Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Fasihi Ya Kiswahili Karatasi Ya 3 Question Paper

Fasihi Ya Kiswahili Karatasi Ya 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2009



1. USHAIRI - (LAZIMA)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali (Alama 20)
1. Hao miungu waliosimama kichaka
Wambieni wakae chini warefu kaeni chini
Wengi nyuma,hatuoni
Hatutaki vyenu vichafu visogo kuona kaeni chini miungu,
Kaeni chini miungu, kaeni chini.

2. Ndugu kaeni chini, kaeni chini ndiyo amri
Acheni acheni kelele kelele za jaza-tumbo
Kaeni chini!Tulonyuma kweli yatuchoma mioyo
Twataka chagua watu, watu watu
Mlipewa uongozi, ukawapaka rangi
Na madaraka,madaraka yakawalevya
Sasa yavueni wapisheni wenye nia!

3. Ama hamjaona hasira ikifura ya wengi watu
Ulizeni ya saidi aliyechomoa sokoni
Na ya Abdalla aliyegonga masikini?
Miungu, nanyi ndungu, chini pwetekeni
Tuwakanyage tupitie mbele tujisukume
Sisi twauza bidhaa ninyi mwauza maneno!
Tuko sawa haikai mdomoni.

4. Kateni yote misitu, fimbo tuenee
Na vinyago tuwachonge watoto wachezee
Kausheni yote maziwa maji tulowanishe
Kukipambazuka wasiweze ruka angani
Kokeni moto mashujaa wa uonevu tuwabanike
Kamwe hapatakuwa na kilio wala matanga
Bali hoi hoi za ushindi na madaraka kwa Umma.

Maswali
(a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka.( Alama 1)
(b) Taja maudhui ya shairi hili (Alama 2)
(c) Ni funzo gani linalojitokeza katika shairi hili (Alama 4)
(d) Taja na ueleze mkondo wa kishairi uliotumika katika shairi hili. (Alama 4)
(e) Fafanua matumizi ya tamathali za usemi katika kusawiri ujumbe kwenye shairi hili. (Alama 4)
(f) Andika ubeti wa kwanza kwa lugha nadhari (Alama 3)
(g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi. (Alama 2)
(i) Ikifura
(ii) Pwetekeni

RIWAYA
Jibu swali la 2 au la 3.
SAIDI A. MOHAMMED (UTENGANO)
2. 'Utengano' ni anwani mwafaka ya riwaya yake S. A. Mohammed. Thibitisha (Alama 20)
3. "Mkinipa mimi kura zenu nitajenga njia, nitawapa watu kazi,nitajenga skuli zaidi na maisha yenu yatakuwa katika raha."
(a) Eleza muktadha wa kauli hii (Alama 4)
(b) Msemaji ana dosari zipi zinazomfanya atoe ahadi hizi? (Alama 6)
(c) Onyesha namna wanasiasa walivyosawiriwa katika riwaya hii (Alama 10)

TAMTHILIA
Jibu swali la 4 au la 5
Kithaka wa Mberia: Kifo Kisimani
4. "Mateso ndiyo hewa wanayopumua wanabutangi." Thibitisha ukweli wa kauli hii. (Alama 20)
5. Kuna nini? Nilikutunza vizuri ulipokuwa askari wangu.
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili (Alama 4)
(b) Eleza mchango wa anayerejelewa katika ukombozi wa Butangi (Alama 8)
(c) Eleza sifa sita za anayezungumza (Alama 6)
(d) Mwandishi ametumia mbinu gani ya uandishi katika dondoo hili (Alama 2)

HADITHI FUPI
K.W.Wamitila (Mhariri)
Mayai waziri wa maradhi na hadithi nyingine.
6. Huku ukirejelea hadithi zozote tatu,onyesha vile diwani ya mayai waziri wa maradhi imeshughulikia swala la Taasubi ya kiume. (Alama 20)

FASIHI SIMULIZI
7. (a) Fafanua sifa zinazobainisha fasihi simulizi (Alama 10)
(b) Taja aina nne za nyimbo (Alama 4)
(c) Elezea dhima za methali (Alama 6)






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers