Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.
Nyamira-Kiswahili Paper 2 Question Paper
Nyamira-Kiswahili Paper 2
Course:Secondary Level
Institution: Mock question papers
Exam Year:2009
Jina ………………………………………………………… Nambari Yako ……………………
Shule ………………………………………………………. Sahihi ……………………………
102/2
KISWAHILI
Karatasi 2
(Lugha na Isimu -Jamii)
Julai / Agosti 2009
MUDA: Saa 2 ½
NYAMIRA DISTRICT SECONDARY SCHOOLS
JOINT EVALUATION TEST - 2009
Hati ya Kuhitimu Cheti cha Elimu ya Sekondari
102/2
KISWAHILI
Karatasi 2
(Lugha na Isimu -Jamii)
MUDA: Saa 2 ½
MAAGIZO:
• Andika jina lako na namba yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
• Tia sahihi yako ipasavyo.
• Jibu maswali yote.
• Majibu yako yaandikwe katika nafasi zilizoachwa.
KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE
SWALI UPEO ALAMA
1 15
2 15
3 40
4 10
JUMLA
Karatasi hii ina kurasa 9 ambazo zimepigwa chapa.
Mtahiniwa anashauriwa kuhakikisha kurasa zote hizo zimepigwa chapa sawasawa.
1. UFAHAMU
Soma makala yafuatayo ili ujibu maswali yanayofuata.
Ponografia ni tendo, maandishi, picha au michoro inayoonyesha au kueleza uchi wa mtu au vitendo vya ngono kwa ajili ya kuchochea ashiki ya kuifanya. Mambo haya machafu huwasilishwa ana kwa ana kupitia sinema, magazeti, vitabu, muziki, televisheni, tovuti na kanda za kunasia picha na sauti.
Ponografia imekuwepo tangu jadi, hasa katika nchi za magharibi. Lakini sasa limekuwa tatizo sugu. Hii ni kwa sababu imeenea kote ulimwenguni mithili ya moto mbugani wakati wa kiangazi. Kuenea kwake kumechangiwa na mambo kadha wa kadha. Mchango mkubwa zaidi ukiwa umetokana na kuimarika kwa vyombo vya teknolojia ya habari na mawasiliano. Matumizi ya tarakilishi, mdahilishi na viungambali vya picha yamesambaza ponografia ilivyoanza. Hata hivyo, kazi hii hubuniwa au kutengenezwa na makundi mbalimbali ya watu. Miongoni mwa hawa ni watu wasiojali maadili. Pili, kuna wale wenye matatizo ya kisaikolojia na kijamii. Wao hutengeneza na kueneza uchafu huu kwa lengo la kuvuruga maadili katika jamii au kuchukiza wanajamii waadilifu. Kundi lingine ni lile la wanaoichukulia ponografia kama nyenzo ya kutosheleza ashiki zao. Hivi sasa, kundi kubwa ni lile la wanaotumia matusi haya kama njia ya kuchuma. Kwa mfano, baadhi ya wanamuziki hutumia ponografia kuvutia wateja na hivyo kuzidisha mauzo yao.
Kushamiri kwa wimbi na uonyeshaji wa ponografia kuna athari kubwa kwa jamii hasa watoto. Ingawa watu wengine hudai picha hizi haziwaathiri, upo ushahidi kuonyesha kuwa wale wanaotazama picha za ngono hupata matatizo. Lazima ieleweke kwamba kinachoonekana kwa jicho au kusikika kwa sikio huathiri fikira au hisia. Picha za matusi zinachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu akili. Badala ya kuzingatia mambo muhimu kama vile masomo, watu huanza kutafakari mambo machafu.
Vijana wengi ni kama bendera, huyaiga wanayoyaona na kuyasikia. Hili ni tatizo linalowafanya kuacha mkondo wa maadili. Hivyo basi wengi hushawishiwa kuingilia shughuli za ngono mapema kabla hawajakomaa kimwili, kiakili na kihisia. Matokeo yake ni ukahaba, utendaji mbaya shuleni, mahudhurio mabaya darasani na mimba zisizotarajiwa. Vijana wengi huacha shule kabisa huku wengine wakiambukizwa magonjwa ya zinaa ambayo yanaweza kuwaletea mauti.
Yasemekana kuwa akili za binadamu hunasa zaidi mambo yanayowasilishwa kwa picha na hivyo basi matusi haya yaweza kudumishwa katika kumbukumbu zao. Tabia mbaya kama vile ushoga, ubasha na usagaji huwa matokeo yake na hata mielekeo ya vijana hugeuka wanapoanza kuiga mitindo mibaya ya mavazi yanayoanika uchi wao. Hali kadhalika, lugha, ishara na miondoko inayohusiana na ngono huibuka . Yote haya yanakinzana na desturi za Mwafrika. Si ajabu visa vya ubakaji vinaongezeka kuchapo. Utazamaji wa picha chafu aghalabu huandamana na maovu mengine kama vile unywaji pombe na matumizi ya vileo vingine ambavyo huchochea uchu wa ngono na kuibua tabia za kinyama. Kuendelea kuzitazama picha hizi huzifanya nishai na hisia za watu kuwa butu, huondoa makali kiasi kwamba hata katika utu uzima mtu hupoteza mhemko wa kawaida na kugeuzwa kuwa mtegemezi wa ponografia. Tatizo hili linaenea kwa vishindo mijini na vijijini. Ipo haja ya dharura kuikinga jamii kutokana na malezi haya yasiyo na kizuizi.
Kuuongeza ufahamu wa umma wote kuhusu uovu wa picha hizi, watu wazima kuwajibika kwa kuwalinda na kuwahimiza vijana kuhusu maovu haya na wale wenye midahilishi, video na sinema kutowaruhusu vijana kutazama uchafu huu kunaweza kuwa namna ya kuyakinga au hata kuyaepuka madhara ya ponografia. Ni sharti pia sheria izuie na kupiga marufuku utengenezaji na uenezaji wa upungufu huu. Bila shaka, sheria na hatua kali ziweze kuchukuliwa dhidi ya waivunjao. Hali kadhalika, wazazi wasijipweteke tu bali wawaelekeze watoto wao ipasavyo na kila mtu alitekeleze jukumu lake.
MASWALI
(a) Yape makala uliyosoma anwani mwafaka. (alama 1)
………………………………………………………………………………………………………
(b) Toa sababu za kusambaa kwa uchafu unaozungumziwa katika taarifa. (alama 3)
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..
……………………………………………………………………………………………………..
(c) ‘Bendera hufuata upepo’. Thibitisha ukweli wa usemi huu kulingana na makala. (alama 3)
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
(d) Ni kwa nini ni muhimu kuwakanya vijana dhidi ya uchafu huu? (alama 2)
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
(e) Ni hatua zipi zinazofaa kuchukuliwa dhidi ya aina ya uozo unaozungumziwa na mwandishi?
(alama 3)
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
(f) Fafanua msamiati huu kimuktadha. (alama 3)
i) uchu
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
ii) wasijipweteke
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
iii) nishai
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
2. UFUPISHO
Dhuluma kwa wanawake sio matokeo ya siasa baada ya uhuru, bali ni matokeo ya hali iliyokuwepo tangu enzi za mababu zetu; kabla ya ukoloni. Kubaguliwa na kudhulumiwa kwa wanawake kisiasa kunaoana na kunyonywa kwake kijamii kunakoshuhudiwa siku nenda miaka rudi.
Elimu ya jadi ilimwandaa mwanamke kuwa chombo kitiifu cha mwanamume.Mwanamke aliandaliwa katika unyago na katika mfumo mzima wa malezi kuwa chombo cha kumtumikia mwanamume-kumstarehesha, kumfariji, kumlisha na kumzalia watoto. Mwanamke tangu jadi hakuruhusiwa kushiriki katika shughuli za kisiasa na utawala wala hakuna mtu aliyeamini kwamba mwanamke angeweza kushikilia wadhifa wowote wa uongozi.
Demokrasia ya jadi naihusudu sana; ambapo wazee walikaa chini ya mbuyu na kuamua mambo ya jumuiya. Mahakama ya kijiji ilikuwa aghalabu ni ya wazee na wanaume peke yao. Hakukuwa na mwanamke aliyeshirikishwa, hata kama alikuwa ajuza. Sifa waliyokuwa nayo wanawake ni ile ya usihiri na uganga. Mwanamke yeyote aliyezeeka alidhaniwa kuwa bingwa wa uchawi, ulozi na ushirikina. Kwa hivyo, wanawake ndio waliokuwa washirikina wakubwa, maana fursa ya kupata elimu pana zaidi hawakuwa nayo. Si ajabu kuwa mwanamke alipojitokeza na kusema jambo la busara, alipuuzwa na pengine kutukanwa hadharani.
Kwa bahati nzuri, kumezuka mwamko uliotuingiza katika enzi mpya. Vita vya wanawake vya kujihami na kujiendeleza katika ulimwengu unaotawaliwa na wanaume vimetapakaa kote katika kila sehemu ya dunia. Wanawake wengi wamekiuka misingi na mizizi ya utamanduni na kung’oa asasi za kijamii na itikadi ambazo daima zimeendelea kumnyanyasa na kumuumbua utu mwanamke tangu jadi. Watetezi wa haki za wanawake zamani walilaumu suala la serikali za mataifa kutochukua hatua za utekelezaji wa maazimio yaliyoendelea kupitishwa na Umoja wa Mataifa mwaka hadi mwaka. Huku masuala ya wanawake ya kijamii, utu na utamaduni yakishangiliwa kupitishwa, watetezi wameeleza wasiwasi wao ikiwa kupitishwa kwa maazimio kutasaidia kuleta maendeleo ya haraka kwa wanawake kimataifa au katika nchi moja. Fauka ya hayo, baadhi ya wachunguzi wanaonelea kuwa rnaazimio mengi hayadokezi hatua za kufikiwa haki za wanawake.
Maazimio mengine yanazungumzia juu ya kuondolewa kwa ubaguzi dhidi ya wanawake, kushiriki kwao katika uendelezaji wa amani ya kimataifa na ushirikiano wa kimataifa, majukumu yao katika jamii, mfuko wa Umoja wa Mataifa wa wanawake (Unifem) na kuimarisha hadhi ya wanawake katika sekretariati ya Umoja wa Mataifa miongoni mwa shughuli nyingine katika mkabala huu.
Wanawake wameonyesha vipaji vyao katika nyanja mbalimbali za maisha; siasa, uchumi, utawala na kadhalika. Wanawake wamejikakamua na kudhihirisha kuwa wao pia wana jukumu muhimu la kutekeleza ili kuyaongoza maisha yao na ya watu wengine. Wadumishaji wa dhuluma za kijinsia hawana budi kusalimu amri na kuukubali ukweli huu, wapende wasipende. Mtazamo juu ya haki sawa unatokana na kukubaliwa na kuondolewa kwa aina zote za ubaya dhidi ya wanawake. Kwa bahati mbaya, itikadi na mila za kiasili bado hazitupi nafasi ya kuwashangilia wanawake wanaojitolea mhanga kutetea hadhi yao pamoja na ya wanyonge wengine. Wao huonekana kama waasi, wapinga mila na watovu wa utii.
(a) Bila kubadilisha maana asilia, fupisha aya tatu za kwanza. (Maneno 45 – 55) (alama 6, 1 ya utiririko)
Matayarisho
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………….
Jibu
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………….
(b) Kwa kurejelea aya tatu za mwisho, pambanua hoja muhimu zinazoguziwa na mwandishi. (Maneno 60 – 65) (alama 9, 2 za utiririko)
Matayarisho
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
Jibu
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………………………………………………………….
3. MATUMIZI YA LUGHA
(a) Sahihisha sentensi: (alama 2)
(i) Mitume hiyo siyo ambayo tunaijua.
……………………………………………………………………………………………….
(ii) Wasikilizaji sasa wanaburudika na muziki kutoka idhaa la taifa hii.
……………………………………………………………………………………………….
(b) Ikanushe sentensi hii katika umoja. (alama 2)
Wasingecheza kiustadi wasingeshinda katika michezo ile.
……………………………………………………………………………………………….
(c) Tambulisha nyakati na hali katika sentensi: (alama 2)
(i) Wachezaji walikuwa wanafanya mazoezi.
……………………………………………………………………………………………….………………………………………………………………………………………………
(ii) Nyang’ate alipoingia alitukemea.
……………………………………………………………………………………………….………………………………………………………………………………………………
(d) Eleza maana za sentensi. (alama 2)
(i) Kwa nini wasililie hapa?
……………………………………………………………………………………………….………………………………………………………………………………………………
(ii) Kwa nini wasilie hapa?
……………………………………………………………………………………………….………………………………………………………………………………………………
(e) Tambua ngeli za nomino zifuatazo. (alama 2)
(i) njama …………………………………………………………………
(ii) mate ……………………………………………………………………
(iii) meko ……………………………………………………………………
(iv) kiroboto …….……………………………………………………………
(f) Andika udogo na ukubwa wa neno ‘kidole’. (alama 2)
(i)……………………………………………(ii)……………………………………………………
(g) Tunga sentensi mbili tofauti kubainisha matumizi ya KWA. (alama 2)
(i)……………………………………………………………………………………………….……
(ii)…………………………….………………………...……………………………………………
(h) Onyesha shamirisho kipozi na kitondo katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
Msichana alimkaririra mgeni shairi.
(i) ……………………………………………………………………………………………
(ii)……………………………………………………………………………………………
(i) Tumia vitenzi hivi katika sentensi mojamoja katika jinsi ya kufanyiwa. (alama 2)
(i) nywa
……………………………………………………………………………………………….
(ii) pa
……………………………………………………………………………………………….
(j) Kistari kifupi ( - ) aghalabu hutumika kuendeleza sauti hasa katika vihisishi. Onyesha matumizi mengine matatu ya alama hii akifishi. (alama 3)
(i)…………………………………………………………………………………………………….
(ii)……………………………………………………………………………………………………(iii)…………………………………………………………………………………………………
(k) Tunga sentensi kubainisha tofauti kimaana kati ya vitawe: (alama 2)
(i) chuma
………………………………………………………………………………………………
(ii) jua
………………………………………………………………………………………………
(l) Ziandike upya sentensi hizi kwa mujibu wa maagizo uliyopewa. (alama 2)
(i) Kiyondi aliukomelea mlango alipovisikia vishindo.
(Anza kwa :Mlango…………………..)
………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………….
(ii) Mvua ilinyesha sana alasiri hiyo. Wachezaji walicheza mpira vizuri tu.
(Tumia ‘japo’)
………………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………….
(m) Tunga sentensi sahihi kubainisha matumizi ya KI kuonyesha: (alama 4)
(i) masharti
……………………………………………………………………………………………….
(ii) ngeli
……………………………………………………………………………………………….
(iii) kufanyika vitenzi viwili au zaidi wakati mmoja
……………………………………………………………………………………………
(iv) kielezi namna
…………………………………………………………………………………………….....
(n) Tambua hali na matumizi ya kisarufi ya neno lililopigwa mstari katika sentensi: (alama 1)
Mtu mzee anapaswa kuheshimiwa
………………………………………………………………………………………………….
(o) Andika katika usemi halisi. (alama 2)
Mwalimu aliwaagiza wanafunzi warudi darasani, warejelee madaftari yao ya kumbukumbu na kuikosoa kazi hiyo.
…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
(P) Andika katika umoja. (alama 2)
Tembe ambazo tulizimeza zilikuwa chungu.
……………………………………………………………………………………………………
(q) Eleza maana za semi au nahau: (alama 4)
(i) kwenda mbweu
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
(ii) shika sikio
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
(r) Toa jina mwafaka kwa maelezo. (alama 2)
(i) Nywele katika mikono na miguu ya binadamu.
………………………………………………………………………………………………
(ii) Mtu anayesukuma/anayekokota mkokoteni au rukwama.
………………………………………………………………………………………………
4. ISIMU - JAMII
(a) Eleza ukionyesha bayana tofauti baina ya lahaja na lafudhi. (alama 4)
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
(b) Taja sifa tambulizi za lugha ya misimu (alama 3)
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
(c) Orodhesha sifa kuu za sajili ya siasa. (alama 3)
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………
More Question Papers