Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali Jambazi wa kimataifa ni tatizo lililowasumbua walimwengu kwa muda mrefu sana. Serikali nyingi zimetumia mapesa mengi kwa miaka...

      

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Jambazi wa kimataifa ni tatizo lililowasumbua walimwengu kwa muda mrefu sana. Serikali nyingi
zimetumia mapesa mengi kwa miaka mingi sana zikijitahidi kupambana na janga hili. Hata hivyo,
fanaka haijapatikana, wala haielekei kamwe itapatikana leo au karne nyingi baadaye.
Yamkini tatizo kubwa lililopo ni kuhusu jelezi la dhana ya “ujambazi” tena “tena “wa kimataifa”.
Hili ni tatizo mojawapo na yapo mengi sana. Tatizo la pili ni kiburi. Kuna wale watu binafsi na hasa
viongozi wa nchi kubwakubwa na serikali zao zilizojiaminisha kuwa ujambazi ni balaa kweli, tena
belua, lakini huo ni wa huko, wala hauwezi kuwagusa licha ya muwashtua wao.
Kulingana na maoni ya watakaburi hao,ujambazi ni wa watu ‘washenzi’ wasiostaarabika,
wapatikanao katika nchi zisizoendelea bado. Ujambazi pekee wanaouona unafaa kukabiliwa ni
dhidi ya mbubujiko wa madawa ya kulevya uliosababishwa na vinyangarika kutoka nchi hizo
maalum za ‘’ ulimwengu wa tatu” . Kulingana na wastaarabu wa nchi zilizoendelea, vinyangarika
hivi ndivyo hasa adui mkubwa wa ustaarabu ulimwenguni na ni sharti vifagiliwe mbali bila huruma.
Baada ya kusagwa sagwa, ulimwengu mstaarabu utazidi kutononoka na ahadi ya mbingu hapa
ardhini itakamilika.
Imani ya watu ya kuwa ujambazi wa kimataifa, hata iwapo upo, hauwezi kuwashtua wala
kuwatingisha wao ilikuwa kamili na timamu. Ilikuwa kamili na timamu hadi hapo mwezi Septemba
tarehe 11 mwaka wa 2001, ndege tatu za abiria zilipoelekezwa katika majumba mawili ya fahari,
yenye urefu wa zaidi ya ghorofa mia moja na kuyatwangilia mbali. Mshtuko na kimako! Kimako
kwa kuwa, kabla ya siku hiyo, wamarekani hawangeweza kudhani kwamba ingewezekana taifa
lolote au mtu yeyote kuthubutu kuishambulia nchi yao. Taifa wasifa lililojihami barabara dhidi ya
aina yoyote ile ya uchokozi kutoka pembe lolote la dunia.
Hakuna ulimwenguni mzima, aliyeamini kuwa Marekani ingeweza kushambuliwa. Kwa ajili hiyo,
mshtuko uliitingisha ardhi yote na huzuni ilitanda kote, kama kwamba sayari nzima
imeshambuliwa, wala sio Marekani pekee.
Mintarafu hiyo, Marekani ilipolipiza kisasi kwa kuwaunguza waliokuwemo na wasiokuwemo kwa
mabomu hatari huko Afghanistan, idadi kubwa ya watu duniani ilishangilia na kusheherekea. Kwa
bahati mbaya, tafsiri ya shambulizi la minara – picha ya Newyork na lile la Pentagon, uti wa uwezo
wa kivita wa Marekani, ilizorota. Kuna wengi waliodhani huo ni mwanzo wa vita vya Waislamu dhidi
ya Wakristo na kwa muda, Waislamu wote wakashukiwa kimakosa kuwa ni majambazi wa
kimataifa.
Ukizingatia aya tatu za mwisho, fafanua fikira za watu na mambo yote yaliyotokea baaada ya
Septemba tarehe 11, 2001 (Maneno 65 -75)

  

Answers


kinyua
-Baada ya tarehe hiyo kulikuwa na kimako/mshtuko kwa wamerikani.
-Hakuna ulimwenguni mzima aliyeamini kuwa Marekani ingeweza kushambuliwa.
-Mshtuko au kimako na huzuni zilitanda ulimwenguni mzima/kote ardhini AU mshtuko ulitingiza
ardhi yoe kukawa na kimako na huzuni.
-Marekani ililipiza kisasi kwa kuwaunguza waliokuwemo na wasiokuwemo kwa mabomu kule
Afghanistani.
-Kulikuwa na kusheherekea/idadi kubwa ya watu ilishangilia na kushehereka shambulizi la
Marekani.
-Tafsiri ya shambulizi hili ilizorota.
-Wengi walidhani huo ni mwanzo w avita vya waislamu dhidi ya wakristo.
-Waislamu wote wakashukiwa kimakosa kuwa ni majambazi wa kimataifa.
monica20 answered the question on October 12, 2017 at 15:28


Next: Outline three types of computer operating systems that you know
Previous: Huku ukitoa mfano mmoja mmoja taja makundi mawili ya sauti.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Watu wengine hawawezi kunywa chai au uji bila kutia sukari. Wanatumia sukari kwa hamu na ghamu...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
    Watu wengine hawawezi kunywa chai au uji bila kutia sukari. Wanatumia sukari kwa hamu na
    ghamu bila kutambua kuwa hiyo ni sumu wanayojiongezea mwilini.
    Ni ukweli usiopingika kuwa wazee wa jadi waliishi muda mrefu wakiwa na siha njema kuliko sisi. Hii
    ni kwa kuwa waliishi katika kipindi ambacho sukari inayotengenezwa viwandani. Iwapo ilikuweko,
    ilikuwa bidhaaa ya wateule waungwana kutengenezea vitu kama keki, mahamri, vitumbua na
    kadhalika na akina yahe hawangeweza kuigharamia.
    Watafiti wa maswali ya afya wamegundua kuwa sukari inayotayarishwa viwandani sasa haina
    virutubiushi vyovyote. Hali kadhalika, utaratibu wa viwandani wa kutayarisha sukari ili iwe nyeupe
    na kuichuja huharibu virutubishi vinavyoweza kuwa muhimu mwilini. Umuhimu wa sukari
    wakausaza kwa kutia ladha tamu tu. Umuhimu huu hauwezi kulinganishwa na madhara
    yanayoletwa na sukari hii. Baada ya kusagika mwilini, sukari hii huacha masalio ya aside mwilini
    yenye sumu inayoathiri siha.
    Matumizi ya sukari kwa wingi husababisha madhara mbalimbali mwilini. Kwanza, huchangia kuoza
    na kuharibika kwa meno pamoja na matatizo ya meno kuuma. Pili, sukari nyeupe imehusishwa na
    ongezeko la maradhi ya kisukari, moyo na hipoglisimia au upungufu wa sukari mwilini. Matumizi
    holela ya sukari huleta kipandauso au ugonjwa wa ghafla wa kuumwa upande mmoja wa kichwa
    unaoambatana na kichefuchefu, kutapika na matatizo ya kuona. Pia, sukari huleta maradhi ya
    ngozi na figo, pamoja na ongezeko la kemikali iitwayo kolestroli, ambayo ni ufuta unaonata na
    ambao unatokana na kutoyeyuka kwa mafuta yote mwilini. Kemikali hii ya kolestroli
    inaporundikana moyoni, hufanya mishipa inayotoa damu moyoni na kuisambaza mwilini kuwa
    myembamba na sugu. Moyo hulazimika kusukuma damu kwa nguvu na huenda moyo ukachoka na
    kukoma kufanya kazi.
    Madhara haya ya sukari ndiyo yanayowafanya watu wengi kukiri kuwa sukari, ingawa ni tamu, ni
    sumu mwilini. Wataalamu wa lishe wamependekesa ulaji wa vyakula ka nafaka, matunda, mboga
    na miwa ambavyo vimejaa sukari asilia.
    Fauka ya hayo, sukari inayotoka katika asali ni bora zaidi kwa mwili wa mwanadamu. Asali huwa
    na sukari asilia, vitamin, madini na amino aside. Hivi vyote huwa na manufaa mbalimbali mwilini.
    Mathalani, asali huupa mwili nishati inayohitajika kuendesha shughuli za viungo. Licha ya hayo,
    asali huuchangamsha mwili. Asali huwa na kemikali ambazo husaidia watoto kukua vizuri. Huwezi
    kuzidisha kiwango cha hemoglobini, hivyo kupunguza uwezakano wa watoto kuwa na anaemia
    (upungufu wa damu). Halikadhalika, asali husaidia katika usagaji wa chakula iwapo itatumiwa
    kabla ya mlo. Matumizi ya kijiko kimoja cha asali kila siku husaidia mwili kujikinga dhidi ya
    magonjwa ya kukohoa. Asali husaidia pia kuondoa harufu mbaya kinywani.
    Asali pia inaweza kutumiwa kujipaka. Inapotumiwa kwa njia hii, hutunza ngozi na kuifanya ing’are,
    huondoa vipele na ugumu wa ngozi, pamoja na kutibu kule ngozi ilikokatikatika. Halikadhalika,
    asali hutibu vidonda. Viwanda vingi vya vipodozi vilevile hutumia asali kama malighafi muhimu
    katika utengenezaji wa bidhaa hizo.
    a) Kutokana na taarifa hii, kwa nini wazee wa zamani waliishi muda
    mrefu wakiwa na siha njema kuliko watu wa siku hizi?
    b) Taja matumizi mawili ya sukari nyeupe.
    c) Onyesha madhara matatu ya sukari nyeupe mwilini.
    d) Taja aina ya sukari iliyo na manufaa mwilini mwa mwanadamu au ueleze ni kwa nini.
    e) Eleza manufaa ya asali:
    i) Ndani ya mwili
    ii) Nje ya mwili
    f) Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika taarifa:
    i) Hamu na ghamu
    ii) Akina yahe
    iii) Sugu
    iv)Vipodozi

    Date posted: October 12, 2017.  Answers (1)

  • Nomino zifuatazo ziko katika ngeli gani? (i)Makamasi (ii)Boga(Solved)

    Nomino zifuatazo ziko katika ngeli gani?
    (i)Makamasi
    (ii)Boga

    Date posted: October 12, 2017.  Answers (1)

  • Eleza matumizi mawili ya parandesi kama alama za uakifishaji.(Solved)

    Eleza matumizi mawili ya parandesi kama alama za uakifishaji.

    Date posted: October 11, 2017.  Answers (1)

  • Eleza thana ya nomino za pekee.(Solved)

    Eleza thana ya nomino za pekee.

    Date posted: October 11, 2017.  Answers (1)

  • Eleza matumizi matatu ya kikomo huku ukitolea mifano mwafaka.(Solved)

    Eleza matumizi matatu ya kikomo huku ukitolea mifano mwafaka.

    Date posted: October 11, 2017.  Answers (1)

  • Ni nini umuhimu wa kusanifisha lugha ya Kiswahili?(Solved)

    Ni nini umuhimu wa kusanifisha lugha ya Kiswahili?

    Date posted: October 10, 2017.  Answers (1)

  • Usanifishaji wa lugha ni nini?(Solved)

    Usanifishaji wa lugha ni nini?

    Date posted: October 10, 2017.  Answers (1)

  • Ala tuli ni nini?(Solved)

    Ala tuli ni nini?

    Date posted: October 10, 2017.  Answers (1)

  • Kanusha sentensi hii kwa kutumia kiwakilisho amba (alama 2) Ubao upakwao rangi hupendeza(Solved)

    Kanusha sentensi hii kwa kutumia kiwakilisho amba (alama 2)
    Ubao upakwao rangi hupendeza

    Date posted: October 10, 2017.  Answers (1)

  • Unda nomino mbili kutokana na neno hudumu(Solved)

    Unda nomino mbili kutokana na neno hudumu

    Date posted: October 10, 2017.  Answers (1)

  • Tambua chagizo Ninaenda Nakuru lakini nitarudi saa moja(Solved)

    Tambua chagizo
    Ninaenda Nakuru lakini nitarudi saa moja

    Date posted: October 10, 2017.  Answers (1)

  • Bainisha matumizi ya ‘ni’ katika sentensi ifuatayo: Twendeni tuone mhubiri ni nani?(Solved)

    Bainisha matumizi ya ‘ni’ katika sentensi ifuatayo:
    Twendeni tuone mhubiri ni nani?

    Date posted: October 10, 2017.  Answers (1)

  • Kanusha Mwanafunzi hodari apongezwa na rais.(Solved)

    Kanusha
    Mwanafunzi hodari apongezwa na rais.

    Date posted: October 10, 2017.  Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo katika kauli ya kutendama Habari za kifo chake zilifichwa(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika kauli ya kutendama
    Habari za kifo chake zilifichwa

    Date posted: October 10, 2017.  Answers (1)

  • Andika katika usemi halisi Afisa alitaka kujua idadi ya mahabusu ambao wangeachiliwa keshoye.(Solved)

    Andika katika usemi halisi
    Afisa alitaka kujua idadi ya mahabusu ambao wangeachiliwa keshoye.

    Date posted: October 10, 2017.  Answers (1)

  • Tunga sentensi ukitumia neno ‘kinanda’ kisha ubainishe ngeli yake.(Solved)

    Tunga sentensi ukitumia neno ‘kinanda’ kisha ubainishe ngeli yake.

    Date posted: October 10, 2017.  Answers (1)

  • Andika kwa udogo Nguo yake iliraruliwa na mbwa mkorofi.(Solved)

    Andika kwa udogo
    Nguo yake iliraruliwa na mbwa mkorofi.

    Date posted: October 10, 2017.  Answers (1)

  • Yakinisha Usipojibu swali hii utawaudhi wengi.(Solved)

    Yakinisha
    Usipojibu swali hii utawaudhi wengi.

    Date posted: October 10, 2017.  Answers (1)

  • Andika kwa wingi: Ugomvi ulipozuka pale ulimi wake ulipatapata.(Solved)

    Andika kwa wingi:
    Ugomvi ulipozuka pale ulimi wake ulipatapata.

    Date posted: October 10, 2017.  Answers (1)

  • Kanusha sentensi ifuatayo: Chakula ambacho kimepikwa sasa kisingalinunuliwa jana kisingaliiva mapema.(Solved)

    Kanusha sentensi ifuatayo:
    Chakula ambacho kimepikwa sasa kisingalinunuliwa jana kisingaliiva mapema.

    Date posted: October 10, 2017.  Answers (1)