kutoka kwenye hadithi , thibitisha kuwa msemaji ni mwanamke wa kisasa. (al. 8)
c) Eleza umuhimu wa anayeambiwa maneno haya katika kuijenga hadithi. (al.8)
AU
3. Ali Abdulla: Ndoto ya Mashaka
a) Soma kifungu kifuatacho Kisha ujibu maswali:
Chumba chetu ni Cha kupanga. Kiko ndani ya nyumba moja iliyoko Tandale...eneo la uswahilini. Ni malazi ya umati mkubwa wa pangu pakavu,akina sisi wasakatonge. Ujenzi wake ni ule usio na mpangilio maalum. Chumba chetu,kwa mfano kimekumbatiana na choo Cha jirani. Harufu yote itapikwayo na domo la choo hicho huhamia chumbami mwetu. Choo chenyewe kimeinuka juu kama ghorofa! Ndiyo vyoo vyetu. Ubavu mmoja wa chumba chetu unaoga maji ya mfereji wa China,kama unavyoitwa. Mfereji huo ni wa maji
machafu. Nao hutema uchafu wake katika mto Msimbazi. Yote hayo ni tisa ,kumi ni mvua zinaponyesha. Hiyo ni fursa kubwa kwani wakazi wa Tandale hupatiza kutapisha vyoo vyao. Mbali na kubeba uchafu wa Kila aina,mfereji huo huongezwa mzigo wa matapishi ya vyoo. Hapo tena apewaye ndiye aongezwaye. Nisikilize uvundo huo. Hata mzoga uko nyuma! Sisi huomba dua lakini mfereji china usifurike. Kipindi hicho kwetu huwa Cha maafa makubwa. Kuna majira na nyakati ambazo sisi huchagua kutumia choo za karatasi au choo fataki tupendavyo kukiita. Haja zetu zote ; kubwa na ndogo ,kwa watoto wetu na sisi watu wakubwa huzifanya ndani ya karatasi za plastiki. Na muda si muda kwenye giza na ukungu utasikia pruuuu...pwaa! Mtu katupa fataki yake nje. Ole wako ukipatikana nayo usoni. Na mvua nazo zinazozidisha mafuriko. Ndipo utakaposikiavsauti za vigogo zikitangaza kuwa watu wa mabondeni wahame. Waende wapi? Hawasemi lakini!
i) Bainisha aina za taswira ambazo zimetumika katika kifungu hiki. (al.3)
ii) chambua vipengele vingine nane vya kimtindo vilivyotumika katika kifungu.(al.8)
S. Omar:Shibe Inatumaliza
b)"Tunakula tu. Vyetu na vya wenzetu...Na watakaozaliwa miaka hamsini ijayo."
i) Eleza muktadha wa dondoo hili.(al.4)
ii) Thibitisha ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari kwa kutoa hoja tano.(al.5)
SEHEMU YA C: RIWAYA
Assumpta K. Matei: Chozi la Heri
Jibu swali la 4 au la 5
4.(a)Kwa kurejelea wimbo wa shamsi akitoka ulevini,jadili uhimu wake katika kujenga maudhui ya riwaya.(al.10)
b) Jadili mifano kumi ya changamoto wanazopitia wahafidhina kwa kurejelea mazungumzo Kati ya Ridhaa na Tila.
Au
5.(a)"...Wewe hujui kwamba umaskini unaweza kuupujua utu wa mtu,akatenda hata asiyoyakusudia kutenda?"
i) Eleza muktadha wa dondoo hili.(al.4)
ii) Kwa kurejelea wahusika sita kwenye riwaya,dhihirisha ukweli wa kauli hii.(al.6)
b)"Huyu ambaye mama alimwona kuwa gae,kumbe Sasa ndiye chombo cha kunivusha bahari hii ya dhiki?"
i) Eleza muktadha wa dondoo hili.(al.4)
ii) Bainisha tamathali moja ya usemi ambayo imetumiwa katika dondoo hili.(al.1)
iii) Tathmini umuhimu wa msemaji katika kuijenga riwaya.(al.5)
SEHEMU YA D: USHAIRI
Jibu swali la 6 au la 7
6. Soma shairi lifuatalo Kisha ujibu maswali.
Wanaume,nauiliza mwafanyani?
Paka shume,jigeuza ni kwa nini?
Mungurume,chezacheza majiani
Kwa nini?
Utamwona,mwanamume kashaini
Anang'ona, na selume chochoroni
Ndio Lana ajipime japatani?
Kwa nini?
Japo yeye,ana wake sheriani
Ni ladhaye,amshike wa fulani
Shukuruye,ni mateke kwa wandani
Kwa nini?
Mke wake,atamwacha singizini
Atoroke,parakacha migombani
Kumbe kake,anakocha kwa jirani
Kwa nini?
Kutwa kazi,pesa yake huioni
Kijakazi, atamke tukalani?
Kate ndizi,changa kwake itojani?
Kwa nini?
Mume pesa,cumhumbageni
Azitesa,toto zake firauni
Apepesa,mwendo wake ulevini
Kwa nini?
Bwana miye,nakuona tafrani
Nimezeye,huku ninaishi ndani
Bora miye,kutengana nawe jini
Kwa nini?
Kanzu moja,myaka saba nivaeni?
Si viroja,tajaiba hadharani
Ngojangoja,mi sihaba mejihini
Kwa nini?
Nimepata, habarizo kwa fulani
Kuwa hata,kwa jamazo honekani
Hata mbata,kwa nduguzo patikani
Kwa nini?
Hutosheki,asilani abadani
Pesa laki, wafujani mfukoni?
Tahamaki, mikononi huzioni
Kwa nini?
Nacha sema,nenda zangu mabondeni
Fanya mema,mlimwengu duniani
Sijasema,mke wangu nakosani?
Kwa nini?
Maswali
a) Fafanua mambo sita wanayoyafanya wanaume na kusababisha nafsineni alalamike.(al.6)
b) Huku ukitoa mifano,bainisha aina mbili za uhuru alizotumia mshairi.(al.2)
c) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo: (al.3)
i)Idadi ya vipande katika mishororo
ii) Idadi ya mizani katika mishororo
iii) Mpangilio wa vina katika beti
d) Andika ubeti wa sita kwa lugha ya nathari.(al.4)
e) Bainisha nafsi neni katika shairi hili.(al.2)
f) Andika aina mbili za urudiaji zilizotumiwa katika shairi.(al.2)
g) Eleza maana ya msamiati ufuatao kulingana na shairi.(al.1)
Viroja-
7.Soma shairi lifuatalo Kisha ujibu maswali.
Muhibu wangu muhibu,nakwita niitikiya
Nakwita ndoo karibu,upate kunisikiya
Nakuuliza nijibu,sinifite hata moya
Usinifite nambiya,lilokuudhi ni lipi?
Lililo langu ni lako,na lako ni langu piya
Liloudhi moyo wako,si vibaya kunambiya
Sifundike maudhiko,mwenzangu utaumiya
Usinifite nambiya,lilokuudhi ni lipi?
Jambo lisokupendeza,iwapomekufanyia
Ni vyema kuniongeza,kajuwa ya sawa ndiya
Kuliko kulinyamaza,na kunikasirikiya
Usinifite nambiya,lilokuudhi ni lipi?
Nambiya nipate juwa,nambiya Sasa nambiya
Wasiwasi umekuwa,ni mwingi uloninginya
Juwa utanitunguwa,ndilo ulokisudiya?
Usinifite nambiya,lilokuudhi ni lipi?
Iliyo sababu yangu,hata hauliza haya
Ni kwamba baruwa zangu,mbili nilokuleteya
Hujazijibu mwenzangu,mno umelimatiya
Usinifite nambiya,lilokuudhi ni lipi?
Kila siku ikipita,huwa nikitarajiya
Baruwa yako kupata,nijuwe yako afiya
Lakini sishi kudata,huwa karibu kuliya
Usinifite nambiya,lilokuudhi ni lipi?
Mawazo Kila namna,moyoni yanipitiya
Hata Sasa nna dhana,juu yako afiya
Labda waumwa Sana,kunijuza wacheleya
Usinifite nambiya,lilokuudhi ni lipi?
Ituze yangu nafusi,kwa baruwa kuneteya
Nileteya kwa upesi,sizidi kulimatiya
Unitowe wasiwasi,moyoni uloninginya
Usinifite nambiya,lilokuudhi ni lipi?
Maswali
a) Lipe shairi hili anwani mwafaka.(al.1)
b) Eleza umbo la shairi.(al.4)
c) Bainisha nafsi neni katika shairi.(al.2)
d) Andika aina nne za uhuru wa kishairi zilizotumiwa katika shairi hili.(al.4)
e) Bainisha mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi.(al.2)
f) Andika ubeti wa sita kwa lugha ya tutumbi.(al.4)
g) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo.(al.3)
i)Idadi ya vipande katika mishororo
ii) Mpangilio wa vina katika beti
h) Bainisha toni ya shairi hili.(al.1)
SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI
8.(a) (Akizungumza,Kila mtu hubabaika)
i) Tambua kipera hiki.(al.1)
ii)Umepewa jukumu la kuwasilisha kipera hiki kwa hadhira ya watoto. Eleza mtindo utakaoutukia.(al.4)
iii) Bainisha kipengele Cha kimtindo kilichotumika katika kipera hiki.(al.2)
b)(i) Eleza maana ya vitanza ndimi.(al.2)
ii)vitanza ndimi vina dhima gani katika jamii?(al.5)
iii)Umeamua kutumia mbinu ya kushiriki katika ukusanyaji wa data kuhusu vitanza ndimi . Eleza manufaa ya kuitumia mbinu hii.(al.6)
More Question Papers
Exams With Marking Schemes