Maazimio mengine yanazungumzia juu ya kuondolewa kwa ubaguzi dhidi ya wanawake, kushiriki kwao katika uendelezaji wa amani ya kimataifa na ushirikiano wa kimataifa, majukumu yao katika jamii,...

      

Maazimio mengine yanazungumzia juu ya kuondolewa kwa ubaguzi dhidi ya wanawake,
kushiriki kwao katika uendelezaji wa amani ya kimataifa na ushirikiano wa kimataifa,
majukumu yao katika jamii, mfuko wa Umoja wa Mataifa wa wanawake (Unifem) na
kuimarisha hadhi ya wanawake katika sekretariati ya Umoja wa Mataifa miongoni mwa
shughuli nyingine katika mkabala huu.
Wanawake wameonyesha vipaji vyao katika Nyanja mbalimbali za maisha; siasa, uchumi,
utawala na kadhalika. Wanawake wamejikakamua na kudhihirisha kuwa wao pia wana jukumu
muhimu la kutekeleza ili kuyaongoza maisha yao na ya watu wengi. Wadumishaji wa dhuluma
za kijinsia hawana budi kusalimu amri na kuukubali ukweli huu, wapende wasipende.
Mtazamo juu ya haki sawa unatokana na kukubaliwa na kuondolewa kwa aina zote za ubaya
dhidi ya wanawake wanaojitolea mhanga kutetea hadhi yao pamoja na ya wanyonge wengine.
Wao huonekana kama waasi, wapinga mila na watovu wa utii.
b) Kwa kurejelea aya mbili za mwisho, eleza maswali muhimu anayoibua mwandishi
(maneno 60 -65)

  

Answers


kinyua
b) – Maazimio mengine yanazungumzia kuondolewa kwa ubaguzi dhdi ya wanawake
- Pia kushiriki kwao katika kuendeleza amani na ushirikiano wa kimataifa
- Yanazungumzia majukumu yao katika jamii na mfuko wa UNIFEM na kuimarisha hadhi ya
wanawake
- Wanawake wameonyesha vipaji vyao katika Nyanja tofauti
- Wamedhihirisha kuwa wana jukumu muhimu la kutekeleza
- Mtazamo kuhusu haki sawa unatokanana kukubaliwa na kuondolewa kwa ubaya wote dhidi ya
wanawake wanaotetea hadhi ya wanyonge
monica20 answered the question on October 10, 2017 at 15:04


Next: Who is the longest serving president in the world?
Previous: Eleza maana ya mofimu

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions