Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Watu wengine hawawezi kunywa chai au uji bila kutia sukari. Wanatumia sukari kwa hamu na ghamu...

      

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Watu wengine hawawezi kunywa chai au uji bila kutia sukari. Wanatumia sukari kwa hamu na
ghamu bila kutambua kuwa hiyo ni sumu wanayojiongezea mwilini.
Ni ukweli usiopingika kuwa wazee wa jadi waliishi muda mrefu wakiwa na siha njema kuliko sisi. Hii
ni kwa kuwa waliishi katika kipindi ambacho sukari inayotengenezwa viwandani. Iwapo ilikuweko,
ilikuwa bidhaaa ya wateule waungwana kutengenezea vitu kama keki, mahamri, vitumbua na
kadhalika na akina yahe hawangeweza kuigharamia.
Watafiti wa maswali ya afya wamegundua kuwa sukari inayotayarishwa viwandani sasa haina
virutubiushi vyovyote. Hali kadhalika, utaratibu wa viwandani wa kutayarisha sukari ili iwe nyeupe
na kuichuja huharibu virutubishi vinavyoweza kuwa muhimu mwilini. Umuhimu wa sukari
wakausaza kwa kutia ladha tamu tu. Umuhimu huu hauwezi kulinganishwa na madhara
yanayoletwa na sukari hii. Baada ya kusagika mwilini, sukari hii huacha masalio ya aside mwilini
yenye sumu inayoathiri siha.
Matumizi ya sukari kwa wingi husababisha madhara mbalimbali mwilini. Kwanza, huchangia kuoza
na kuharibika kwa meno pamoja na matatizo ya meno kuuma. Pili, sukari nyeupe imehusishwa na
ongezeko la maradhi ya kisukari, moyo na hipoglisimia au upungufu wa sukari mwilini. Matumizi
holela ya sukari huleta kipandauso au ugonjwa wa ghafla wa kuumwa upande mmoja wa kichwa
unaoambatana na kichefuchefu, kutapika na matatizo ya kuona. Pia, sukari huleta maradhi ya
ngozi na figo, pamoja na ongezeko la kemikali iitwayo kolestroli, ambayo ni ufuta unaonata na
ambao unatokana na kutoyeyuka kwa mafuta yote mwilini. Kemikali hii ya kolestroli
inaporundikana moyoni, hufanya mishipa inayotoa damu moyoni na kuisambaza mwilini kuwa
myembamba na sugu. Moyo hulazimika kusukuma damu kwa nguvu na huenda moyo ukachoka na
kukoma kufanya kazi.
Madhara haya ya sukari ndiyo yanayowafanya watu wengi kukiri kuwa sukari, ingawa ni tamu, ni
sumu mwilini. Wataalamu wa lishe wamependekesa ulaji wa vyakula ka nafaka, matunda, mboga
na miwa ambavyo vimejaa sukari asilia.
Fauka ya hayo, sukari inayotoka katika asali ni bora zaidi kwa mwili wa mwanadamu. Asali huwa
na sukari asilia, vitamin, madini na amino aside. Hivi vyote huwa na manufaa mbalimbali mwilini.
Mathalani, asali huupa mwili nishati inayohitajika kuendesha shughuli za viungo. Licha ya hayo,
asali huuchangamsha mwili. Asali huwa na kemikali ambazo husaidia watoto kukua vizuri. Huwezi
kuzidisha kiwango cha hemoglobini, hivyo kupunguza uwezakano wa watoto kuwa na anaemia
(upungufu wa damu). Halikadhalika, asali husaidia katika usagaji wa chakula iwapo itatumiwa
kabla ya mlo. Matumizi ya kijiko kimoja cha asali kila siku husaidia mwili kujikinga dhidi ya
magonjwa ya kukohoa. Asali husaidia pia kuondoa harufu mbaya kinywani.
Asali pia inaweza kutumiwa kujipaka. Inapotumiwa kwa njia hii, hutunza ngozi na kuifanya ing’are,
huondoa vipele na ugumu wa ngozi, pamoja na kutibu kule ngozi ilikokatikatika. Halikadhalika,
asali hutibu vidonda. Viwanda vingi vya vipodozi vilevile hutumia asali kama malighafi muhimu
katika utengenezaji wa bidhaa hizo.
a) Kutokana na taarifa hii, kwa nini wazee wa zamani waliishi muda
mrefu wakiwa na siha njema kuliko watu wa siku hizi?
b) Taja matumizi mawili ya sukari nyeupe.
c) Onyesha madhara matatu ya sukari nyeupe mwilini.
d) Taja aina ya sukari iliyo na manufaa mwilini mwa mwanadamu au ueleze ni kwa nini.
e) Eleza manufaa ya asali:
i) Ndani ya mwili
ii) Nje ya mwili
f) Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika taarifa:
i) Hamu na ghamu
ii) Akina yahe
iii) Sugu
iv)Vipodozi

  

Answers


kinyua
(a)Wazee hao hawakutumia sukari nyeupe, kwa hivyo hawakujiongezea mwilini au waliishi katika
kipindi ambacho sukari inayotengenezwa viwandani haikuweko.
b) (i) Hutumika katika vinywaji kama uji na chai.
(ii)Hutumika kupika vyakula kama keke au mahamri
(c) (i) Huchangia kuoza na kuharibika kwa meno pamoja na matatizo ya meno kuuma.
(ii) Husababisha maradhi ya kisukari, moyo na hipoglisimia.
(iii) Huleta maradhi ya ngozi, figo na ongezeko la kolestroli, ambayo ni kemikali hatari mwilini.
(iv) Huleta kipandauso; ugonjwa wa ghafla wa kuumwa na kichwa upande mmoja.
(d) Sukari yenye manufaa ni ya asilia itokanayo na vyakula kama nafaka, matunda, mboga na
miwa na asali kwa sababu huwa na virutubishi vimejaaa sukari asilia)
(e) (i) Ndani ya mwili
a) Huupa mwili vitamin, madini na amino asidi.
b) Huupa mwili nishati.
c) Huchangamsha mwili/husaidia usagaji wa chakula/husaidia mwili kujikinga na maradhi kama
homa/huzidisha kiango cha himoglobini na kupunguza uwezekano wa watoto wadogo kupata
anemia/husaidia pia kuondoa harufu mbaya kinywani.
(ii) Nje ya mwili
d) Hufanya ngozi kung’ara/huondoa vipele na ugumu wa ngozi/hutibu kule ngozi imekatika
katika/na vidonda vilivyotokana na kuchomeka (kujipaka kutibu vidonda)
(f) (i) Hamu na ghamu- kutarajia ukiwa na tama kubwa, shauku, uchu.
(ii) Akina yahe – Watu wa kawaida, watu wa tabaka la chini, maskini, fukara, wakati walahoi.
(iii) Sugu – ngumu (iv) Vipodozi – vitu au bidhaa za kurembesha k.m. mafuta na poda.
monica20 answered the question on October 12, 2017 at 15:24


Next: Explain two types of user interfaces in a computer system
Previous: Define the term 'incomplete records'.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions