Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Kansbag Kiswahili Karatasi Fasihi Question Paper

Kansbag Kiswahili Karatasi Fasihi 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2009



102/3
KISWAHILI
KARATASI 3
(FASIHI)
SAA 2½







KANSBAG PROJECTIONS FORM FOUR TERM 1 EXAMINATION 2009
Kenya Certificate of Secondary Education
KISWAHILI
KARATASI 3
SAA 2½








MAAGIZO
- Jibu maswali manne pekee
- Swali la kwanza ni lazima
- Maswali hayo mengine matatu yanachaguliwa kutoka sehemu nne zilizobaki yaani riwaya, tamthilia mayai waziri wa maradhi na fasihi simulizi
- Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja


1) SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI YAFUATAYO
1) Sitokuwanayo,dawamu daima,
Dhiki nilonayo,iliyon’egema,
Ta’wa mbali nayo,utuwe mtima.

2) utuwe mtima,na kutabaridi,
‘papatuwe kama,uwa la waridi,
Zitakapokoma,zakwe tashdidi.

3) zakwe tashdidi,zinganilemeya,
nitajitahidi,kuzifumiliya,
nipate muradi,ninaongojeya.

4) ninaongojeya, pasi ati ati,
kwa moyo mmoya,tama sikati,
ungalimatiya,si kwamba sipati

5) si kwamba sipati,kwa kukawa kija,
hatuwa siruti,mudawe nangoja,
saa hainipiti,talivaa koja.

6) Talivaa koja,la yangu subira,
Nitate natija, ilo barabara,
Subira kwa mja,ndilo jambo bora.

7) Ndilo jambo bora, litakikanalo,
Hili kila mara,mtu awe nalo,
Makubwa madhara, kutokuwa.

MASWALI
1.
a) Eleza ujmbe unaojiotokeza katika shairi hili 2mk
b) Taja majina ya mishororo ya shairi hili 3mk
c) Eleza muundo wa shairi hili 5mk
d) Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari 3mk
e) Eleza jinsi mwandishi ametumia uhuru wake katika shauri hili kwa kutoa mifano mitatu 3mk
f) Eleza maana ya maneno haya kulingana na shairi;- 3mk
i. mtima
ii. dhiki
iii. madhara
g) Taja tashbihi moja iliyotumika katika shairihili 1mk




2) TAMTHLIA
KITHAKA WA MBERIA: KIFO KISIMANI
SWALI LA 2 AU LA 3
2. Hotuba yote hii ni ya nini? Inatupeleka wapi?niambie (kimya kifupi) usiniangalie kama kwamba mimi ni chui mwenye pembe!
i. Eleza muktadha wa dondoo hili 4mk
ii. Andika mbinu mbili za uandishi zinazojitokeza katika dondoo hili 2mk
iii. Eleza sifa za anayeulizwa maswali katika dondoo hili 6mk
iv. Eleza mambo yaliyosababisha kuanguka kwa utawala wa mtemi bokono 8mk

3. Kwa kutolea mifano onyesha namna mwandishi wa tamthlia ya kifo kisimani amefaulu katika matumizi ya mbinu ya kinaya 20mk

3) RIWAYA
SAID A MOHAMMED:-UTENGANO
4. Akacharaza vile ugomvi ulivyotokea ,atialinijia mimi. Arererere arererere,arererere –sijui wewe.
a) yaweke maneno haya katika muktadha wake 4mk
b) yaelekea msomaji alikuwa na chuki na kusudio la kulipiza kisasi. Eleza namna wahusika mbalimbali walionyesha chuki kufikia kiwango cha kulipiza kisasi 16mk

4) HADITHI FUPI
5. K.W. Wamitila- Mayai Waziri wa Maradhi na hadithi nyingine.
Eleza namna unyanyasaji wa mwanamke umejitokeza katika hadithi zifuatazo
a) Uteuzi wa moyoni 10mk
b) Kachukua hatua nyingine 10mk

5) FASIHI SIMULIZI
6.
i. Eleza sifa za ngano za mazimwi 5mk
ii. Eleza mbinu zozote tano anazoweza kutumia mtambaji wa hadithi ili iwe yenye mnato kwa hadhira yake 10mk
iii. Eleza tofauti tano kati ya hekaya na hurata 5mk






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers