Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Rarieda-Kiswahili Paper 2 Question Paper

Rarieda-Kiswahili Paper 2 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2009



–Jina ……………………………………………… Namba yako ………………………………...
Shule ……………………………………………. Sahihi ya mtahiniwa ………………...……..
Tarehe ………………………………………

102/2
KISWAHILI
Karatasi ya 2
Lugha
Julai / Agosti 2009
Saa 2 ½






MTIHANI WA TATHMINI YA PAMOJA
WILAYA YA RARIEDA - 2009
HATI YA KUHITIMU KISOMO CHA SEKONDARI KENYA – (K.C.S.E.)

KISWAHILI
Karatasi ya 2
Lugha
Julai / Agosti 2009
Saa 2 ½





MAAGIZO:

Jibu maswali yote. Majibu yako yaandikwe katika nafasi zilizoachwa katika kijitabu hiki cha maswali.

Kwa Matumizi ya Mtahini Pekee
Swali Upeo Alama
1 15
2 15
3 40
4 10
JUMLA



Karatasi hii ina kurasa 10 zilizopigwa chapa
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo.


1. UFAHAMU
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuatia.
Vipindi mbalimbali vya historia vimeshuhudia kuibuka kwa magonjwa ya ajabu. Magonjwa hayo yamehangaisha watu na kuzishughulisha bongo za wanasayansi na madaktari katika kutafuta tiba. Magonjwa kama vile tauni, kifua kikuu, homa ya matumbo na ndui ni baadhi ya yale yaliyotisha sana nyakati fulani za historia ya binadamu. Magonjwa haya yaliwaua maelfu ya watu na kutibua mifumo na taratibu za maisha ya watu.
Hata hivyo magonjwa hayo yaliweza kuchunguzwa na kutafutiwa tiba kabla ya kumaliza kabisa kizazi cha binadamu. Lakini hii ni baada ya kuwasukuma maelfu ya watu kaburini. Ulimwengu wa sasa unashuhudia janga jingine la maradhi sugu ya Ukimwi. Neno “UKIMWI” lilitoholewa kutokana na athari za ugonjwa huo mwilini. Neno “UKIMWI” humaanisha Ukosefu wa Kinga Mwilini, ambapo herufi za kwanza za maneno matatu ziliunganishwa pamoja na kuunda neno hilo. Ugonjwa huu ambao tayari umewaua mamilioni ya watu kote ulimwenguni unazidi kuenea kwa kasi, mfano wa moto katika kichaka. Kutokana na kasi yake ya kuua watu, ugonjwa wa UKIMWI umepewa majina kama vile ‘umeme’ na pia ‘ugonjwa wa vijana’. Watu wengi wanaoambukizwa virusi vya UKIMWI ni wale walio na miaka kati ya 15 hadi 49. Kundi hili kwa kweli ndilo, linalohesabiwa kuwa na nguvu za kutunza jamii kwa njia nyingi. Iwapo wengi katika kundi hili watakumbwa na maradhi haya, watasalia wakongwe na watoto wasioweza kujimudu.
Nchini Kenya, UKIMWI uligunduliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 1984. Kufika mwezi wa Juni 1996, inakisiwa kuwa ugonjwa huu ulikuwa umewaua watu wapatao 65,647 nchini . Hivi sasa, inasemekana kuwa takriban watu zaidi ya 500 hufa kila siku nchini Kenya kutokana na janga hili. Aidha, imethibitishwa kwamba takriban wafu milioni mbili u nusu tayari watapoteza maisha yao kutokana na kuambukizwa virusi vya ugonjwa huu humu nchini. Maradhi haya sasa yamekuwa janga la kitaifa.
Kutokana na kuongezeka kwa visa vya UKIMWI, hospitali na zahanati nyingi kote nchini zinashindwa kukidhi mahitaji ya wagonjwa. Kwa hivyo makundi ya kujitolea na mashirika mbalimbali yameundwa ili kuwahudumia wagonjwa wa UKIMWI. Baadhi ya makundi hayo hutoa tiba ya kisaikolojia pamoja na kuwapa ushauri wa hima ya kuishi, badala ya kukata tamaa. Wagonjwa wengi pia huishia kutibiwa nyumbani kwao.
Lakini jambo la kuzingatia ni hili, tujifunze kutokana na historia. Tuwe na matumaini kwamba siku moja tiba ya ugonjwa huu itapatikana. Hii ni kwa sababu tumethibitishiwa haya kutoka katika historia yetu wenyewe. Ikiwa magonjwa yaliyosababisha vifo vya wengi kutokana na ukosefu wa tiba yalitokomezwa kupitia juhudi za kimatibabu, sembuse huu ugonjwa tulio nao sasa? Huku tukijikinga kutokana na maradhi haya tusife moyo bali tuwe na matumini kwani subira huvuta heri.

Maswali
a) Fafanua vifungu vifuatavyo (alama2)
i) Kutibua mifumo na taratibu za maisha ya watu.
………………………………………………………………………………..
………………………………………………………………………………..
………………………………………………………………………………..
ii) Kuwasukuma maelfu ya watu kaburini.
………………………………………………………………………………..
………………………………………………………………………………..
………………………………………………………………………………..
b) Eleza aina ya magonjwa yafuatayo:- (alama2)
i) Tauni
………………………………………………………………………………..
………………………………………………………………………………..
………………………………………………………………………………..
ii) Ndui
………………………………………………………………………………..
………………………………………………………………………………..
………………………………………………………………………………..
c) Kwa nini ugonjwa wa UKIMWI umepewa majina ya kimajazi (alama1)
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
d) Eleza madhara ya UKIMWI kulingana na taarifa (alama3)
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
e) Taja harakati zinazoendelezwa kukumbana na janga hili. (alama2)
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
f) Eleza mienendo inayopaswa kuendelezwa kuondoa kukata tamaa (alama3)
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika taarifa. (alama2)
i) Mifumo ………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………….
ii) Heri ………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………….
2. UFUPISHO
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuatia.
Ama kweli maisha ya vijana wa kisasa yanatofautiana na kuhitilafiana pakubwa na yale ya wazee wao. Sio katika mavazi, mienendo, mitazamo, mawazo na mielekeo tu bali pia katika kipengele kingine chochote utakachofikiria. Yote haya ni vielelezo vya jinsi kizazi cha leo kinavyoishi katika ulimwengu ambao ni kivuli tu cha ule wa vizazi vilivyotangulia. Baadhi ya watu wameieleza hali hii kuwa maisha sio jiwe. Kwao basi, si ajabu katu kuwaona vijana wakizungumza lugha yao ya kipekee au wakivaa nguo zinazobana ajabu na kudhihirisha bayana maungo yao badala ya kuyasitiri.
Hata hivyo, watu wengi wameonelea kwamba hali ya maisha ya vijana wa leo ni maasia yanayotokana na utundu na hata ukatili wao. Upande huu umetoa rai kwamba kizazi hiki kisingepotoka kama tu kingezingatia na kustahi utamaduni wa wahenga wao ambamo wazazi wao ndimo walimokulia. Wanazidi kufafanua kuwa nyendo hizi za miaka ya nyuma zilithamini sana amali kama uaminifu, heshima kwa wazee ama wakuu, bidii, ushirikiano, ukarimu, unyenyekevu, hadhari katika kila jambo, utiifu na pia kujitegemea. Yote haya yamesahaulika ama tuseme yamepuuzwa katika “utamaduni wa kisasa”.
Swali linalozuka sasa ni je, tunapaswa kuwahukumu vijana wa leo kwa kutumia vigezo au masharti gani? Tuwapige darubini kwa kutegemea hali ilivyo hivi leo duniani ama tuwapime kwa mujibu wa jinsi maisha ya baba na babu zao yalivyokuwa. Jibu la swali hili ni gumu na sharti lifafanuliwe kwa makini lisije likaegemea upande wowote.
Mathalan, ni jambo lisilopingika kuwa maisha ni utaratibu unaoathirika na hivyo kubadilika daima. Angalia kwa mfano jinsi maendeleo ya elimu, sayansi, mawasiliano na hata ufundi yalivyoyageuza maisha siku hizi. Yamkini vijana wa barani Afrika wakaona na hata kuzungumza kwa wenzao kutoka Uropa, Asia na Marekani bila hata kunyanyuka hapa kwao nyumbani. Athari ya filamu, video, vitabu, magazeti, majarida na kadhalika haikadiriki. Haya, kwa kiasi yamewafanya vijana hata kupevuka kabla ya wakati wao. Isitoshe, mambo haya yameweza kuwazuzua na kuwaaminisha ya kuwa yale wanayojifunza ni kweli. Matokeo yamekuwa ni wao kuudunisha utamaduni wao wa asili na kuupapia ule wa wageni waliowaathiri. Tusisahau kuwa ujana ni tembo la mnazi na rahisi kwao kubadili mawazo.
Lakini hatuwezi kuwasamehe vijana wanaokosa akili razini kwa kupotoshwa na kucharika na yote wanayoyapokea kutoka ugenini na hivyo kuanza kudhalilisha utamaduni wa Waafrika. Hata hivyo, badala ya kuwakashifu wanapopotea njia ama kuwapongeza wanapotenda yale tunayoyategemea tu, ni wajibu mkubwa wa wazazi kuwaongoza na kuwasaidia vijana kuwa na uwezo mkubwa na kufanya uteuzi mwafaka katika maisha yao.

Maswali
a) Bila kupoteza maana iliyokusudiwa na mwandishi wa kifungu, fanya muhtasari wa aya ya
kwanza na ya pili. (maneno 40) (alama 6, 1 ya utiririko)
Matayarisho
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
Nakala safi ……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….

b) Fupisha aya mbili za mwisho. (maneno 50) (alama 9, 1 ya utiririko)
Matayarisho
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….

Nakala safi
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………………….

3. MATUMIZI YA LUGHA
a) Taja sifa kuu za kutambulisha irabu i (alama1)
……………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………….
b) Tunga sentensi ukitumia vitenzi vifuatavyo:
i) Kitenzi kishirikishi kipungufu (alama2)
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
ii) Kitenzi kishirikishi kikamilifu
……………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………….
c) Tunga sentensi ukitumia kihusishi ‘katika’ kutoa dhana ya: (alama1)
Hali
……………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………….
d) Tunga sentensi moja yenye viungo vifuatavyo vya sarufi. (alama3)
i) Shina la kitenzi cha silabi moja
ii) Mnyambuliko wa kitenzi kauli ya kufanyia
iii) Kikanushi
iv) Kiwakilishi cha wakati uliopita
v) Mtendwa katika nafsi ya tatu umoja
vi) Kiima katika nafsi ya pili wingi
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
e) Eleza huku ukitoa mifano ya sentensi mwafaka kwa nini majina ya ngeli ya
KI- VI huitwa kitenzi – jina (alama2)
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
f) Tunga sentensi zenye mipangilio ifuatayo:- (alama2)
i) Kishazi tegemezi na kishazi huru
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………


ii) Kishazi huru na kishazi huru
……………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………….
g) Huku ukitoa mifano mwafaka eleza muundo wa majina ya ngeli ya A – Wa (alama5)
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
h) Tunga sentensi ukitumia viwakilishi vifuatavyo. (alama3)
i) Kiwakilishi nafsi huru
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
ii) Kiwakilishi nafsi kiambata
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
iii) Kiwakilishi ngeli
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
i) Tunga sentensi ukitumia vitenzi vifuatavyo katika kauli ya kufanyiza. (alama2)
i) La
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………

ii) Fa
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
j) Eleza matumizi ya KI katika sentensi ifuatayo (alama4)
Nyamunga na kitoto wamekuwa wakila wakiimba kikasuku
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
k) Tofautisha sentensi zifuatazo kimaana (alama2)
i) Diang’a amekula mkate wote
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………

ii) Diang’a amekula mkate wowote
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
l) Andika kivumishi kitokanacho na kitenzi kifuatacho (alama2)
i) Nyooka ………………………………………………………………………
ii) Ng’aa ………………………………………………………………………...
m) Tunga sentensi sahihi ukitumia visawe vya maneno yafuatayo (alama2)
i) Dalali …………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………..
ii) Dalili ………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………..






n) Changanua sentensi ifuatayo kwa vishale (alama3)
Watoto wote walitumwa ingawa wengine walibaki
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
o) Andika kwa msemo wa taarifa sentensi ifuatayo (alama2)
“Sisi hatutakubali kuchezewa leo namna hii.” Leo alisema
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
p) Andika sentensi ifuatayo katika udogo na ukubwa. (alama 2)
Nyoka na ndege hawakai katika nyumba moja.
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
q) i) Andika sentensi yakinishi kutokana na hii (alama1)
Chakula hakipikiki vizuri
……………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………….
ii) Geuza sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea huku ukiondoa amba (alama1)
Mtoto ambaye alikula ndiye ambaye alilia
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………











4. ISIMU JAMII
a) Eleza kwa kutoa mifano mwafaka tofauti zipatikanazo kati ya sajili ya maabadini na ya
wanahirimu (alama6)
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
b) Eleza sababu zozote nne ambazo huchangia kwa watu kuchanganya na
kuhamisha msimbo (alama4) ……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………………






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers