Get premium membership and access revision papers, questions with answers as well as video lessons.

Rarieda District Kiswahili Paper 3 Question Paper

Rarieda District Kiswahili Paper 3 

Course:Secondary Level

Institution: Mock question papers

Exam Year:2009



102/3
KISWAHILI
Karatasi ya 3
FASIHI
Julai / Agosti 2009
Saa 2 ½






MTIHANI WA TATHMINI YA PAMOJA
WILAYA YA RARIEDA - 2009
HATI YA KUHITIMU KISOMO CHA SEKONDARI KENYA – (K.C.S.E.)

KISWAHILI
Karatasi ya 3
FASIHI
Julai / Agosti 2009
Saa 2 ½





MAAGIZO:
• Jibu maswali manne pekee
• Swali la kwanza ni la lazima
• Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki yaani: Tamthilia, Hadithi fupi, Ushairi na Fasihi Simulizi
• Usijibu maswali mawili kutoka katika sehemu moja.












Karatasi hii ina kurasa1 3 zilizopigwa chapa
Watahiniwa lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa sawa sawa na kuwa maswali yote yamo.






SEHEMU A: RIWAYA (S. A. MOHAMED – UTENGANO)
1. Thibitisha kuwa anwani ya “Utengano” ni anwani faafu kwa riwaya hii. (alama20)

SEHEMU B: HADITHI FUPI:
MAYAI WAZIRI WA MARADH NA HADITHI NYINGINE – K.W. WAMITILA
2. Kwa kurejelea hadithi ya “Fumbo la Mwana” thibitisha kuwa dawa za kulevya zina athari
kubwa kwa jamii. (alama20)
AU
3. Suala la haki za watoto limejitokeza waziwazi katika “Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi
Nyingine.” Kwa kurejelea hadithi zozote tatu, onyesha ukweli wa kauli hii. (alama20)

SEHEMU C: TAMTHILIA (KITHAKA WA MBERIA – KIFO KISIMANI)
4. “Wewe ni mzalendo thabiti kama wanabutangi wengine. Wewe ni mpenda amani na utulivu kama
wazalendo wengine wa Butangi. Wewe si mtu mbaya.”
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama4)
b) Taja na ufafanue maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili (alama6)
c) Eleza sifa za msemaji na msemewa (alama10)
AU
5. Jumuiya ya Kifo Kisimani ni ya watu walionyimwa mengi. Fafanua. (alama20)

SEHEMU D: FASIHI SIMULIZI
6. a) Fafanua sifa tatu za kila mojawapo ya vipera vya fasihi simulizi vifuatavyo (alama6)
i) Vitendawili
ii) Methali
b) Mawaidha yana dhima gani katika jamii? Eleza. (alama6)
c) Bainisha sifa za nyimbo. (alama4)
d) Eleza umuhimu wa nyimbo za kisiasa (alama4)

SEHEMU E: USHAIRI
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
1. Hayawani nondokeya, nondokeya nenda mbali
Melaniwa huna haya, leo haja kukabili
Kimbiya nenda Ulaya, upi ndo wako usuli?
Umbakaji haini.

2. Watoto waulizani, changudoa mekushinda?
Umezua vya uhuni, kuyachafua makinda
Pinga kama si punguani, adilifu mekushinda
Umbakaji haini.




3. Wahanyahanya yayaya, mitaani patupatu
Matendoyo kubwayaya, umewasinya wenetu
Nairobi na Siaya, kote kote lithubutu
Umbakaji haini

4. Jogoo kuparagia, kifaranga ni halali?
Ukimwi wawapatia, huna akili kamili
Nakutungia sheria, takufunga ukubali
Umbakaji haini.

MASWALI
a) Lipe shairi hili anwani mwafaka. (alama1)
b) Shairi hili ni la bahari gani? Thibitisha jawabu lako. (alama4)
c) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa pili. (alama2)
d) Taja na ueleze tamathali za lugha tatu alizotumia mshairi. (alama3)
e) Andika ubeti wa nne kwa lugha ya nathari. (alama4)
f) Taja matendo yoyote matatu mabaya ya anayesemwa. (alama3)
g) Eleza jinsi mshairi alivyotumia uhuru wake wa utunzi. (alama3)






More Question Papers


Popular Exams


Mid Term Exams

End Term 1 Exams

End Term 3 Exams

Opener Exams

Full Set Exams



Return to Question Papers