Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Kiwahili Paper 3 Mock Embu District Question Paper
Kiwahili Paper 3 Mock Embu District
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2006
WILAYA YA EMBU- MTIHANI WA MWIGO
Hati ya kuhitimu elimu ya sekondari
Kiswahili
Karatasi 102/3
Julai/ Agosti 2006
FASIHI SIMULIZI
1. Soma utungo ufuatao kasha ujibu maswali.
Lala mlezi wa mwana (*2)
Mama yako
Ameenda mtoni
Lala, lala, mlezi wa mwana (*2)
Akipata nyama
“mlezi unaweza kwenda nyumbani”
Akipata mboga
“mlezi unaweza kuja kula”
Kiazi cha motto kimekwisha kabisa
Uji wa motto
Umekwisha kabisa
Umekwisha kabisa
Umekwisha kabisa
a) I) huu ni wimbo wa aina gani? Alama 1
II) toa sababu za jibu lako. Alama 2
b) Taja mbinu moja ya lugha iliyotumiwa katika utungo huu na utoe mfano. Alama 2
c) Eleza uhusiano kati ya mama motto na mlezi wa motto. Toa sababu. Alama 4
d) Taja aina nyingine nne za nyimbo katika fasihi simulizi. Alama 4
e) Taja shughuli za akina mama kulingana na wimbo huu. Alama 3
TAMTHILIA
KIFO KISIMANI: KITHAKA WA MBERIA
2. Kichwani umetawaliwa na neon moja tu. Uchunguzi! Usaliti wako wako umetosha na unachosha. Mlango ndio ule! Toka Butangi haihitaji tena tena mashauri yako. Nenda ukajishauri mwenyewe.
a) Eleza muktadha wa maneno haya. Alama 4
b) Kwa nini uchunguzi unahitajika. Alama 4
c) Eleza tabia za msemaji. Alama 6
d) Eleza athari zake kwa Butangi. Alama 6
3. a) Eleza juhudi zinazofanywa ili kuikomboa Butangi. Alama 10
b) Ni mambo gani yalikwaza juhudi za ukombozi. Alama 10
RIWAYA
MWISHO WA KOSA: Z BURHANI
4. Sina muda mwingi. Karibu ghasia zitanza na kwa hivyo nitakueleza hadithi yangu kwa ufupi tu.”
a) Eleza muktadha wa maneno haya. Alama 4
b) Ghasia zinazorejelewa hapa ni zipi? Alama 2
c) Msemaji wa maneno haya alikuwa amefikwa na jambo lipi? Alama 4
d) Eleza hadithi inayorejelewa hapa.
5. Z. Burhani ameangazia uozo/ uovu wa kijamii katika riwaya ya mwisho wa kosa. Jadili alama 20
HADITHI FUPI
6. Mayai waziri wa maradhi na hadithi nyingine: K.W. Wamitila ( mhariri)
“nyumbani chakula cha mchana hakikulika vizuri. Alikula kidogo tu akaenda zake kulala. Akiwa kitandani ndoto za mchana zilianza kumsumbua. Katika ndoto ya kwanza aliota yeye na mawaziri wengine pamoja na wabunge kadhaa wakiwa ndani ya baa wakinywa pombe. Chupa zilikuwa zimejaa mezani na kesi nyingine nyingi zilikuwa zimepangwa pembeni zikiwasubiri. Nyama za kuku na mbuzi zilikuwa nyingi.”
a) Ni mambo gani yaliyokuwa yametendeka kabla ya ndoto hii? Alama 10
b) Eleza tabia za Mayai Waziri wa Maradhi kama zinavyojitokeza katika ndoti hii. Alama 4
c) Taja ndoto zingine mbili alizoziota Bwana Mayai. Alama 2
d) Mayai Waziri alikuwa amefanya kazi nyingi baada ya kumaliza masomo yake. Zitaje kazi hizo. Alama 4
USHAIRI
7. Soma shairi lifuatalo kasha ujibu maswali.
Wangu niliyekupenda, leo nitakufukuza
Kuishi umenishinda, waniletea mayaza
Ola vile nimekonda, jasadi nimepooza
Uwache kuniumiza, ni heri mwana kunenda
Ulikuwa wangu nyonda, huba nikaikoleza
Kukupenda kama tunda, embe lenye uliwaza
Ukajigeuza punda, eke umenicharaza
Uwache kuniumiza, ni heri mwana kunenda
Nimekonda kama ng’onda, mwandani wanilemaza
Sautiyo ya kinanda, sitaki kusikiliza
Sikutaki bora kwenda, muhibu wanishangaza
Uwache kuniumiza, ni heri mwana kunenda
Kinyume ulipokwenda, nilidhani kuteleza
Na wewe hukujilinda, nyendo mbaya kupunguza
Cha kuvunda kishavunda, hata ukikifukiza
Uwache kuniumiza, ni heri mwana kunenda
Mja wewe wanishinda, kwa tama wachukiza
Kila kitu unadanda, kingawa cha kuumiza
Huwi ndani ya kibanda, huishi kujitembeza
Uwache kuniumiza, ni heri mwana kunenda
a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka. Alama 2
b) Elza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa pili. Alama 3
c) Ni jambo lipi zuri ambalo atalikosa. Alama 2
d) Ni ila gani anayoiona kwa mpenziwe. Alama 2
e) I) shairi ni la bahari gani? Alama 2
ii) toa sababu alama 2
f) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya nathari. Alama 4
g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yaliyotumiwa katika shairi. Alama 3
I)mayaza
ii) sautiyo
III) muhibu
More Question Papers